Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 11,208
- 20,517
Unanifahamu mzuka mzee baba napenda hayo makitu mbaya kabisa🤗🤗Biashara ya mirungiiii. [emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787] to arusha
Sent using Jamii Forums mobile app
Unanifahamu mzuka mzee baba napenda hayo makitu mbaya kabisa🤗🤗Biashara ya mirungiiii. [emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787] to arusha
Sent using Jamii Forums mobile app
Wala usijali mkuu maana mm wala sijutii lile lilikua daraja la kunifikisha nilipo sasaSo sorry brother
Sometimes mtu unaweza hisi maisha yamekupiga ila ukitoka na kusikiliza wengine unapata kila sababu ya kumshukuru Mungu
Binafsi maisha yalinipiga ila si kwa kukosa vocha ama chakula ama nauli ila ni kwa kile nilichoamini napaswa kufikia ktk maisha bila ya kuajiriwa
Hivyo nilikataa nafasi kadhaa za kuajiriwa hapo naelekea kumaliza chuo July 2018 bro wangu akiwa na cheo kampuni x ya utalii akaniambia kuna nafasi maliza chuo uje upige kazi temporal kama store keeper bila chenga nikamchana sitaki kuajiriwa,,, metoka chuo direct ifakara kulima mpunga huko sikurudisha hata mia katikati hapo nikiusubiria mpunga nikauza sana mayai ya kuchemsha na sambusa... by dec 2018 nikawa na uhakika dili la mpunga lishabuma na mebaki sina hata mia pamoja na wenzangu tukapata idea ya kulima maharage Gairo tukaweka mipango sawa then nikarudi home maza alikuwa mgonjwa sana home pale nikaungaunga mixer kuomba nikapata laki 6 nikatoa washikaji wakakodi mashamba na hiyo hiyo ikatosha hadi kwenye mavuno tulikodi heka 20... Wakati wa mavuno wenzangu wakawa na harakati nyingine za hapa na pale mi ikawa ndio wajibu wangu kwenda kusimamia uvunaji huko huko nikasoma gap la kununua maharage kwa wakulima na kuyapeleka town kuuza mixer nilifanya juu chini yetale mashamba ya pamoja nikavuna fasta na kuuza ile hela nikawa nazungushia kununua na kuuza + 2m niliyoomba home kusema kweli ile biashara haina hasara na hela niliiona kiasi chake kilichonikwamisha niliuugua kama mwezi nipo hoi hivyo nilivyopoona msimu ukawa ndio unaishia na hela ya shamba tukagawana ila nikawa bado na chenchi za kuendelea kununua gunia kadhaa na kupeleka town... By sept 2019 nikapata fursa ya kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara ya nafaka ulioitishwa na waziri wa kilimo hapo niliziona fursa kibao na nikapata motisha wa kurudi shamba kupambana upya... Nilirudi ila msimu ulikuwa umefika mwisho haswaa maharage hamna target ikawa ni kusubiria ya mtukula Uganda nikiwaza kwenda huko na shs 3m zangu naona haitoshi ila nikizungumza na watu wananiambia inatosha sana kibaya hapo ni October na msimu unaanza DEC kuelekea January halo nilipata stress na hofu ya kuitumia pesa kutokana na kukosa mzunguko hadi ikafikia hatua ya kuomba kibarua ili nijipange kwa msimu utakaokuja...
Mungu mkubwa kabla ya kupata hicho kibarua ikatokea mama mmoja aliyekuwa ktk ule mkutano tumefahamiana kwa bahati mbaya tu yaan ilitokea mekosea namba nikimtafuta mtu mwingine aliyehit ktk ule mkutano ambae nae alikuwa akimtafuta pia basi nikampa mawasiliano yake mixer story tukajuana na nikawa nampigia kumuuliza feedback kama amefanikiwa kupata msaada toka kwa yule mtu... Siku ya siku nawaza kurudi home akaniambia nina shida sana ya mahindi fanya kunitafutia yeye anasaga sembe na dona nikaingia machaka kadhaa mwisho nikapata chimbo la mahindi na kuyasafirisha hadi dsm kusema kweli baada ya kuanza hiyo biznez upepo ulichange na stress zikanipungua maana nilifikia hatua ya kufata vyeti chuo ili nikaombe kazi... Huu ni ufupisho wa ufupisho sababu niliyofanya na kuyapanga hapo ktkt ni mengi siwezi andika yote ikiwa ni pamoja na kupoteza hela na muda kwenye drop shipping kupitia darasa lililoanzishwa na bwana frank frain Byera Deo Corleone
Mpaka sasa msimu umeisha ila namshukuru Mungu mepata network kubwa dsm na mtaji umekuwa ghafla toka kusafirisha mahindi tani 5 hadi 11 hapa kuna pesa fulani niliomba nikaongezea kwenye mtaji na kupitia hili zao najiona nikitengeneza pesa ya maana mwaka huu... Mungu tu ajalie na kuepusha balaa yoyote
#2020 twenty twenty, twenty plenty
😂😂
Tutaku okota mtaroni mda sio mrefuMim sasahv maisha ndo yananipiga hpa na hili ndo wazo lakijinga ninalofanya..View attachment 1325906
Sent using Jamii Forums mobile app
Igoma pamoja sana mkuu, anga hizi.Dah! Nilipomaliza A'level, sikuwa na pesa kabisa. Nikapigika kitaa, ila chakula napata home. Nilisota kukosa pesa, maana nilikosa mkopo HELB. Nikakaa kitaa miaka 2. Wakati huo naona Tabora kugumu sana. Nilizoea pocket money za kutosha, sasa niko zero.
Wakati huo,(Tbr) kitaani kwetu nakuona kama vile Jehanamu. Siku moja nikaenda mjini kutafuta hata vibarua nipate kazi ya kuingiza hata 2000/= nikakutana na jamaa tulosoma shule moja. Ila yeye alituacha ndiyo tuko F2(O'level ). Akanielekeza anapopigia kazi. Tukawa tunawasiliana.
Nilikuwa namwita Usalama wa Taifa!
Siku moja akaniunganisha na dada mmoja kutoka France, akadai anatafuta mtu wa kupiga naye kazi, kwakuwa niko vizuri kwa English itapendeza zaidi. Nikaona haya ndiyo maisha. Yule dada tuliishia kuwa wapenzi tu. Kazi haikuwepo. Ikawa ni kutoka out, kula, kunywa na kupigana mashine tu. Ila alinibadilisha kwa kiasi kikubwa na nikawa wa tofauti. Ila pesa sina. Nami kilio changu ilikuwa pesa. Nikawa mpole tu.
Yule dada baadae alikuja kunambia kauli iliyonikosesha amani, tena tulisafiri mbali kidogo ndipo usiku wake akanishauri habari za kujiunga FM(Free Mason)
Akanielezea faida za kuwa kule nyingi sana. Nikamwambia nitampa jibu next weekend.
Tukarudi mjini, siku narudi home tu. Kumbe mama yangu ameshafunuliwa hayo maono, maana mama ni bonge la Mlokole, ni mshika imani ile ngumu kabisa. Yaani alinisimulia yote kama vile tulikuwa pamoja. Nilibaki nimeshangaa tu. Alikuwa amenisubiria kwa hamu sana. Baadae mahusiano yetu na yule dada wa France hayakudumu baada ya kukataa ombi lake ila aliumia sana.
Baadae nilizuiwa kuwa natoka home kiholela. Nikawa mtu wa home.
Nikakumbuka, kuna wakati mjomba alitupa story za kufanya magendo kutoka nchini Burundi. Pia Burundi ni nchi ambayo ni vyepesi sana mtu kwenda nchi za S.A na Ulaya ila tu uwe na taaruma yeyote na nauli. Nikashuka Kigoma ( ujombani)
Nikapata rafiki wa kuvuka naye Burundi, kule yeye alikuwa na baba zake wadogo.
Tukapanga safari tukavuka mpakani, tukaingia Burundi sasa. Upande wa ziwa Tanganyika, kabonga, tukapita Nyanza, hadi Kalonda. Tukalala hapo. Nakumbuka hapo kidogo nipigwe risasi wakinishuku kuwa ni mtusi,dah! Maana wenyeji wetu walikuwa wahutu. Yule rafiki yangu ndiye akawaambia huyu ni Mtanzania kabisa.
Nikaanza harakati za kwenda Bujumbura na kurudi. Chibitoke pia nilikuwa nafika na Makamba. Na kule juu milimani kwa wafugaji. Tulichange pesa pale Nyanza, bahati ikawa upande wangu. Maana jamaa alijikuta ananipa pesa nyingi zaidi za Kirundi naona hakuwa na ufahamu zaidi.
Nilifundishwa kufanya Business kule na mbinu nyingi sana. Ikiwemo ya kutovaa vizuri unapokuwa mfanyabiashara. Hawanunui ukiwa smart.
Sasa, nikiwa Burundi bila vibali ila nikapata shauku ya kuvuka tena niende Rwanda bila kibali chochote! Maisha haya! Umasikini unakufanya kuwa shujaa! Nikavuka ila sikuchelewa huko nikarudi tena kusaka Burundi. Nikapata vijisenti kiasi nikarudi Tz tena.
Nikakaa kidogo, ndipo nikapata zari la sponsorship ya elimu ya juu (full sponsorship). Nikafurahi sana. Maana chuoni sikusumbuka hata kidogo. Walinigharamia kila kitu. Nilijibidisha sana school, maana sikupenda niwaangushe wafadhili wangu.
Baada ya chuo sasa. Nikawa vizuri maana nilikutana tena na zari la mtoto mkali kutoka nje(Ulaya).
Sasa, mawazo yangu nikajisemea sijui naye atakuwa na fikra za kuniingiza FM! Ila hakuwahi hata kunambia hayo mambo kabisa. Alikuwa bado ni mwanafunzi, huku alikuja kufanya field tu.
Ila tuliishi vizuri naye. Ila huyu sasa alitaka hadi kusahau kilichomleta Africa kwa sababu ya mapenzi. Kuna wakati mapenzi yananoga hadi hufikirii kama yatavunjika.
Baadae alikwenda kwao.
(Hii ni story ndefu )
Baadae sasa nikapigika kupata kazi. Acha kabisa aisee! Kilichokuwa kinanisaidia ni muonekano wangu na mavazi tu.
(Hapa nasisitiza, unapopata pesa za kutosha, nunua nguo hata kama hutazivaa sana leo, miaka ijayo zitakusaidia sana. Hasa zile za heshima ). Nilikuwa napendeza mbaaya ila sina hata buku!
Mwaka 2015 nikapata kibarua sehemu moja ivi mkoa X, kwa malipo kidogo sana.
Baadae nikapata kazi 2016 kwenye Kampuni moja. Mungu ni mwema hadi sasa.
Ila nilichojifunza kwenye huu uzi, ni kwamba "unaweza kuona umesota sana, kumbe kuna watu wamesota zaidi yako".
Toka asubuhi nausoma huu uzi comment moja moja.
Dah! Ngoja niagize ugali samaki mkubwa hapa Igoma nijipongeze kidogo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tutapanga siku moja tuonane aisee!Igoma pamoja sana mkuu, anga hizi.
Aisee! Tutapanga siku moja tuonane pia tufahamiane.Mwamba kumbe upo Igoma Hongera sana karibu BUHONGWA
Mbinu mbinu Muhimu Mkuu!
Dah pole sana bwana mze, usiwaze utatoboa tena..Nimesoma uzi huu kwa kweli watu wamepitia msoto Ila maisha safari wengi washatoboa wachache wapo kwenye situation.
Mine is a little different
Mara tu baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo haukupita mwezi nikapata kazi kwene international NGO mshahara ulikua unatosha na safari kibao.
Nilifanya kwa muda wa miaka 9.baada ya hapo kazi ikakata nyumba ipo kwa linta.kiinua mgongo nilichopata Kama milioni 4 kutoka kazini nikaezeka upande.ujenzi ulinila sana hela sikua na ramani yoyote nyumba niliyokua nakaa Kodi imeisha.nikahamia kwangu.
Nilitamani kila kazi kuanzia kuuza nyanya hadi maandazi nilishawahi fanya kazi nalipwa 90 kwa mwezi niliona muujiza
Fikiria kutoka mshahara wa milioni 2.8 mpaka elfu tisini na nikashukuru jinsi msoto ulivonikamata
Japo Bado nasota Ila angalau nilipata kazi za hapa na pale za mwezi mwezi Ila nimejifunza kwamba.
Kujijenga ni muhimu hata kama una ndugu wanakuzunguka
Nikikumbuka kipato changu chote miaka 9 nimeishia kuwasomesha wadogo zangu ambao kwa Sasa wananidharau inanouma
Aiseeeeeee....NB:haka kastory nimehadithia juu juu tuu kwasababu siwezi kuandika sana,
Katika harakati za maisha na ugumu wa maisha tulikutana na mkongomani story za hapa na pale mpaka kuzoeana akasema kama tupo tayari kujilipua kuna sehemu uko congo DRC kuna almasi nje nje ,ni kuingia kwenye maji tuu na kuzitafuta basi tukajipanga ,tukaenda kwa papa mmoja ivi tukamuuliza kama anaweza kununua almasi ya congo ambayo itakuwa imeingia kwa njia za panya akasema anaweza ,sisi hatukuwa vizuri kifedha hivyo tuliona mambo ya kufatilia vibali yatatukatisha tamaa,kuna jamaa akatuchorea ramani ya njia za panya na gharama yake mpaka kufika kasai tshikapa congo,
Tulienda kwa kupitia Rwanda,tukatoka Rwanda kwa njia za Panya tukaingia bukavu ,tulitulia bukavu kwa siku kadhaa,tukaanza safari ya kuitafuta tshikapa ipo mpakani mwa congo na angola,ilituchukua wiki nzima kufika huko kwa sababu ya miundombuni ya barabara na usafiri pia ulikuwa wa shida na enzi hizo kulikuwa hamna boda boda kama sasa,hatimaye tulifika tshikapa ,tulipumzika kwa siku kadhaa na kuzungumza na wenyeji ili kupata abc’s za sehemu ambayo ina migodi ya almasi lakini walitushauri ni hatari sana kwenda huko migodini kwani hakuna usafiri wa uhakika ni bora kama tuna pesa tuishie kijiji cha kamabue na tununue diamond kwa wachimbaji wadogo,sisi hatukuwa na pesa ya kuweza kununua maana mpaka kufika huko tumeunga unga basi tuliambiwa kuna nyoka sana inatupasa tubebe dawa ya sumu ya nyoka,iyo dawa ni unga unga mweusi,
Siku siku tukaanza safari ya kuelekea kijiji cha kamabue ili tuweze kuifikia migodi ilitupasa tusafiri kwenye mto kasai kwa kutumia boat ambayo ilikuwa ni tia maji tia maji,lengo ilikuwa ni kufika sehemu ambayo wanatafuta diamond chini ya maji,nyoka walikuwa ni wengi sana na tulianza kuingiwa na hofu,hatimaye tulifika sehemu tukatia nanga pamoja na mwenyeji wetu,tulivyoshuka tuu hatujakaa sawa mwenzetu akagongwa na nyoka mkonononi sijui alikuwa anafanya nini,yule mwenyewe wetu akatusadia kumpa huduma ya kwanza kwa kutumia ile dawa kienyeji na ikatupasa turudi haraka tshikapa kumpeleka mwenzetu hospitali ilituchukua siku tatu kufika tshikapa kuna vijiji tulikuwa tukifika inabidi tulale,Mwenzetu alipona na hatutaka tena kurudi kule migodini ,tukasema ni bora tukajipange tutafute mtaji wa kwenda kununua kwa wachimbaji wadogo.Asanteni
SK2016
Gallius
dexterous
The 13
WAKU-GOOGLE
[B][SIZE=5]Root[/SIZE][/B] mkorinto
Mkuu kwanini usimtafute Ontario akupe mbili tatu za kutoboa...Basi wakuu,nilipoenda chuo nikaendeleza harakati zangu,nilikua nauza nguo,kofia,sabuni hasa hasa manjano akina dada wanazipenda sana hizi,liwa,n.k. Nikawa dalali wa simu na assets mbalimbali. Yani nilikua bize haswaa muda wote kichwa yangu inawaza pesa tu,japo mkopo sikukosa japo kwa asilimia kadhaa,hapo mixer niliambatanisha vyeti vya vifo vya kutosha,yani full viambata.
First year mapema semester ya pili nikajichanga vijisent vyangu vya mtaa na nyingine nyingine nikachukua boxer mpyaaaa!!! then nikamuachia mwanangu Yuzzo kitaa apigie kazi.
Mikosi ikaanza upyaa...
Third year final semester nikaibiwa hiyo pikipiki,wahuni walikata rock wakatembea nayo,(kilikua ni kitendo cha kuingia ndani na kuchukua koti,kutoka nje wameacha alama tu za matairi chini. Daah niliumia sana but nikapiga moyo konde. Hapo katikati sijasimulia jinsi miradi ya saloon,chips na mitumba ilivyokufa kisa wana,sitaki story iwe ndefu.
Msoto mkali baada ya Chuo.
Basi wakuu,nikamaliza chuo then nikarud kitaa kupambana,hapo sina A wala B,kila kitu kimepukutika,nina akiba tu kiasi. Nikajaribu kucheki upepo street nikaona pagumu, nikapata wazo la kwenda kuuza moja kati kiwanja changu nje kidogo ya mji(hivi nilinunua bei ya mbuzi kipindi cha ufreelancer wangu,sehemu fulani panaitwa Kitasengwa).
Sikua na namna nikauza then nikamchek mwanangu fulan yuko Mbeya tukazama bush kwako kuchek mali nije nayo town (kosa kubwa kutokusoma alama za nyakati) daah mvua ikaharibu kila kituuu!! Tukakwama bush kama week mbili nikajikuta nazidi kuishiwa tu na hakuna tumaini la kuokoa mzigo.
Niko bush nahangaika napata taarifa huku getto wameiba kila kitu!
Daah wakuu! Nilitamani hata nitoweke tu duniani,nikajiona si kitu mbele ya uso wa dunia! Nikawaza mengi sana! Why Mungu ananiacha nitaabike hivi?
Nilidhoofu sanaaa,sikua hata na hamu ya kutafuta pesa tena! Nikajiona ni mtu nisiepiga hatua katika maisha. Yani bush nmekula loss na huku town wameniliza kila kitu daah wakuu!!
Kwa kifupi nilichoka nikachakaa,hali ikazidi kuwa mbaya nikaona bora nirudi kwa jamaa wa TIGO,jamaa wakanipa mashine zile za kusajilia line kwa alama za vidole "FAMOCO" kidume nikaingia kitaa daah!
Nikaona hapa hakuna namna wacha nipige kazi,issue nzuri ni kuwa mtu akiniona alikua anadhani either nimetoka makao makuu au niko kitengo tofauti na kile cha kusajili,hapa nazungumzia usmart,convincing,e.t.c. So nilipiga noti kwa kiasi fulani mpaka December 31 nilikua nishapata kianzio nikaachana na ile kazi, ijapokuwa kwasasa bado sijakaa sawa kabisa ila angalau ninacho kianzio.
Hayo ni baadhi tu ya niliyopitia wakuu,jambo la msingi katika maisha ni kutokukata tamaa,haijalishi ni magumu kiasi gani unapitia. Ukianguka usilale hapo hapo,inuka songa mbele kwa umakini zaidi.
Maisha ni kama mshale,ili uende mbali zaidi ni lazima uvutwe sana nyuma,so GOD PULLS US BACK TO SHOOT US FORWARD.
Sent using Jamii Forums mobile app
Vidmate nipe mchongo huo mkuu.Yule muhuni yule duh!!! Hadi leo nikiongea na bongo katuni hataki hata kumsikia alimponza akamaliza akiba yake yote hahahah
Ngoja Siku mjomba akukatae..Baada ya kumaliza chuo niliyofautiana na mzee. Nikasepa zangu na kuanzisha biashara ya juisi k.koo.
Niliuza juisi kwa mkokoteni. Yani natengeneza kwenye ndoo alafu napaki sehemu nauza. Nilikuwa nanunua bites kwa jamaa mmoja hivyo nauza na juisi. Faida haikuwa kubwa sana lkn changamoto zikawa nyingi sana.
Kuna siku niligonga garibya jamaa mmoja na mkokoteni wangu maglasi yote chini paaaaa. Kama unavyojua wamachinga wa k.koo kila mtu kelele wengine wakishangilia.
Kijana nimejawa hofu na woga, jamaa mwenye gari alinizingua sana ukicheki Gari nimepasua taa ya nyuma na bampa.
Watu waliniombea pale lkn wapi. Akanisachi na kuchukua pesa zote na mkokoteni akabeba.
Mambo ya biashara yakafia pale. Nikarudi zangu gheto na kuwaza nianze fanya nini. Baada ya wiki ya msoto ndipo nikafanya maamuzi ya kwenda kuomba kazi kwa mjomba wangu ambae anamiliki maukumbi makubwa ya harusi.
Sikutegemea kama angenipokea vizuri vile, palepale nikapelekwa kwenye moja ya ukumbi wake na kutangazwa meneja.
Nyota ndio ilianza kung'aa kuanzia hapo. Mambo si mabaya sasa, watu waliokuwa wananijua nauza juisi walikuwa hawajui kama nimesoma. Leo wakinikuta wananiambia nilikuwa USALAMAA wala sio muuza juisi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Watu tumesota sana, ndio maana sipendi kuishi maisha ya kishenzi, kula sana bata.
Maamaaeee!!
Pamoja sana kaka
👊👊👊Baada ya kumaliza chuo niliyofautiana na mzee. Nikasepa zangu na kuanzisha biashara ya juisi k.koo.
Niliuza juisi kwa mkokoteni. Yani natengeneza kwenye ndoo alafu napaki sehemu nauza. Nilikuwa nanunua bites kwa jamaa mmoja hivyo nauza na juisi. Faida haikuwa kubwa sana lkn changamoto zikawa nyingi sana.
Kuna siku niligonga garibya jamaa mmoja na mkokoteni wangu maglasi yote chini paaaaa. Kama unavyojua wamachinga wa k.koo kila mtu kelele wengine wakishangilia.
Kijana nimejawa hofu na woga, jamaa mwenye gari alinizingua sana ukicheki Gari nimepasua taa ya nyuma na bampa.
Watu waliniombea pale lkn wapi. Akanisachi na kuchukua pesa zote na mkokoteni akabeba.
Mambo ya biashara yakafia pale. Nikarudi zangu gheto na kuwaza nianze fanya nini. Baada ya wiki ya msoto ndipo nikafanya maamuzi ya kwenda kuomba kazi kwa mjomba wangu ambae anamiliki maukumbi makubwa ya harusi.
Sikutegemea kama angenipokea vizuri vile, palepale nikapelekwa kwenye moja ya ukumbi wake na kutangazwa meneja.
Nyota ndio ilianza kung'aa kuanzia hapo. Mambo si mabaya sasa, watu waliokuwa wananijua nauza juisi walikuwa hawajui kama nimesoma. Leo wakinikuta wananiambia nilikuwa USALAMAA wala sio muuza juisi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Watu tumesota sana, ndio maana sipendi kuishi maisha ya kishenzi, kula sana bata.
Maamaaeee!!
Sio mchongo jamaa alitupotezea muda na hela zetu akijidai katajirika kupitia drop shipping kumbe wongo