Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Kuna jamaa mmoja mtaani kwetu Buza anaamka saa 9 alfajiri, ikifika saa 5 asubuhi yupo kijiwe cha kahawa wanabishana kuhusu kama Yesu ni Mungu au la. Watu hawajui kazi anayofanya ila kuna siku moja nilibahatika kukutana naye mitaa ya Kigamboni anatembeza mboga nyumba kwa nyumba.

Kumbe huwa anaamka alfajiri kununua mboga sokoni Kariakoo halafu anaenda kutembeza kwenye mitaa ya mbali ili watu wasijue kazi anayofanya. Ama kweli mjini shule! [emoji4][emoji3][emoji16][emoji23][emoji2][emoji52][emoji28][emoji38][emoji56]

Sent using Jamii Forums mobile app
Napenda sana mishe zile alafu ukute mpaka saa 5 una faida km ya 10k na kuendelea km una mpango wa kusoma unaweza rudi shule bila tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naona kma unabana sana matumizi
Matumizi ya mshahara wa 2.8
Kodi ya nyumba 300,000,
Servive ya gari 100,000,
mafuta ya gari 150,000,
mizinga ya wana ukoo 30,000
Matumizi ya jikoni 400,000,
Breakfast na lunch kazini 200,000,
Luku na Maji 80,000,
Ada ya mtoto shule za awali within miaka 9 utakuwa na watoto 3 (300,000)
house girl 50,000,
nguo viatu kiwi,kunyoa ndevu 50,000,
vitu vya kuchezea watoto 20,000
kuwatumia wazazi 100,000,
vocha kila mwezi 20,000,
harambee za kanisani 50,000
Pesa ya wife matumizi yake 200,000
majukumu ya kijamii (harusi) 50,000
matibabu 60,000

ukiwa na kamchepuko kila mwezi ukikagonga mara mbili geti tu uwe na 80,000, hakajala, etc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kumaliza Vida to 4 nilikaa kitaa life la wazazi likaanza kuwa gumu saana, nilikuwa najipitisha supermarket, kila siku, siku Moja nilikutana na mzungu, mmoja wa kike ndio kwanza amedondoka Toka Europe(zali) nikaanza kumdodosa kwa umombo akanikubali, alipoingia supermarket wauzaji walikuwa hawamuelewi saana, wamewazoea wazungu wa kibongo kisw-english, baaasi sina hili wala yule yule demu mdosi akanifuata faster, niende nikawasaidie wale wauzaji(zali) Tulipofika ndani daaah, nilifanikisha kila kitu mzungu alichokitaka, akanichukua kwake, nikawa house boy wake ila kama baba mwenye nyumba maana kila kitu kwangu, bajet Lak 2 kwa siku, breakfast [emoji505], lunch [emoji899], dinner [emoji899] &drinks daah. Kilichoendelea siku zijazo.............
Itaendelea.....................

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahan sana wadau nimechelewa kuchangia huu mjadala heavy asikwambie mtu maisha kuna kipindi yanakaza kiasi mtu unanyongorota kabisa km sio kupinda kuna kkipindi nilipewa tender ya kulinda shule aisee ile kaz km huna chale itakoma yaan kuna kipindi usingiz unakuchukua unasikia km kuna mtu anakutikisa uamke unaamka huonk mtu mara unasikia nje kuna mtu anakuita unachungulia dirishan huoni mtu kuna siku nilizabwa vibao na mtu nisiyemuona toka siku nikaacha
[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha haya!!acha tu,Mungu ndio anajua nlikotoka na anisamehe kwa mambo nloyafanya mpaka kufika hapa.ila Kama ni msoto nshapitia sana tena wa kutisha. Ila amini usiamini hakuna maisha unapata kirahisi rahisi tu lazima upambane sana
 
Hauko peke yako!

Sent using Jamii Forums mobile app
QUOTE="mwita ke mwita, post: 34101193, member: 25257"]
Matumizi ya mshahara wa 2.8
Kodi ya nyumba 300,000,
Servive ya gari 100,000,
mafuta ya gari 150,000,
mizinga ya wana ukoo 30,000
Matumizi ya jikoni 400,000,
Breakfast na lunch kazini 200,000,
Luku na Maji 80,000,
Ada ya mtoto shule za awali within miaka 9 utakuwa na watoto 3 (300,000)
house girl 50,000,
nguo viatu kiwi,kunyoa ndevu 50,000,
vitu vya kuchezea watoto 20,000
kuwatumia wazazi 100,000,
vocha kila mwezi 20,000,
harambee za kanisani 50,000
Pesa ya wife matumizi yake 200,000
majukumu ya kijamii (harusi) 50,000
matibabu 60,000

ukiwa na kamchepuko kila mwezi ukikagonga mara mbili geti tu uwe na 80,000, hakajala, etc
[/QUOTE]
Hayo matumizi makubwa sana kwangu beside I am a woman very low profile.
But ambitions comes with the kind of money you have.
I have 8 siblings they all studied in private schools ada si chini ya 1.5 per year for each.but hayo hayazuii kusave hell so nakubaliana na wadau wanaoshangaa nawaelewa kabisa
Ila msoto wangu siwezi fananisha na watu wengine Bado najifunza kwani Sasa nafanya kazi za muda which are not bad
 
mimi nimekuelewa sana, watu hawawezi kukuelewa, wanachukulia kama hukuwa makini, ila najua ulivyopitia aiseee
 
Nimerudia kusoma ×5

YAANI UMESEMA

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Then umeachishwa kazi huna kitu.

Hivi ni sijaelewa au sijasoma vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
hamna cha ajabu hapo mkuu tatizo hujafikiria kwa upana, inawezekana kabisa kwa mtu kupitia hayo na zaidi
 
Mmenikumbusha maisha ya chuo, nipo zangu chuoni na jamaa wanaotoka familia tajiri sana, wao kila mwezi wanatumiwa sio chini ya $300 kwa ajili ya matumizi ya chakula, mavazi na luxuries zingine. Mimi natoka familia ya kawaida sana, maisha ya kawaida sana, nikajisemea nisipochekecha akili nitakuwa zobaaaa. Hivi huku mbali kweli nisubiri pesa za wazee, hapana!!

Nikatoka zangu, nikaenda supermarket moja ilikuwa inabamba sana mji huo, nikaomba kazi wakasema hatuwezi kukuajiri coz huna vibali vya ajira, dadeq níkaona sasa hapa nafeli, pesa naitaka nijikimu na pia nidundulize ili nikimaliza chuo niwe na pesa za kuanzia life. Nikaacha kujichanganya na wana "weusi" manake niliona nikiwa nao nitapoteza mda wangu, nikaanza kutafuta urafiki na classmates zangu "weupe", nikapata kama jamaa wawili na dada mmoja nae hakutokea mji ule. Yule dada akawa rafiki yangu sana ila sikutaka hata kumfanya "kimasihara" coz nilijua nitaharibu. Nikamuuliza kuhusu kazi baada ya masomo, akasema ataniunganisha na jamaa zake nao wanafanya kazi part time. Kweli nikakutana na jamaa, wakaniambia the best option ni kazi za construction, wages ni kubwa kuliko huko supermarket au kusafisha barabara kutoa mabarafu. Nikasema poa nipelekeni, nikapelekwa kuna bosi wa kike na MD wa kampuni ni kidume, yule MD akasema hatuwezi kufanya kazi na "mtu wa namna hii", nikajua tu ngozi yangu inaninyima kazi, bahati nzuri yule boss wa kike alinihurumia, akabembeleza sana kwa MD mwisho nikakubaliwa.

Nikapeleka ratiba yangu ya masomo, wakanipangia kazi kutokana na ratiba zangu. Dadeq sitasahau, nilikuwa nalala mda mchache sana, nikitoka class hata sirudi maskani, naenda site napiga kazi at -25°C, kuna kipindi baridi ilifika -40°C, nimevaa gloves za baridi lakini vidole vinaungua kama napitisha kwenye moto, navaa soksi nzito na buts zenye sufi ndani, lakini miguu inakakamaa, vidole vinakufa ganzi lakini kazi lazima ifanyike, wenzangu wanachapa Smirnoff, Vodka, wanavuta sigara balaa ili kutoa baridi, dadeq sitasahau, ila nashukuru nilibaki vile, nilijaribu kidogo kuonja Smirnoff [emoji41] . Baadae nilikuja kuzoea na kuona ni kawaida sana, wenzangu waliniona bonge la kidume, working at -20 to 35°C nje kabisa ilikuwa ni changamoto kubwa kuwahi kutokea.

Nilivyokaribia kumaliza chuo nikapata kazi kwenye kiwanda cha samaki, life was I bit easier there. Walinipenda sana the way nilikuwa nafanya kazi kwa kujituma, hadi namaliza pale boss alinifanyia goodbye party, na kupewa zawadi. Hapa ndio nilipata kuzichakata punani bila hiana, nilihakikisha nalitendea kabila langu haki[emoji23][emoji23].
 
Shikamoo mpare
 
@sakayo hawa ndio ulisema unataka eeeh?
 
Dah! Nilipomaliza A'level, sikuwa na pesa kabisa. Nikapigika kitaa, ila chakula napata home. Nilisota kukosa pesa, maana nilikosa mkopo HELB. Nikakaa kitaa miaka 2. Wakati huo naona Tabora kugumu sana. Nilizoea pocket money za kutosha, sasa niko zero.

Wakati huo,(Tbr) kitaani kwetu nakuona kama vile Jehanamu. Siku moja nikaenda mjini kutafuta hata vibarua nipate kazi ya kuingiza hata 2000/= nikakutana na jamaa tulosoma shule moja. Ila yeye alituacha ndiyo tuko F2(O'level ). Akanielekeza anapopigia kazi. Tukawa tunawasiliana.
Nilikuwa namwita Usalama wa Taifa!

Siku moja akaniunganisha na dada mmoja kutoka France, akadai anatafuta mtu wa kupiga naye kazi, kwakuwa niko vizuri kwa English itapendeza zaidi. Nikaona haya ndiyo maisha. Yule dada tuliishia kuwa wapenzi tu. Kazi haikuwepo. Ikawa ni kutoka out, kula, kunywa na kupigana mashine tu. Ila alinibadilisha kwa kiasi kikubwa na nikawa wa tofauti. Ila pesa sina. Nami kilio changu ilikuwa pesa. Nikawa mpole tu.

Yule dada baadae alikuja kunambia kauli iliyonikosesha amani, tena tulisafiri mbali kidogo ndipo usiku wake akanishauri habari za kujiunga FM(Free Mason)
Akanielezea faida za kuwa kule nyingi sana. Nikamwambia nitampa jibu next weekend.

Tukarudi mjini, siku narudi home tu. Kumbe mama yangu ameshafunuliwa hayo maono, maana mama ni bonge la Mlokole, ni mshika imani ile ngumu kabisa. Yaani alinisimulia yote kama vile tulikuwa pamoja. Nilibaki nimeshangaa tu. Alikuwa amenisubiria kwa hamu sana. Baadae mahusiano yetu na yule dada wa France hayakudumu baada ya kukataa ombi lake ila aliumia sana.

Baadae nilizuiwa kuwa natoka home kiholela. Nikawa mtu wa home.

Nikakumbuka, kuna wakati mjomba alitupa story za kufanya magendo kutoka nchini Burundi. Pia Burundi ni nchi ambayo ni vyepesi sana mtu kwenda nchi za S.A na Ulaya ila tu uwe na taaruma yeyote na nauli. Nikashuka Kigoma ( ujombani)
Nikapata rafiki wa kuvuka naye Burundi, kule yeye alikuwa na baba zake wadogo.

Tukapanga safari tukavuka mpakani, tukaingia Burundi sasa. Upande wa ziwa Tanganyika, kabonga, tukapita Nyanza, hadi Kalonda. Tukalala hapo. Nakumbuka hapo kidogo nipigwe risasi wakinishuku kuwa ni mtusi,dah! Maana wenyeji wetu walikuwa wahutu. Yule rafiki yangu ndiye akawaambia huyu ni Mtanzania kabisa.

Nikaanza harakati za kwenda Bujumbura na kurudi. Chibitoke pia nilikuwa nafika na Makamba. Na kule juu milimani kwa wafugaji. Tulichange pesa pale Nyanza, bahati ikawa upande wangu. Maana jamaa alijikuta ananipa pesa nyingi zaidi za Kirundi naona hakuwa na ufahamu zaidi.
Nilifundishwa kufanya Business kule na mbinu nyingi sana. Ikiwemo ya kutovaa vizuri unapokuwa mfanyabiashara. Hawanunui ukiwa smart.

Sasa, nikiwa Burundi bila vibali ila nikapata shauku ya kuvuka tena niende Rwanda bila kibali chochote! Maisha haya! Umasikini unakufanya kuwa shujaa! Nikavuka ila sikuchelewa huko nikarudi tena kusaka Burundi. Nikapata vijisenti kiasi nikarudi Tz tena.

Nikakaa kidogo, ndipo nikapata zari la sponsorship ya elimu ya juu (full sponsorship). Nikafurahi sana. Maana chuoni sikusumbuka hata kidogo. Walinigharamia kila kitu. Nilijibidisha sana school, maana sikupenda niwaangushe wafadhili wangu.

Baada ya chuo sasa. Nikawa vizuri maana nilikutana tena na zari la mtoto mkali kutoka nje(Ulaya).

Sasa, mawazo yangu nikajisemea sijui naye atakuwa na fikra za kuniingiza FM! Ila hakuwahi hata kunambia hayo mambo kabisa. Alikuwa bado ni mwanafunzi, huku alikuja kufanya field tu.
Ila tuliishi vizuri naye. Ila huyu sasa alitaka hadi kusahau kilichomleta Africa kwa sababu ya mapenzi. Kuna wakati mapenzi yananoga hadi hufikirii kama yatavunjika.
Baadae alikwenda kwao.
(Hii ni story ndefu )

Baadae sasa nikapigika kupata kazi. Acha kabisa aisee! Kilichokuwa kinanisaidia ni muonekano wangu na mavazi tu.
(Hapa nasisitiza, unapopata pesa za kutosha, nunua nguo hata kama hutazivaa sana leo, miaka ijayo zitakusaidia sana. Hasa zile za heshima ). Nilikuwa napendeza mbaaya ila sina hata buku!

Mwaka 2015 nikapata kibarua sehemu moja ivi mkoa X, kwa malipo kidogo sana.
Baadae nikapata kazi 2016 kwenye Kampuni moja. Mungu ni mwema hadi sasa.

Ila nilichojifunza kwenye huu uzi, ni kwamba "unaweza kuona umesota sana, kumbe kuna watu wamesota zaidi yako".
Toka asubuhi nausoma huu uzi comment moja moja.

Dah! Ngoja niagize ugali samaki mkubwa hapa Igoma nijipongeze kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmenikumbusha maisha ya chuo, nipo zangu chuoni na jamaa wanaotoka familia tajiri sana, wao kila mwezi wanatumiwa sio chini ya $300 kwa ajili ya matumizi ya chakula, mavazi na luxuries zingine. Mimi natoka familia ya kawaida sana, maisha ya kawaida sana, nikajisemea nisipochekecha akili nitakuwa zobaaaa. Hivi huku mbali kweli nisubiri pesa za wazee, hapana!!

Nikatoka zangu, nikaenda supermarket moja ilikuwa inabamba sana mji huo, nikaomba kazi wakasema hatuwezi kukuajiri coz huna vibali vya ajira, dadeq níkaona sasa hapa nafeli, pesa naitaka nijikimu na pia nidundulize ili nikimaliza chuo niwe na pesa za kuanzia life. Nikaacha kujichanganya na wana "weusi" manake niliona nikiwa nao nitapoteza mda wangu, nikaanza kutafuta urafiki na classmates zangu "weupe", nikapata kama jamaa wawili na dada mmoja nae hakutokea mji ule. Yule dada akawa rafiki yangu sana ila sikutaka hata kumfanya "kimasihara" coz nilijua nitaharibu. Nikamuuliza kuhusu kazi baada ya masomo, akasema ataniunganisha na jamaa zake nao wanafanya kazi part time. Kweli nikakutana na jamaa, wakaniambia the best option ni kazi za construction, wages ni kubwa kuliko huko supermarket au kusafisha barabara kutoa mabarafu. Nikasema poa nipelekeni, nikapelekwa kuna bosi wa kike na MD wa kampuni ni kidume, yule MD akasema hatuwezi kufanya kazi na "mtu wa namna hii", nikajua tu ngozi yangu inaninyima kazi, bahati nzuri yule boss wa kike alinihurumia, akabembeleza sana kwa MD mwisho nikakubaliwa.

Nikapeleka ratiba yangu ya masomo, wakanipangia kazi kutokana na ratiba zangu. Dadeq sitasahau, nilikuwa nalala mda mchache sana, nikitoka class hata sirudi maskani, naenda site napiga kazi at -25°C, kuna kipindi baridi ilifika -40°C, nimevaa gloves za baridi lakini vidole vinaungua kama napitisha kwenye moto, navaa soksi nzito na buts zenye sufi ndani, lakini miguu inakakamaa, vidole vinakufa ganzi lakini kazi lazima ifanyike, wenzangu wanachapa Smirnoff, Vodka, wanavuta sigara balaa ili kutoa baridi, dadeq sitasahau, ila nashukuru nilibaki vile, nilijaribu kidogo kuonja Smirnoff [emoji41] . Baadae nilikuja kuzoea na kuona ni kawaida sana, wenzangu waliniona bonge la kidume, working at -20 to 35°C nje kabisa ilikuwa ni changamoto kubwa kuwahi kutokea.

Nilivyokaribia kumaliza chuo nikapata kazi kwenye kiwanda cha samaki, life was I bit easier there. Walinipenda sana the way nilikuwa nafanya kazi kwa kujituma, hadi namaliza pale boss alinifanyia goodbye party, na kupewa zawadi. Hapa ndio nilipata kuzichakata punani bila hiana, nilihakikisha nalitendea kabila langu haki[emoji23][emoji23].
Ulichakata nini? sijaelewa vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom