Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

2011wakati nimehitimu kidato cha nne nilienda kumtafuta, nilifanikiwa kumpata ila nathubutu kusema in a safari hii iliniongezea maumivu zaidi. Haikuchukua hata two weeks nikaondoka kwake,nikarejea nikipokua.
2016 nikarejea tena kuweka mambo sawa, wakati huu nilikua mtu mzima kiasi so nilifanikiwa kuweka mambo sawia.

NB: "Every Mom Is Nice Except Mine" (EMINEM)

Sent using Jamii Forums mobile app
Okay,sawa mkuu...this time nikupe pole kwa kuwa na mama ambaye ni harshy.
The mum is still worth it whatsoever character she exibits, nadhani wewe umefanya kwa nafasi yako, am praying for your prosperity bro.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAMA UNA MWONGOZO NIPE MKUU,

KUNA MTOTO WA KIKE WA SISTER ANATAKA AJE KUISHI KWANGU,
WAKATI AWALI ALIKAA MIEZI MIWILI TU AKAONA ANAKOSA UHURU,
AKASEPA.

NA MIMI PRINCIPLE YANGU NI KUWA HAKUNA KUJIACHIA KWA BINTI AISHIYE KWANGU-
AKITAKA KUJIACHIA AKAISHI KWAKE.

ND'O NAFIKIRIA NAMNA YA KUMSAIDIA-
NIPE MWONGOZO FASTA!!!

Sent using Jamii Forums mobile app


Hyo principle nenda nayo hvyohvyo mkuu!ana miaka mingap kwani?
 
Nimecheka kama chizi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ilikua 2013 wakati nasubiri matokeo ya kidato cha nne kama sikosei ilikua mwezi january.Kutokana na ukata wa kukaa home mda mrefu huku nikikosa hata pesa za vocha na bi mother akiwa amepigika nikawa nina njaa iliokithiri(sio njaa ya kula njaa ya hela).

Jioni ya siku moja kabala ya tukio mshikaji wangu Dullah akaniambia amepata kazi ya ukarani kwenye ghala la korosho kesho yake anaanza,nikamwambia basi nami anifanyie mpango akasema sawa atajaribu.

Siku ya tukio niko zangu home asubuhi kama saa 7 na dk kadhaa.,Dullah akaja kuniita nikatoka nje nikakutana na huyo mama tukawa watatu mimi,mama na dula,mazungumzo yalikua hivi.
Mama: hujambo?
Mimi: sijambo shikamoo
Mama: dulla ameniambia na wewe unataka kazi ndo nikamtum aje kukuita,kama upo tayari tuongozane.
Mimi : ndio mama nipo tayari na kwakua nimeshanawa ngoja nivae tu simpo twende(mpaka hapa nikajua ukarani)

Njiani yule mama akatuuliza "hivi mmekunywa chai?" Sisi tukamjibu kwa pamoja "bado"...mara akasema "eeee msije mkaniangukia huko,tukifika nitawanunulia chai"..nikauliza "kwani mama ni kazi gani,si kuandika tu"? Sikujibiwa ,mara paap tukawa tumefika kiwanda(ghala) cha korosho pale mbagala kokoto.Kweli akatuagizia chai na chapati mbili mbili,wakati nakunywa chai nilikutana na jamaa mmoja anaitwa robert(nilimzoea kwa jina la jirani) ikabidi aniulize vipi dogo mbona uko hapa ? Nikamjibu "nimekuja kufanya kazi bro humo kiwandani" akasema utaweza ndugu yangu kubeba gunia za korosho ? Nikamjibu mimi sibebi gunia tumeambiwa tutakua makarani.,akasema sawa ila kama ni kubeba gunia ndugu yangu wewe hutaweza humo ndani ni kama jehanam,Dullah akaninong'oneza achana nae mama mwenyewe ni kiongozi na ndo kasema tutakua makarani.

Mara saa 2:30 ikafika tukawa tumeingia tukaambiwa tubadilishe nguo tukavaa za kazi(hapa kichwani niakanza kujawa na masawali) Yule jirani akasema haya dogo karibu jehanam..aisee unabeba gunia(kiroba) la kwanza likaenda la pili likaishia kati wahindi wakaanza kupiga kelele nimemwaga korosho na kuchana kiroba(wakuu gunia kuliweka mgongoni sio kazi kazi ipo kwenye miguu namaanisha balance ndo ishu). Ikabidi nihamishiwe kwenye kupakia korosho maana kubeba siwezi huko nako ilikua balaa gunia zilikua nyingi balaa halafu hakuna vitendea kazi hakuna mask wala gloves mikono ilichubuka ukitaka kupumzika wahindi wanapiga kelele .

Yule Dullah mara akapokea simu(ya uongo) ghafla nikamuona anaanza kulia akaulizwa kulikoni akasema amefiwa na babu yake doh ikabidi aruhusiwe asepe nikawa nimebaki mimi na wengine.Mpaka kufika saa 6 mchana niko hoi mikono vidonda vitupu,nakumbuka nilimwambia Yule Jirani dah hapa si tayari tumeshamaliza akasema hapana dogo bado kabisa nikazidi kuchoka na kujuta nikamuuliza tena inamaana maisha yako jirani ndo yako hapa akasema ndio nina miaka 5 na nilianza kama wewe ila kwa sasa nishazoea na wewe utazoea,akaanza kunitajia wengine huyu ana miaka 3,7 mpaka 9 aisee nikastaajabu sana mara akaja muhindi tukahamishiwa kiwanda kingine kubeba gunia tupu ili ziletwe huku zipakiwe aisee ilikua balaa gunia zina vumbi nikaishiwa nguvu kwa kukisa hewa ikabidi nitolewe nje ya stoo...

Baada ya hapo tukarudishwa kiwanda kile cha mwanzo kwa ajili ya kuendelea kupakia mpaka kufika huo muda nikikohoa natoa kohozi jeusi nikipenga kamasi hivyo hivyo nikasema hapa hapana ngoja nitoroke..walinzi wakaniuliza unaenda wapi nikasema nimeagizwa mmoja akauliza mbona umebeba na nguo zako sikuangalia nyuma nikawa nishafungua mlango nikaondoka.Kufika home kifua na mwili unaniuma nakohoa balaa nikamuona Dullah aliponiona alicheka sana akasema yeye hakufiwa ila aliona kazi imemshinda alitafuta kisingizio(huyo dullah ni mbavu ila alichemka sasa jiulize hiyo kazi ilikua ngumu kiasi gani).

Ilipofika saa 1 usiku akaja yule mama kuniulizia akasema mbona nimeondoka sijaaga na hela sikuchukua,nikamuuliza hiyo hela hapo unayo? Akasema hana kaicha nikaifuate kesho yake nikamjibu hapana nimesamehe...wiki nzima niliumwa kifua na mwili na tangu siku hiyo nikaapa sitakuja kufanya kazi kwa muhindi wale jamaa ni wauwaji kazi kubwa vifaa hakuna au duni.

Ndefu samahani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njoo na damu mbichi lita na robo nikupatie bure.. Ila hutapata zaidi ya mahitaji ya siku

Jr[emoji769]
Kama ni mahitaji ya siku yaliyonona, hiyo 1250ml ya damu mbichi nakuletea hata kesho asubuhi ukitaka mkuu. Naenda pale vingunguti machioni nakinga naipiga Anticoagulant (EDTA au HAPARIN) asubuhi na mapema nakukabidhi kitu kibichi kabisa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Basi wakuu,nilipoenda chuo nikaendeleza harakati zangu,nilikua nauza nguo,kofia,sabuni hasa hasa manjano akina dada wanazipenda sana hizi,liwa,n.k. Nikawa dalali wa simu na assets mbalimbali. Yani nilikua bize haswaa muda wote kichwa yangu inawaza pesa tu,japo mkopo sikukosa japo kwa asilimia kadhaa,hapo mixer niliambatanisha vyeti vya vifo vya kutosha,yani full viambata.
First year mapema semester ya pili nikajichanga vijisent vyangu vya mtaa na nyingine nyingine nikachukua boxer mpyaaaa!!! then nikamuachia mwanangu Yuzzo kitaa apigie kazi.
Mikosi ikaanza upyaa...
Third year final semester nikaibiwa hiyo pikipiki,wahuni walikata rock wakatembea nayo,(kilikua ni kitendo cha kuingia ndani na kuchukua koti,kutoka nje wameacha alama tu za matairi chini. Daah niliumia sana but nikapiga moyo konde. Hapo katikati sijasimulia jinsi miradi ya saloon,chips na mitumba ilivyokufa kisa wana,sitaki story iwe ndefu.

Msoto mkali baada ya Chuo.
Basi wakuu,nikamaliza chuo then nikarud kitaa kupambana,hapo sina A wala B,kila kitu kimepukutika,nina akiba tu kiasi. Nikajaribu kucheki upepo street nikaona pagumu, nikapata wazo la kwenda kuuza moja kati kiwanja changu nje kidogo ya mji(hivi nilinunua bei ya mbuzi kipindi cha ufreelancer wangu,sehemu fulani panaitwa Kitasengwa).
Sikua na namna nikauza then nikamchek mwanangu fulan yuko Mbeya tukazama bush kwako kuchek mali nije nayo town (kosa kubwa kutokusoma alama za nyakati) daah mvua ikaharibu kila kituuu!! Tukakwama bush kama week mbili nikajikuta nazidi kuishiwa tu na hakuna tumaini la kuokoa mzigo.
Niko bush nahangaika napata taarifa huku getto wameiba kila kitu!
Daah wakuu! Nilitamani hata nitoweke tu duniani,nikajiona si kitu mbele ya uso wa dunia! Nikawaza mengi sana! Why Mungu ananiacha nitaabike hivi?
Nilidhoofu sanaaa,sikua hata na hamu ya kutafuta pesa tena! Nikajiona ni mtu nisiepiga hatua katika maisha. Yani bush nmekula loss na huku town wameniliza kila kitu daah wakuu!!

Kwa kifupi nilichoka nikachakaa,hali ikazidi kuwa mbaya nikaona bora nirudi kwa jamaa wa TIGO,jamaa wakanipa mashine zile za kusajilia line kwa alama za vidole "FAMOCO" kidume nikaingia kitaa daah!
Nikaona hapa hakuna namna wacha nipige kazi,issue nzuri ni kuwa mtu akiniona alikua anadhani either nimetoka makao makuu au niko kitengo tofauti na kile cha kusajili,hapa nazungumzia usmart,convincing,e.t.c. So nilipiga noti kwa kiasi fulani mpaka December 31 nilikua nishapata kianzio nikaachana na ile kazi, ijapokuwa kwasasa bado sijakaa sawa kabisa ila angalau ninacho kianzio.

Hayo ni baadhi tu ya niliyopitia wakuu,jambo la msingi katika maisha ni kutokukata tamaa,haijalishi ni magumu kiasi gani unapitia. Ukianguka usilale hapo hapo,inuka songa mbele kwa umakini zaidi.
Maisha ni kama mshale,ili uende mbali zaidi ni lazima uvutwe sana nyuma,so GOD PULLS US BACK TO SHOOT US FORWARD.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeandika nikafuta.

Nimekumbuka ni Intl NGO na safari za nje ‘kibao’ kwa miaka 9, mshahara 2.8M ila kiinua mgongo ni 4M tu... maisha yako tofauti sana.

Kisha baadae karudi kugombea kazi ya mshahara 90k na aliishi fresh tu, maisha yana vionjo vingi sana.... yote inawezekana.
HAKUNA UHALISIA HAPO MKUU,
JAMAA KALETA CHAI TU HUMU!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi wakuu,nilipoenda chuo nikaendeleza harakati zangu,nilikua nauza nguo,kofia,sabuni hasa hasa manjano akina dada wanazipenda sana hizi,liwa,n.k. Nikawa dalali wa simu na assets mbalimbali. Yani nilikua bize haswaa muda wote kichwa yangu inawaza pesa tu,japo mkopo sikukosa japo kwa asilimia kadhaa,hapo mixer niliambatanisha vyeti vya vifo vya kutosha,yani full viambata.
First year mapema semester ya pili nikajichanga vijisent vyangu vya mtaa na nyingine nyingine nikachukua boxer mpyaaaa!!! then nikamuachia mwanangu Yuzzo kitaa apigie kazi.
Mikosi ikaanza upyaa...
Third year final semester nikaibiwa hiyo pikipiki,wahuni walikata rock wakatembea nayo,(kilikua ni kitendo cha kuingia ndani na kuchukua koti,kutoka nje wameacha alama tu za matairi chini. Daah niliumia sana but nikapiga moyo konde. Hapo katikati sijasimulia jinsi miradi ya saloon,chips na mitumba ilivyokufa kisa wana,sitaki story iwe ndefu.

Msoto mkali baada ya Chuo.
Basi wakuu,nikamaliza chuo then nikarud kitaa kupambana,hapo sina A wala B,kila kitu kimepukutika,nina akiba tu kiasi. Nikajaribu kucheki upepo street nikaona pagumu, nikapata wazo la kwenda kuuza moja kati kiwanja changu nje kidogo ya mji(hivi nilinunua bei ya mbuzi kipindi cha ufreelancer wangu,sehemu fulani panaitwa Kitasengwa).
Sikua na namna nikauza then nikamchek mwanangu fulan yuko Mbeya tukazama bush kwako kuchek mali nije nayo town (kosa kubwa kutokusoma alama za nyakati) daah mvua ikaharibu kila kituuu!! Tukakwama bush kama week mbili nikajikuta nazidi kuishiwa tu na hakuna tumaini la kuokoa mzigo.
Niko bush nahangaika napata taarifa huku getto wameiba kila kitu!
Daah wakuu! Nilitamani hata nitoweke tu duniani,nikajiona si kitu mbele ya uso wa dunia! Nikawaza mengi sana! Why Mungu ananiacha nitaabike hivi?
Nilidhoofu sanaaa,sikua hata na hamu ya kutafuta pesa tena! Nikajiona ni mtu nisiepiga hatua katika maisha. Yani bush nmekula loss na huku town wameniliza kila kitu daah wakuu!!

Kwa kifupi nilichoka nikachakaa,hali ikazidi kuwa mbaya nikaona bora nirudi kwa jamaa wa TIGO,jamaa wakanipa mashine zile za kusajilia line kwa alama za vidole "FAMOCO" kidume nikaingia kitaa daah!
Nikaona hapa hakuna namna wacha nipige kazi,issue nzuri ni kuwa mtu akiniona alikua anadhani either nimetoka makao makuu au niko kitengo tofauti na kile cha kusajili,hapa nazungumzia usmart,convincing,e.t.c. So nilipiga noti kwa kiasi fulani mpaka December 31 nilikua nishapata kianzio nikaachana na ile kazi, ijapokuwa kwasasa bado sijakaa sawa kabisa ila angalau ninacho kianzio.

Hayo ni baadhi tu ya niliyopitia wakuu,jambo la msingi katika maisha ni kutokukata tamaa,haijalishi ni magumu kiasi gani unapitia. Ukianguka usilale hapo hapo,inuka songa mbele kwa umakini zaidi.
Maisha ni kama mshale,ili uende mbali zaidi ni lazima uvutwe sana nyuma,so GOD PULLS US BACK TO SHOOT US FORWARD.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole Sana..... Nimeishi Sana zizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom