Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Baada ya muda mrefu kutaabika nkajikuta Sina kila kitu!yaani from hero to zero!!kitu pekee nlikua nimebaki nacho ni nyumba ila Sasa utakula nyumba?lazima maisha yaendelee! Nkauza nyumba nipate msingi Cha ajabu mtu aliyenipa wazo la biashara mpya ndie alinunua nyumba tena kwa kuilipia nusu nusu nkajikuta pesa imeisha na Niko ndani ya hiyo hiyo nyumba!!nkageuka kuwa mpangaji akaanza kuniomba Kodi ya nyumba

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha! Imebid nicheke maisha haya
 
Nilinunua chupi za kike na sandals nikaenda zangu sokoni tengeru mimi na wifi yangu. tukakodisha meza sh 3000 tukamwaga machupi na maviatu.
Wafanyabiashara wengine wakawa wanatushangaa maana tumepiga pamba jeans zimetukaa vzr na masmartphone makubwaa hlf tumekuja na gari tumepark hapo. Tuliambulia kuuza pair moja ya kiatu sh 4000 tukatoa hela ya meza tukabaki na buku.
Hatukurudi tena.
home[emoji16][emoji16]

[emoji23][emoji23][emoji23]pole sana muhenga!!
 
Sio kuuza tuu, nilienda kuzifuata msituni ndo nakuja kuuza!!

Kabla ya hapo nilikuwa nahubiri sokoni, kwenye vituo vya mabasi sadaka ikawa hainitoshi nikaamua kwenda msituni kukata kuni na kuuza!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mdogo wangu nimecheka sana. Ulihubiri kabisa?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mdogo wangu nimecheka sana. Ulihubiri kabisa?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Umewezaje kunicheka jamani!! Nilihubiri mnoo, huo ndo ulikuwa mtaji wangu sikuwa na mtaji wa kuanzia kabisaa! Wazo likaja naweza kuhubiri injili nipate sadaka!
 
Hahaha, kweli sakayo? Safi sana, maisha haya lazima kujiongeza.
 
NB:haka kastory nimehadithia juu juu tuu kwasababu siwezi kuandika sana,

Katika harakati za maisha na ugumu wa maisha tulikutana na mkongomani story za hapa na pale mpaka kuzoeana akasema kama tupo tayari kujilipua kuna sehemu uko congo DRC kuna almasi nje nje ,ni kuingia kwenye maji tuu na kuzitafuta basi tukajipanga ,tukaenda kwa papa mmoja ivi tukamuuliza kama anaweza kununua almasi ya congo ambayo itakuwa imeingia kwa njia za panya akasema anaweza ,sisi hatukuwa vizuri kifedha hivyo tuliona mambo ya kufatilia vibali yatatukatisha tamaa,kuna jamaa akatuchorea ramani ya njia za panya na gharama yake mpaka kufika kasai tshikapa congo,
Tulienda kwa kupitia Rwanda,tukatoka Rwanda kwa njia za Panya tukaingia bukavu ,tulitulia bukavu kwa siku kadhaa,tukaanza safari ya kuitafuta tshikapa ipo mpakani mwa congo na angola,ilituchukua wiki nzima kufika huko kwa sababu ya miundombuni ya barabara na usafiri pia ulikuwa wa shida na enzi hizo kulikuwa hamna boda boda kama sasa,hatimaye tulifika tshikapa ,tulipumzika kwa siku kadhaa na kuzungumza na wenyeji ili kupata abc’s za sehemu ambayo ina migodi ya almasi lakini walitushauri ni hatari sana kwenda huko migodini kwani hakuna usafiri wa uhakika ni bora kama tuna pesa tuishie kijiji cha kamabue na tununue diamond kwa wachimbaji wadogo,sisi hatukuwa na pesa ya kuweza kununua maana mpaka kufika huko tumeunga unga basi tuliambiwa kuna nyoka sana inatupasa tubebe dawa ya sumu ya nyoka,iyo dawa ni unga unga mweusi,
Siku siku tukaanza safari ya kuelekea kijiji cha kamabue ili tuweze kuifikia migodi ilitupasa tusafiri kwenye mto kasai kwa kutumia boat ambayo ilikuwa ni tia maji tia maji,lengo ilikuwa ni kufika sehemu ambayo wanatafuta diamond chini ya maji,nyoka walikuwa ni wengi sana na tulianza kuingiwa na hofu,hatimaye tulifika sehemu tukatia nanga pamoja na mwenyeji wetu,tulivyoshuka tuu hatujakaa sawa mwenzetu akagongwa na nyoka mkonononi sijui alikuwa anafanya nini,yule mwenyewe wetu akatusadia kumpa huduma ya kwanza kwa kutumia ile dawa kienyeji na ikatupasa turudi haraka tshikapa kumpeleka mwenzetu hospitali ilituchukua siku tatu kufika tshikapa kuna vijiji tulikuwa tukifika inabidi tulale,Mwenzetu alipona na hatutaka tena kurudi kule migodini ,tukasema ni bora tukajipange tutafute mtaji wa kwenda kununua kwa wachimbaji wadogo.Asanteni

SK2016
Gallius
dexterous
The 13
WAKU-GOOGLE

[B][SIZE=5]Root[/SIZE][/B] mkorinto
Pole sana aisee! Ile kauli ya Maisha ni vita, hapo ndipo inapoeleweka.

Vipi sasa mlitokaje huko au bado mko Congo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom