Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Dah! Nilipomaliza A'level, sikuwa na pesa kabisa. Nikapigika kitaa, ila chakula napata home. Nilisota kukosa pesa, maana nilikosa mkopo HELB. Nikakaa kitaa miaka 2. Wakati huo naona Tabora kugumu sana. Nilizoea pocket money za kutosha, sasa niko zero.

Wakati huo,(Tbr) kitaani kwetu nakuona kama vile Jehanamu. Siku moja nikaenda mjini kutafuta hata vibarua nipate kazi ya kuingiza hata 2000/= nikakutana na jamaa tulosoma shule moja. Ila yeye alituacha ndiyo tuko F2(O'level ). Akanielekeza anapopigia kazi. Tukawa tunawasiliana.
Nilikuwa namwita Usalama wa Taifa!

Siku moja akaniunganisha na dada mmoja kutoka France, akadai anatafuta mtu wa kupiga naye kazi, kwakuwa niko vizuri kwa English itapendeza zaidi. Nikaona haya ndiyo maisha. Yule dada tuliishia kuwa wapenzi tu. Kazi haikuwepo. Ikawa ni kutoka out, kula, kunywa na kupigana mashine tu. Ila alinibadilisha kwa kiasi kikubwa na nikawa wa tofauti. Ila pesa sina. Nami kilio changu ilikuwa pesa. Nikawa mpole tu.

Yule dada baadae alikuja kunambia kauli iliyonikosesha amani, tena tulisafiri mbali kidogo ndipo usiku wake akanishauri habari za kujiunga FM(Free Mason)
Akanielezea faida za kuwa kule nyingi sana. Nikamwambia nitampa jibu next weekend.

Tukarudi mjini, siku narudi home tu. Kumbe mama yangu ameshafunuliwa hayo maono, maana mama ni bonge la Mlokole, ni mshika imani ile ngumu kabisa. Yaani alinisimulia yote kama vile tulikuwa pamoja. Nilibaki nimeshangaa tu. Alikuwa amenisubiria kwa hamu sana. Baadae mahusiano yetu na yule dada wa France hayakudumu baada ya kukataa ombi lake ila aliumia sana.

Baadae nilizuiwa kuwa natoka home kiholela. Nikawa mtu wa home.

Nikakumbuka, kuna wakati mjomba alitupa story za kufanya magendo kutoka nchini Burundi. Pia Burundi ni nchi ambayo ni vyepesi sana mtu kwenda nchi za S.A na Ulaya ila tu uwe na taaruma yeyote na nauli. Nikashuka Kigoma ( ujombani)
Nikapata rafiki wa kuvuka naye Burundi, kule yeye alikuwa na baba zake wadogo.

Tukapanga safari tukavuka mpakani, tukaingia Burundi sasa. Upande wa ziwa Tanganyika, kabonga, tukapita Nyanza, hadi Kalonda. Tukalala hapo. Nakumbuka hapo kidogo nipigwe risasi wakinishuku kuwa ni mtusi,dah! Maana wenyeji wetu walikuwa wahutu. Yule rafiki yangu ndiye akawaambia huyu ni Mtanzania kabisa.

Nikaanza harakati za kwenda Bujumbura na kurudi. Chibitoke pia nilikuwa nafika na Makamba. Na kule juu milimani kwa wafugaji. Tulichange pesa pale Nyanza, bahati ikawa upande wangu. Maana jamaa alijikuta ananipa pesa nyingi zaidi za Kirundi naona hakuwa na ufahamu zaidi.
Nilifundishwa kufanya Business kule na mbinu nyingi sana. Ikiwemo ya kutovaa vizuri unapokuwa mfanyabiashara. Hawanunui ukiwa smart.

Sasa, nikiwa Burundi bila vibali ila nikapata shauku ya kuvuka tena niende Rwanda bila kibali chochote! Maisha haya! Umasikini unakufanya kuwa shujaa! Nikavuka ila sikuchelewa huko nikarudi tena kusaka Burundi. Nikapata vijisenti kiasi nikarudi Tz tena.

Nikakaa kidogo, ndipo nikapata zari la sponsorship ya elimu ya juu (full sponsorship). Nikafurahi sana. Maana chuoni sikusumbuka hata kidogo. Walinigharamia kila kitu. Nilijibidisha sana school, maana sikupenda niwaangushe wafadhili wangu.

Baada ya chuo sasa. Nikawa vizuri maana nilikutana tena na zari la mtoto mkali kutoka nje(Ulaya).

Sasa, mawazo yangu nikajisemea sijui naye atakuwa na fikra za kuniingiza FM! Ila hakuwahi hata kunambia hayo mambo kabisa. Alikuwa bado ni mwanafunzi, huku alikuja kufanya field tu.
Ila tuliishi vizuri naye. Ila huyu sasa alitaka hadi kusahau kilichomleta Africa kwa sababu ya mapenzi. Kuna wakati mapenzi yananoga hadi hufikirii kama yatavunjika.
Baadae alikwenda kwao.
(Hii ni story ndefu )

Baadae sasa nikapigika kupata kazi. Acha kabisa aisee! Kilichokuwa kinanisaidia ni muonekano wangu na mavazi tu.
(Hapa nasisitiza, unapopata pesa za kutosha, nunua nguo hata kama hutazivaa sana leo, miaka ijayo zitakusaidia sana. Hasa zile za heshima ). Nilikuwa napendeza mbaaya ila sina hata buku!

Mwaka 2015 nikapata kibarua sehemu moja ivi mkoa X, kwa malipo kidogo sana.
Baadae nikapata kazi 2016 kwenye Kampuni moja. Mungu ni mwema hadi sasa.

Ila nilichojifunza kwenye huu uzi, ni kwamba "unaweza kuona umesota sana, kumbe kuna watu wamesota zaidi yako".
Toka asubuhi nausoma huu uzi comment moja moja.

Dah! Ngoja niagize ugali samaki mkubwa hapa Igoma nijipongeze kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwamba kumbe upo Igoma Hongera sana karibu BUHONGWA
 
Mimi sio kuwaza tu bali nlipigika tena nikiwa mdogo..

Ipo iv baada ya kumaliza la saba nlikataa kuendelea na shule nikazamia mjini nkapata kazi mshahara kwa mwezi 15k nkapiga kama mwaka nikawa na 180kb nkaona hyo kazi inanipotezea mda nkachukua hyo 180kb nkaenda lipia driving school nikiwa na miaka16 tu

Nkasoma kwa miezi kadhaa nkachukua cheti ila leseni nkaambiwa umri na kimo vinapishana na sheria za nchi,hapo iliniuma maana lengo langu lilikua nipate leseni nikatafute kazi ya kuendesha tax.

Nikarudi mtaan nmekaa kama siku mbili wazo likanijia niende garage nkajifunze kutengeneza magari huko ndio nlikutana na binadamu wasiokua na huruma ata chembe kwanza kumbuka hapa kabla ya kuruhusiwa kujifunza kuna form anatakiwa kujaza mzazi wako ili ata jek likifyatuka huko ukafa wao hawatahusika kwa chochote..

Nakumbuka nlipigika unaingia garage saa12 asubuhi ukiwahi sana kutoka ni saa5usiku na hulipwi ata mia ya pipi..

Gari lumekata spring ikichomelewa unatakiwa kuibeba mda huo huo haijalishi imepoa au haijapoa kuna siku sijui ni lichuma gani lizito lilikuja chomelewa af mm nlikua nmetoka ile narud tu nambiwa sogeza ilo chuma huku,kuja kushika nliungua mpaka ngozi za viganja zikabaki kwenye chuma..wala jamaa ni washenzi sana!

Kesho yake sikwenda garage nlibaki nyumban naugulia maumivu mda wote npo na ndoo ya maji barid nmeloweka huko mikono maana ilikua inawaka moto mbaya..

Baada ya siku mbili nkarudi kwa mwajiri wangu Wa 15k kwa mwezi mikono nyuma kama mateka akanihurumia nkaingia kazini japo sikuipenda ila sikua na chaguo tena..

Now wale walionitesa garage mm ndio mteja wao ata kama ni kopo la castle..

Sent using Jamii Forums mobile app
So sorry brother
 
Hapo wala kukuiba.Na Mungu ndio alimwongoza she he akupatie bahasha Ili upate rizki .That is the way it is.
Nilipokuwa chuo mwaka wa pili, bum limekata home siwezi kuomba kwani nilikuwa najisomesha mwenyewe . Nikafikiria nikaona nikipata bum nikanunue jezi niwe nauza, biashara ikakubali ikawa inanilipa, ghafla mtaji ukakakata nyumbani kulikuwa na mamatatizo ikanilazimu kusolve. Nakumbuka siku hiyo ilikuwa alhamis nili lala njaa. Ijumaa naamka njaa yaniuma vibaya Sana utumbo unawasha halafu Sina ramani ya kupata pesa.siku hiyo nikamkumbuka mungu niaksema wacha niende masjid na Leo ijumaa. Nikaenda msikiti mmoja uko town msikiti wa waarabu. Sasa bhana Yule sheikh wa pale msikitini akajichanganya akaniona mstaarabu sijui kwa kuwa navaa miwani ya macho. Akanipa bahasha ya kaki akaniomba nisimame mlangoni Ili waumini wakiingia kusali waweke sadaka kwenye Ile bahasha ya kaki. Nikasimama waumini wakioita wanaupia sadaka mpaka muda wa khotuba ulipofuka nikaenda kukaa nisikize khotuba. Happy njaa inauma utumbo na akili havikuwana ushirikiano. Utumbo unawasha, kichwani naona Kama wadudu wanatembea. Nikaenda chooni haja ndogo, nilipomaliza nikaitoa Ile bahasha kuifungua nakuta noti za 10000 za kutosha. Akili ikanambia to " Mungu ana samehe Saba mara sabini, utakufaa njaa kizembe " Sikuhesabu nikapita na misimbazi 3( 30000) nikarudi ndani msikitini .Tulipomaliza kusali fasta nikamfuata Yule sheikh nikamkabidhi bahasha yake nikamwambia nawahi chuo. Akapokea, nikatembea sikugeuka nyuma.

Mungu atusamehe kwa kweli, kupigika kubaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio Kweli.Mungu Ndo alimpa iyo 30, kwa njia hiyo.Sasa aanguke Kwa njaa afe? Pia Mara nyingi sadaka Ni kwa jili ya mahitaji kama huyo.Mungu Ndo alimpa iyo 30,
Mungu aliamua kukupima imani yako,matekeo ya mtihani ukaangukia pua,kama uliomba toba mungu atakusamehe.....unatakiwa uwe muumini Wa kweli sasa Wa kuswali sana na kufuga uchebe!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeuza ubuyu chuo. Wateja dharau mingi sana. Wanakopa kulipa deni mpaka ugomvi.

Nachukua ubuyu kwa babu issa packet moja 1000, naagiza packet 100 hiyo inakua tsh 100,000/=. Plus cost ya kusafirishia 20,000/=. Nikiuza mmoja 2000/= hapo faida napata kama 80,000/= it's alot faida nzuri. Sema nlikua nauza packet moja Hadi 4 kwa siku. Biashara ilikua slow lakini nikawa sikosi pesa ya kula kila siku

Changamoto niliokutana nayo kwenye hiyo biashara kuna mama mmoja nae alikua mwanachuo, mzanzibari yeye akamwambia mume wake amnunulie ubuyu nae awe ana uza. Akaja na mbwembwe eti anauza mmoja 1500/= mimi nikienda na wangu wa 2000/= wateja wanaleta dharau mbona flani anauza bei ya chini. Nikarudi zangu maskani nikakaa kuwaza sasa next step. Pesa naitaka lakini bei sitaki kushusha. Baada ya kuwaza na kuwazua nikaona sio mbaya nikaenda supermarket nikanunua vile vikopo vina mfuniko nikaja kufanya packaging, kwenye ile packet ya 2000/= mimi nikawa natoa vikopo vitatu, kila kopo nauza buku. So nikawa napata 3000/= nikamuacha yule shoct anauza 1500/= [emoji23][emoji23][emoji23]. Biashara ni akili asiee

Nilijaribu hadi kujifunza kupika kashata, nikanunua raw material zote , nikazama utube kucheki jinsi ya kupika kashata. Aisee hii ilinishinda kashata zilikua zinatoka ngumu kama mawe. Nikaachana nazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee we ni mpambanaji haswa,sorry jimbo lipo wazi?...
 
Matumizi ya kizembe na kijinga yaani yaani unaona uko sahihi kabisa kuandika list ya matumizi yasiyo na maana.

2.8 ni pesa nyingi sanaaa kwa scale ya maisha ya Tz na umasikini wa familia zetu unless utokee familia ya MO hata uwe unasomesha na ujue hakuna asiye somesha mimi nishasomesha sana...alichofanya jamaa na wewe ni uharibu wa pesa.

Salary kama hiyo 2.8 mimi sio miaka 9 huko miaka 2 tu na Triple ×3

Una toka kwenye salary hiyo unaachishwa kazi tu unagombania kazi ya 90000/= kwa mwezi kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila mbuzi anakula kwa urefu wake, huu mshahara aliokuwa anapokea mwita ke mwita , kwa mtu aliezoea kupanda basi na kula mihogo anaona ni mkubwa ila akiupata matumizi yanazidi, huu mshahara ni kama wa walimu wengi wa vyuoni, wengi wao wana maisha ya kawaida sana hata hawajajenga na gari wanazotumia zina miaka
 
Maisha Yana Vingi Sana

Mimi Niligonga O Advance Bihawana Hapo Dodoma

Kurudi Kitaa Dah Raia Wote Wanajua Mim Naenda Chuo Muda Ulipofika Nikawa Bado Nipo Nikasingizia Mkopo Kumbe Nilipiga Bashite La PCB Yaan Pure 0 (Gs Na BAM Zote F)

Basi Nikamuomba Bro Mmoja Akawa Ananipa Boda Yake Nakula Vichwa Usiku Huwezi Amini Siku Ya Kwanza Usiku Nikagonga Mtu Nikapelekwa Sero Nikakaa Wiki.

Nipo Ndani Nikawaza Vingi Sana Ndipo Nilipotoka Nikajiunga Na Jf Nikapata Kazi Ya Lodge Humu Humu Mshaara 100k Ipo Huko Airport Lakin Shughul Yake Sio Ya Kitoto, Unafua Shuka Watu Wamelana Ndogo Yaan Mav Kabisa Na Hakuna Gloves Kabisa Yaan Unapitia Tabu Mpaka Unaona Dah Hapa Siwez Ila Ukikumbuka Msoto Wa Home Unafanya Then Unasahau, Nilikaa Pale Miez Mitano Nikamuibia Ibia Nikapata Kama 2M.

Nikarudi Kitaa Nikanunua Boda 1.2M Kwa Bro Kuja Kuchunguzwa Kumbe La Wizi Nikaenda Tena Ndan Mwezi Sema Bi Mkubwa Akaja Kunitoa.

Nikarud Mtaan Tena Nikawa Najichanganya Tu Mpaka Nikpata Nafasi Ya Chuo Diploma CO.

Kufika Chuo Ndio Nikaanza Kujifanya Fund Simu Na Laptop, Mtu Akileta Simu Naenda Choon Na Google Jins Ya Kuifungua Na Tatizo Lake, Nikawa Nafanya Hivyo Na Zinapona Na Nyingine Zinazima Kabisa But Nashukuru Mungu Hii Mishe Iliniingizia Pesa Sana Na Ndio Naifanya Mpaka Now Japo Ka Diploma Ninako Ila Sikatumii.

#Wilmer


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipomaliza cha nne,nkapata kazi ya kumenya viazi vya chips maeneo ya magomeni aiseee nlikuwa nameny viazi zaidi ya debe 6-8 per day home mambo yalikuwa magumu sana mother alisha dead tangu nkiwa form 2 so life home lilikuwa ngumu askuambie mtu mshua tungi tu daily
Nkawa naenda asubhi saa 12 nafanya usafi na kufungua goli nakoleza moto napika chai nakunywa then naanza kumenya viazi vyangu hiyo ngoma mpaka saa4 ucku salary 1500 per day

Sasa nkawa na demu wangu anasoma pale babtist sec,anaitwa mary mtot wa wa ushuani upanga magorofa ya BOT,na pale nnapofanya kazi ndio kituo chao cha kuja kula kiepe na mazaga zaga mengine nkaona ooooh isiwe kesi akifungua shule hapa akanikuta mm ndio namenya viazi ntazid kuongeza matatizo na papa ntaishia kuliskia kwenye bomba mkasepaa

Nkapata kazi ya kuuza glosary oale maeneo ya shecklango sinza ndani pale wanapochinja kuku kaglosary kenyew ukiuza sana unapata buk 3-5 na mm mshahara wangu ni chakula tu,so nkawa nakagua bia,soda,wine zilizo expare nazigida tu so full day nimelewa zangu sina habar naiba na krate naenda kuuza ela natombea stakagi shida mim....



Form six,nlipomaliza nkaenda kuwa saidia fundi aisee maeneo ya tegeta madale nilivuta bangi hasa nilichangantikiwa kabisa nkapewa jina nlikuwa naitwa "mother fucker" per day nlikuwa nakula 10000 so nkaona sio case nkawa namuhonga tu dem wangu mary huku najipakulia mtot taratibu

Nlipomaliza chuo nkatafuta kazi weee holla,nkarudi zangu saidia fundi kama kawaida kula 10 per day nkaona maisha ndio haya vuta mabangi sana nlikuwa na laptop nkauza nguo nzur nzur za kutoa mtu ukifika bei nauza staku shida za kingese mm .....
Nlipiga ile kazi nkaja nkapata kazi ya kuuza magodoro pale nyamala natuta mawili hapo ndio nkasettle nkawa napiga pesa nkanza na kuchepuka mary na yy anaona nazingua akapata bwana abafanya kazi airport akailewa ckuwah kushika 4ml za kwangu mm mwenywe ila kipindi hiyo nilizishika

Nkaja kuajiruwa na serekal na ndio umaskini ukaanzia hapo mpaka leo napata ela ya kula tu na watoto wanaenda shuke ila bado natembea na miguu sana and I am not happy at all

Mungu sio wa wote kila mtu apambane anavyojua ili mradi utoboe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Asee we jamaa barikiwa kwa kunichekesha hivi!

Sijawahi kuangua kicheko kama hiki[emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeuza ubuyu chuo. Wateja dharau mingi sana. Wanakopa kulipa deni mpaka ugomvi.

Nachukua ubuyu kwa babu issa packet moja 1000, naagiza packet 100 hiyo inakua tsh 100,000/=. Plus cost ya kusafirishia 20,000/=. Nikiuza mmoja 2000/= hapo faida napata kama 80,000/= it's alot faida nzuri. Sema nlikua nauza packet moja Hadi 4 kwa siku. Biashara ilikua slow lakini nikawa sikosi pesa ya kula kila siku

Changamoto niliokutana nayo kwenye hiyo biashara kuna mama mmoja nae alikua mwanachuo, mzanzibari yeye akamwambia mume wake amnunulie ubuyu nae awe ana uza. Akaja na mbwembwe eti anauza mmoja 1500/= mimi nikienda na wangu wa 2000/= wateja wanaleta dharau mbona flani anauza bei ya chini. Nikarudi zangu maskani nikakaa kuwaza sasa next step. Pesa naitaka lakini bei sitaki kushusha. Baada ya kuwaza na kuwazua nikaona sio mbaya nikaenda supermarket nikanunua vile vikopo vina mfuniko nikaja kufanya packaging, kwenye ile packet ya 2000/= mimi nikawa natoa vikopo vitatu, kila kopo nauza buku. So nikawa napata 3000/= nikamuacha yule shoct anauza 1500/= [emoji23][emoji23][emoji23]. Biashara ni akili asiee

Nilijaribu hadi kujifunza kupika kashata, nikanunua raw material zote , nikazama utube kucheki jinsi ya kupika kashata. Aisee hii ilinishinda kashata zilikua zinatoka ngumu kama mawe. Nikaachana nazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama mawe [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kama nakuona ulivyokuwa ukikasirika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Al manusura niende zangu Lebanon huko nikajichanganye na wazee wa kujilipua.
Nilikua nishapewa Abc zoote. Yaani ile nasema haya njooni mnichukue wangefika hadi kitaani kwetu.. Saa hizi ningekua nimeshikilia Ak47 na nusu kanzu yangu.
Be careful na watu mnaowasiliana nao.
Safari ilikua ya Zenji,Sanaa..then Lebanon. Kisha unapelekwa kukinukisha Israel huko
Waliniahidi dola kibao tu.. kilichoniponza ni vile kupenda kujua vitu na lugha za watu maana jamaa alinivutia jinsi anavyokichapa kiebrania..kiarabu..kizungu na kirusi.
Zenji ningeenda kukutana na wenzangu huko then tupigwe training ya kubrain wash huku familia imeachiwa madorari
Chai ya rangi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakyanani misha haya!!!acha tu.Kuna siku mwaka flan nilishawah kutaman kuwa omba omba wale viwete wanaokaa njian.

Ilikua kama mwez mzima hiv nimekula msoto wa kiwango cha SGR.nikiwa kwenye mishe zangu maeneo ya posta, sina 100 mbovu mfukoni njaa inauma kishenzi jua kali na kiu ya maji imekaba ila hata kandoro siwez mudu kununua nijipooze, hatari na simu hata 0 ya kubip haina salio.

Nakatiza mitaa ya posta pale ilipo postal bank , kuna kiwete anaomba omba ila nadhan alikua break time muda ya saa 7 mchana ametulia, pembeni naliona kwenye mkoba lundo la coins zake, halaf kaletewa pilau nyama na kachumbali kwa juu.Pemben ana maji yake ya uhai ya baridiii halaf mkonon kashika vocha anakwangua ili ajaze salio.

Aliponiona akaanza kuniomba tena na mm hela, Dah, nikapata hasira ilochanganyika na huruma halaf nikajionaje sijui.Kimoyo moyo nikasema ww mjinga ungejua navyokutaman niwe kama ww hapo dakika hii!!!

Nikapita kimya kimya.Nilikua na mshkaji wangu anaitwa Bony basi tulipofika mbela tukacheka sanaaa na kujionea huruma maana na yy alii notice hiyo hali halaf wote tulikua juubya vyuma balaa.
Kweli maisha safari,naimani sahv mambo safi mkuu.
 
Nimesoma uzi huu kwa kweli watu wamepitia msoto Ila maisha safari wengi washatoboa wachache wapo kwenye situation.
Mine is a little different
Mara tu baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo haukupita mwezi nikapata kazi kwene international NGO mshahara ulikua unatosha na safari kibao.
Nilifanya kwa muda wa miaka 9.baada ya hapo kazi ikakata nyumba ipo kwa linta.kiinua mgongo nilichopata Kama milioni 4 kutoka kazini nikaezeka upande.ujenzi ulinila sana hela sikua na ramani yoyote nyumba niliyokua nakaa Kodi imeisha.nikahamia kwangu.
Nilitamani kila kazi kuanzia kuuza nyanya hadi maandazi nilishawahi fanya kazi nalipwa 90 kwa mwezi niliona muujiza
Fikiria kutoka mshahara wa milioni 2.8 mpaka elfu tisini na nikashukuru jinsi msoto ulivonikamata
Japo Bado nasota Ila angalau nilipata kazi za hapa na pale za mwezi mwezi Ila nimejifunza kwamba.
Kujijenga ni muhimu hata kama una ndugu wanakuzunguka

Nikikumbuka kipato changu chote miaka 9 nimeishia kuwasomesha wadogo zangu ambao kwa Sasa wananidharau inanouma
Duh nimeelewa sana point yako ya kujijenga ni muhimu hata kama unasaidia watu,mana binadamu hawana jema na hubadilika.
 
Nimerudia kusoma ×5

YAANI UMESEMA

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Then umeachishwa kazi huna kitu.

Hivi ni sijaelewa au sijasoma vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha unaona kama anakutania au unahisi hujasoma vizuri hahah
 
Back
Top Bottom