Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Samahan sana wadau nimechelewa kuchangia huu mjadala heavy asikwambie mtu maisha kuna kipindi yanakaza kiasi mtu unanyongorota kabisa km sio kupinda kuna kkipindi nilipewa tender ya kulinda shule aisee ile kaz km huna chale itakoma yaan kuna kipindi usingiz unakuchukua unasikia km kuna mtu anakutikisa uamke unaamka huonk mtu mara unasikia nje kuna mtu anakuita unachungulia dirishan huoni mtu kuna siku nilizabwa vibao na mtu nisiyemuona toka siku nikaacha
Mwamini Mungu akulinde.
 
NB:haka kastory nimehadithia juu juu tuu kwasababu siwezi kuandika sana,

Katika harakati za maisha na ugumu wa maisha tulikutana na mkongomani story za hapa na pale mpaka kuzoeana akasema kama tupo tayari kujilipua kuna sehemu uko congo DRC kuna almasi nje nje ,ni kuingia kwenye maji tuu na kuzitafuta basi tukajipanga ,tukaenda kwa papa mmoja ivi tukamuuliza kama anaweza kununua almasi ya congo ambayo itakuwa imeingia kwa njia za panya akasema anaweza ,sisi hatukuwa vizuri kifedha hivyo tuliona mambo ya kufatilia vibali yatatukatisha tamaa,kuna jamaa akatuchorea ramani ya njia za panya na gharama yake mpaka kufika kasai tshikapa congo,
Tulienda kwa kupitia Rwanda,tukatoka Rwanda kwa njia za Panya tukaingia bukavu ,tulitulia bukavu kwa siku kadhaa,tukaanza safari ya kuitafuta tshikapa ipo mpakani mwa congo na angola,ilituchukua wiki nzima kufika huko kwa sababu ya miundombuni ya barabara na usafiri pia ulikuwa wa shida na enzi hizo kulikuwa hamna boda boda kama sasa,hatimaye tulifika tshikapa ,tulipumzika kwa siku kadhaa na kuzungumza na wenyeji ili kupata abc’s za sehemu ambayo ina migodi ya almasi lakini walitushauri ni hatari sana kwenda huko migodini kwani hakuna usafiri wa uhakika ni bora kama tuna pesa tuishie kijiji cha kamabue na tununue diamond kwa wachimbaji wadogo,sisi hatukuwa na pesa ya kuweza kununua maana mpaka kufika huko tumeunga unga basi tuliambiwa kuna nyoka sana inatupasa tubebe dawa ya sumu ya nyoka,iyo dawa ni unga unga mweusi,
Siku siku tukaanza safari ya kuelekea kijiji cha kamabue ili tuweze kuifikia migodi ilitupasa tusafiri kwenye mto kasai kwa kutumia boat ambayo ilikuwa ni tia maji tia maji,lengo ilikuwa ni kufika sehemu ambayo wanatafuta diamond chini ya maji,nyoka walikuwa ni wengi sana na tulianza kuingiwa na hofu,hatimaye tulifika sehemu tukatia nanga pamoja na mwenyeji wetu,tulivyoshuka tuu hatujakaa sawa mwenzetu akagongwa na nyoka mkonononi sijui alikuwa anafanya nini,yule mwenyewe wetu akatusadia kumpa huduma ya kwanza kwa kutumia ile dawa kienyeji na ikatupasa turudi haraka tshikapa kumpeleka mwenzetu hospitali ilituchukua siku tatu kufika tshikapa kuna vijiji tulikuwa tukifika inabidi tulale,Mwenzetu alipona na hatutaka tena kurudi kule migodini ,tukasema ni bora tukajipange tutafute mtaji wa kwenda kununua kwa wachimbaji wadogo.Asanteni




SK2016
Gallius
dexterous
The 13
WAKU-GOOGLE

[B][SIZE=5]Root[/SIZE][/B] mkorinto
mtakahela
 
Sio kuuza tuu, nilienda kuzifuata msituni ndo nakuja kuuza!!

Kabla ya hapo nilikuwa nahubiri sokoni, kwenye vituo vya mabasi sadaka ikawa hainitoshi nikaamua kwenda msituni kukata kuni na kuuza!
@sakayo ww ndio ulikuwa unahubiria kwenye macoaster yanayotoka korogwe kwenda Tanga?,mlikuwa mnapanda kuanzia pale Muheza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tehtehtehteh.... maisha yanamisoto hatari mazee
 
Nimerudia kusoma ×5

YAANI UMESEMA

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Then umeachishwa kazi huna kitu.

Hivi ni sijaelewa au sijasoma vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Ambacho hujaelewa ni nini ? Thamani ya hiyo 90 kwa mwezi alikuja kuiona baada ya kupigika sana na maisha. Kumbuka ajira huwa inakata pasipo kukuandaa. Pia alikuwa kawekeza kwenye nyumba na kusomesha hao ndugu zake.
 
Lazima nibadilike tena zaidi ya yeyote viwanja nitavyokaa mimi sio vya hazi ya chini ILA first nahakikisha iyo 2.8M inakuwa 6M kwa mwezi na nikiachishwa kazi still 3M kwa mwezi inasoma huku nimelalaa.

Mkuu usi kaariri mimi sio mtu wa bata ila nakula bataa purposivelly ndio maana makwambia hiyo pesa nutaitanua kidogo atleast isome 6M mpaka 7M atleast ninaiipenda pesa, napenda life style, expensive shits, facy place ila hivi vyote kuvi afford bila mawazo tanua pesa kwanza, na kwa salary hiyo unahitaji mwaka huu 1 tu kutoka 2.8M kwa mwezi mpaka 6M kwa mwezi miaka yote inayobaki unafunga kiwaanja chochote kile mjini bila stress nitaachishwa kazi.

NB: Point yangu ipo kwenye Balance de between making and spending...make kwanza japo kidogo then spend rest of your life sio una spend totally today kesho lazima ule msoto tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizi plans wengi huwa nazo kipindi huna ila ukishapata ni wachache sana hubaki kwenye mawazo ya mwanzo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipigika ikabidi nikachukue mashati ya buku buku tandale, nikanyosha vizuri nikaenda kuuza kinondoni hadi baharini bila kuuza hata shati moja, wakati huo sina hata mia na njaa inagonga kishenzi.
Mwisho wa siku nikaenda kwenye mti jirani na aghakan nikaanza kupumzika huku napata upepo wa bahari mida kama ya saa tisa alasiri hivi.
Baadae kidogo akaniamsha dada mmoja ana wali ambao umepakiwa kabisa kwenye vile vifungashio, akanambia alikuwa na oda kwa mafundi sasa mmoja hayupo na chakula kishalipiwa, na akasema aliniona toka nikiwa kwa fundi viatu jirani na AZANIA BANK maeneo yale yale ya agakhan.
Nikajisemea moyoni hapa inabidi nisiigize kama desturi ya sisi waafrika, kitu unataka halafu unasema ahsante nimeshiba! Nikamwambia ahsante sana, kweli nilikuwa na njaa.
Niligonga ule wali ndio akili ikakaa sawa (yaani njaa ikizidi hata akili inakuwa na mawenge)
Safari ya kurudi home ikaanza na nikaja kuuza shati moja kwa 2000 pale salander bridge jioni kabisa.
Vp huyo wife material ulimpotezea au ulichukua mzigo?
 
Sometimes mtu unaweza hisi maisha yamekupiga ila ukitoka na kusikiliza wengine unapata kila sababu ya kumshukuru Mungu

Binafsi maisha yalinipiga ila si kwa kukosa vocha ama chakula ama nauli ila ni kwa kile nilichoamini napaswa kufikia ktk maisha bila ya kuajiriwa

Hivyo nilikataa nafasi kadhaa za kuajiriwa hapo naelekea kumaliza chuo July 2018 bro wangu akiwa na cheo kampuni x ya utalii akaniambia kuna nafasi maliza chuo uje upige kazi temporal kama store keeper bila chenga nikamchana sitaki kuajiriwa,,, metoka chuo direct ifakara kulima mpunga huko sikurudisha hata mia katikati hapo nikiusubiria mpunga nikauza sana mayai ya kuchemsha na sambusa... by dec 2018 nikawa na uhakika dili la mpunga lishabuma na mebaki sina hata mia pamoja na wenzangu tukapata idea ya kulima maharage Gairo tukaweka mipango sawa then nikarudi home maza alikuwa mgonjwa sana home pale nikaungaunga mixer kuomba nikapata laki 6 nikatoa washikaji wakakodi mashamba na hiyo hiyo ikatosha hadi kwenye mavuno tulikodi heka 20... Wakati wa mavuno wenzangu wakawa na harakati nyingine za hapa na pale mi ikawa ndio wajibu wangu kwenda kusimamia uvunaji huko huko nikasoma gap la kununua maharage kwa wakulima na kuyapeleka town kuuza mixer nilifanya juu chini yale mashamba ya pamoja nikavuna fasta na kuuza mzigo ile hela nikawa nazungushia kununua na kuuza + 2m niliyoomba home kusema kweli ile biashara haina hasara na hela niliiona kiasi chake kilichonikwamisha niliuugua kama mwezi nipo hoi hivyo nilivyopoona msimu ukawa ndio unaishia na hela ya shamba tukagawana ila nikawa bado na chenchi za kuendelea kununua gunia kadhaa na kupeleka town... By sept 2019 nikapata fursa ya kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara ya nafaka ulioitishwa na waziri wa kilimo hapo niliziona fursa kibao na nikapata motisha wa kurudi shamba kupambana upya... Nilirudi ila msimu ulikuwa umefika mwisho haswaa maharage hamna target ikawa ni kusubiria ya mtukula Uganda nikiwaza kwenda huko na shs 3m zangu naona haitoshi ila nikizungumza na watu wananiambia inatosha sana kibaya hapo ni October na msimu unaanza DEC kuelekea January halo nilipata stress na hofu ya kuitumia pesa kutokana na kukosa mzunguko hadi ikafikia hatua ya kuomba kibarua ili nijipange kwa msimu utakaokuja...

Mungu mkubwa kabla ya kupata hicho kibarua ikatokea mama mmoja aliyekuwa ktk ule mkutano tumefahamiana kwa bahati mbaya tu yaan ilitokea mekosea namba nikimtafuta mtu mwingine aliyehit ktk ule mkutano ambae nae alikuwa akimtafuta pia basi nikampa mawasiliano yake mixer story tukajuana na nikawa nampigia kumuuliza feedback kama amefanikiwa kupata msaada toka kwa yule mtu... Siku ya siku nawaza kurudi home akaniambia nina shida sana ya mahindi fanya kunitafutia yeye anasaga sembe na dona nikaingia machaka kadhaa mwisho nikapata chimbo la mahindi na kuyasafirisha hadi dsm kusema kweli baada ya kuanza hiyo biznez upepo ulichange na stress zikanipungua maana nilifikia hatua ya kufata vyeti chuo ili nikaombe kazi... Huu ni ufupisho wa ufupisho sababu niliyofanya na kuyapanga hapo ktkt ni mengi siwezi andika yote ikiwa ni pamoja na kupoteza hela na muda kwenye drop shipping kupitia darasa lililoanzishwa na bwana frank frain Byera Deo Corleone

Mpaka sasa msimu umeisha ila namshukuru Mungu mepata network kubwa dsm na mtaji umekuwa ghafla toka kusafirisha mahindi tani 5 hadi 11 hapa kuna pesa fulani niliomba nikaongezea kwenye mtaji na kupitia hili zao najiona nikitengeneza pesa ya maana mwaka huu... Mungu tu ajalie na kuepusha balaa yoyote

#2020 twenty twenty, twenty plenty
 
Sometimes mtu unaweza hisi maisha yamekupiga ila ukitoka na kusikiliza wengine unapata kila sababu ya kumshukuru Mungu

Binafsi maisha yalinipiga ila si kwa kukosa vocha ama chakula ama nauli ila ni kwa kile nilichoamini napaswa kufikia ktk maisha bila ya kuajiriwa

Hivyo nilikataa nafasi kadhaa za kuajiriwa hapo naelekea kumaliza chuo July 2018 bro wangu akiwa na cheo kampuni x ya utalii akaniambia kuna nafasi maliza chuo uje upige kazi temporal kama store keeper bila chenga nikamchana sitaki kuajiriwa,,, metoka chuo direct ifakara kulima mpunga huko sikurudisha hata mia katikati hapo nikiusubiria mpunga nikauza sana mayai ya kuchemsha na sambusa... by dec 2018 nikawa na uhakika dili la mpunga lishabuma na mebaki sina hata mia pamoja na wenzangu tukapata idea ya kulima maharage Gairo tukaweka mipango sawa then nikarudi home maza alikuwa mgonjwa sana home pale nikaungaunga mixer kuomba nikapata laki 6 nikatoa washikaji wakakodi mashamba na hiyo hiyo ikatosha hadi kwenye mavuno tulikodi heka 20... Wakati wa mavuno wenzangu wakawa na harakati nyingine za hapa na pale mi ikawa ndio wajibu wangu kwenda kusimamia uvunaji huko huko nikasoma gap la kununua maharage kwa wakulima na kuyapeleka town kuuza mixer nilifanya juu chini yetale mashamba ya pamoja nikavuna fasta na kuuza ile hela nikawa nazungushia kununua na kuuza + 2m niliyoomba home kusema kweli ile biashara haina hasara na hela niliiona kiasi chake kilichonikwamisha niliuugua kama mwezi nipo hoi hivyo nilivyopoona msimu ukawa ndio unaishia na hela ya shamba tukagawana ila nikawa bado na chenchi za kuendelea kununua gunia kadhaa na kupeleka town... By sept 2019 nikapata fursa ya kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara ya nafaka ulioitishwa na waziri wa kilimo hapo niliziona fursa kibao na nikapata motisha wa kurudi shamba kupambana upya... Nilirudi ila msimu ulikuwa umefika mwisho haswaa maharage hamna target ikawa ni kusubiria ya mtukula Uganda nikiwaza kwenda huko na shs 3m zangu naona haitoshi ila nikizungumza na watu wananiambia inatosha sana kibaya hapo ni October na msimu unaanza DEC kuelekea January halo nilipata stress na hofu ya kuitumia pesa kutokana na kukosa mzunguko hadi ikafikia hatua ya kuomba kibarua ili nijipange kwa msimu utakaokuja...

Mungu mkubwa kabla ya kupata hicho kibarua ikatokea mama mmoja aliyekuwa ktk ule mkutano tumefahamiana kwa bahati mbaya tu yaan ilitokea mekosea namba nikimtafuta mtu mwingine aliyehit ktk ule mkutano ambae nae alikuwa akimtafuta pia basi nikampa mawasiliano yake mixer story tukajuana na nikawa nampigia kumuuliza feedback kama amefanikiwa kupata msaada toka kwa yule mtu... Siku ya siku nawaza kurudi home akaniambia nina shida sana ya mahindi fanya kunitafutia yeye anasaga sembe na dona nikaingia machaka kadhaa mwisho nikapata chimbo la mahindi na kuyasafirisha hadi dsm kusema kweli baada ya kuanza hiyo biznez upepo ulichange na stress zikanipungua maana nilifikia hatua ya kufata vyeti chuo ili nikaombe kazi... Huu ni ufupisho wa ufupisho sababu niliyofanya na kuyapanga hapo ktkt ni mengi siwezi andika yote ikiwa ni pamoja na kupoteza hela na muda kwenye drop shipping kupitia darasa lililoanzishwa na bwana frank frain Byera Deo Corleone

Mpaka sasa msimu umeisha ila namshukuru Mungu mepata network kubwa dsm na mtaji umekuwa ghafla toka kusafirisha mahindi tani 5 hadi 11 hapa kuna pesa fulani niliomba nikaongezea kwenye mtaji na kupitia hili zao najiona nikitengeneza pesa ya maana mwaka huu... Mungu tu ajalie na kuepusha balaa yoyote

#2020 twenty twenty, twenty plenty
Nikikumbuka nacheka tu jinsi tulivyokuwa blinded aisee.
Hit PM
 
Back
Top Bottom