vidmate
JF-Expert Member
- May 7, 2018
- 722
- 1,343
Usiache kunitag boss yule mnyambo anawaliza wengi ana id kama 10 hivi
Usiache kunitag boss yule mnyambo anawaliza wengi ana id kama 10 hivi
Hahaha dah hizi online business zinahitaji ujitoe vya kutosha..vip sasa iyo mission ingine mkuuSio mchongo jamaa alitupotezea muda na hela zetu akijidai katajirika kupitia drop shipping kumbe wongo
pole mkuu,NGOJA MIMI NITOE YANGU
Nakumbuka wakt namaliza chuo 2010 nilipigika sana..Nilipitia sana mateso na dharau za kila namna kutoka kwa majirani zangu(esp wazee)
Bahati nzuri nilikuwa na sehemu ya kujihifadh kwa hyo sikuwa na hofu ya kulipa kodi wala nn
Nakumbuka ilibidi nitumie hela niliyobaki nayo(masalio ya boom) kutengeneza mkokoteni wenye uwezo wa kubeba madumu 10
So nikawa nanunua maji dumu sh 100..naenda kuuza maeneo ya mbali na pale nilipo(kama kilomita 8 hv) kwa shilingi 400-500
Hii kazi ilikuwa ngumu sana ila nikawa napata kafaida kazuri tu ka kuweza ku-sustain mahitaji ya hapa na pale
Sasa pata picha hii kazi unaifanyia mtaani kwako na watu wote mtaani wanajua umemaliza chuo alafu unasukuma mkokoteni wa maji...aisee nilipata tabu sana...dharau zilikuwa nyingi sana ila ambayo sintaisahau ni ya demu mmoja kunitolea shombo kali sana baada ya KUMTOKEA..alinipa SHIT ambazo zilinifanya NIUMIE sana
Nashukuru baada ya kama miaka 2 hv tangia nimalize chuo nilipata chance flan hv ambayo imenifanya kdg niwe mtu katika watu na yule manzi alienidharau alianza kuniletea SHOBO zake siku nimerudi mtaani na USAFIRI mmoja wa maana..yeye alizalishwa huko na janaume moja likakataa mimba sa hv yupo tu nyumbani hana inshu!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Unapenda ww kufanya kitu gan..au whts ur hobby!...tumia akili zako za kike kila kitu kitawezekan!...
Unajua hata matapeli inafikaga kipindi ujanja wao unafika mwisho...kila mtu anamjua...utaishije? Omba ht kaz za ndan kwa wahindi wanalipa.nafuu kuliko waafrica
Apo kwenye congo DRC niliandika tuu congo badae nikaongezea DRC ili iwe rahisi kueleweka kwasababu kuna congo mbili Kinshasa na Brazzaville
nisha fanya biashara ba mchizi aka lala na hela yote mbeleWakati nimemaliza chuo sina ramani nikakutana na mwana kitaa,tukapanga dili ya kununua kuku vijijini na kuuza mjini' tukasema tufanye simple research kabla ya kuingia vijiji vya ndanindani kwahiyo tukaona tutembelee vijiji vya karibu' tukajikoki asubuh moja hivi na baiskeli zetu za kukodi huku tumefunga matenga yetu nyuma ya baiskeli mpaka vijijini huku tunapita nyumba kwa nyumba kuulizia kuku, hapo tupo na bajeti kama ya 120' tukanza kununua kwa buku 7 Mpaka 8 kwa matembe na majogoo kwa buku 12 tulizunguka kuanzia alfajir mpaka usiku tukapata kuku kama 12 hivi'.Kwa bei amboyo tulikua nayo kichwani ni kwamba wale kuku wa buku 7 na 8 tunauza kwa buku 11 mbaka 12 na majogoo kuanzia 16 mpaka 18, dadeki ikafika asubuh hao na matenga yetu tunapita chocho kitaa wasituone si unajua noma wasomi tena na tenga la kuku inakua jau' ile tunatua tu sokoni kuku wa kutoka vijiji kama wote wametua sokoni' kumbe wanunuzi huwa hawanunui kuku mmoja mmoja walioko kwenye matenga ' huwa wanawahesabu then wanakulipa kwa ujumla wao , daa nakumbuka walikuja wateja kama watano hivi wote wanaishia bei ya elfu 80 kudadeki , kwahiyo tukawa tunaishia kuangaliana tu na mwana na kuwasepesha, kumbe time inazidi kwenda ikafika kama saa tatu asubh hivi tukaanza kujiona kama tupo sisi tu na kuku zetu, hapo mzee baba tumetoil kinoma tukipiga hesabu baiskeli tumekodi buku jero kutwa afu zipo mbili, msosi, Muda, bei ya kuku ,full kuchoka lakini kwakua ilikua ni kama sehemu ya kujifunza tukapiga moyo konde..huku na huku akatokea mwana mmoja ndio akatugea maufundi na lecture lakutosha kuhusu hiyo biashara' akatuambia tuzunguke kwenye baa na mama ntilie tutapiga pesa maana huwa wananunia kwa jumla' basi tukajikoki tukaanza kuzungusha mzigo' daa dakika kama 20 tukamaliza kuuza tukapata kama 140k hivi ila kimsingi ilikua hasara' tukarudi kwa jamaa akazidi kutupa maufundi namna ile biashara ilivyo nae kumbe ndio ulikua mchongo wake kutoa kuku vijijini kuleta town ' tukaona mambo si ndio hayo bhana full kumwamini jamaa tukaungana naye " tukatupia mtaji wetu kama 800k hivi hao vijiji vya mbali na wilayani tukakusanya wakutosha kuleta town, huku mchakato wote akiwa anausimamia yeye, tukagonga faida kimtindo tukafanya kama miezi 3 hivi jamaa akalala mbele kusikojulikana na mpunga wote mshenzi yule, na hapo ndio ikawa mwisho wa biashara
Sent using Jamii Forums mobile app
Yes....mishahar siku zote haitoshi...pole
Noma sanaJINSI NILIVYO INGIA KWENYE KUSAFIRISHA MIRUNGI BILA KUJUA
Msi mind mwandiko
Ilikuwa kipindi niko kitaa tu sina hili wala lile nilikuwa mtu wa mishe za town hasa katika maswala ya kuchukua order za kuku kwenye ma super market naenda kutafuta wale wazito kwa bei ya 6000 nakuja kuuza kwa 6500. Kwa week nilikuwa niko poa tu.
Sasa majanga ni pale siku manager alikuja kujua deal kamili kuhusu upigaji wangu kibarua kikaota nyasii.
Nikaa anza kusota mtaani na kuangalia njia nyingine, kama unavyo jua vijana kipindi hicho nilikuwa ni mtu wa kujichanganya kiasi sio sana so nikawa ni mtu wa tungi sana na kila siku zinavyo zidi kwenda ndo kabisaa nazidi kuwa pierre, sasa kuna jamaa alikuwa akija sehemu ninapo kula tungi huwa hakai sana akija na demu wake ni dakika mbili wanaagiza nyagi wana ongea anaingia cha fasta gesti na wanaacha tungi mezani wanasepa zako. Nilikuwa nawaona mara kwa mara nikienda pale.
Siku nimekaa sina hili wala lile niko na glass yangu nimetulia na ki nokia torch changu naona jamaa kaingia na aka kaa akawa kama ana msubiri demu wake akanipa hii tukasalimia fresh.
Mara akaanza kutoa lawama pale kuhusu mademu kuchelewa na amemuambia tokea kitambo sana kuwa aje nikachangia mada kiasi nikaona kasogea tuka piga story.
konyagi ndogo yake ikawa imeisha akaagiza akanichukulia na mimi safari na jogoo 2 fresh.
Basi jamaa akaniuliza ishugani nafanya nikamwambia sina mishe basi akaniambia kwa mwonekano wako mzee unafaa kabisa kuungana na mimi nikamtania kumwambia nini kuuza bangi au akasema hapana akadai kuwa anasafirisha mizigo kutoka boda mpaka arusha na huwa hailipiwi kodi so ni kama magendo hivi akadaii atakuwa ananipa nauli pamoja na deliver salary.
Nikasema hii deal basi nikampa number pale nikawa na sikilizia.
Siku napigiwa akaniambia dogo vaa vizurii kuna ishu unapelekea leo naona mzigo ni mwingi sana. Basi nafika akanichukua na gari tukaenda maeneo flani ndanii hukoo kuna nyumba ina fensi safi tukaingi na kulikuwa hapaishi mtu wakati nyumba ni kubwa tu.
Wakanipa beg nikasikia harufu ya mirungi mzee niliogopa sema nikajikaza wakanipa moyo wakadai wewe kazi yako ni kupeleka na kufikisha basi. so acha wasi wasi.
Wakafunga wao waka pack kwenye gari lao aisee kwa staili ile hakuna mtu anaweza jua.
Wakasema ni pande mabasi makubwa ya kutoka x kwenda x ndo salama nikapanda na hapo nyuma walinipiga unyunyu mkali sana ili ninukie kuepusha harufu ya mirungi asikwambie mtu ilikuwa natetemeka balaa mtu akiniangalia tu nahisi amenishtukia gari ikisimama najua ni mimi yani nilikuwa sina amani kabisa.
Thank god nikafika eneo lenyewe nikashuka nikapiga simu nikaa ambiwa kuwa ni subiri kumbe bwana wanakaa mahali wanakuangalia kwanza kisha wanakupigia simu kama mara 2 au 3 ndo wanakuja.
jamaa kafika pale akanipokea kisha nikamfata kwa nyuma tukawa tunaenda kama tuna panda gari stend njiani akanipa buku 15 akaniambia kuwa wewe sepa tusha malizana.
Dhaaa aisee niliona nimetua mzigo nikafanya kama mara 8 hivi wakanitema maana nilikuwa najiamini kuliko wao.
Na kuna mmoja alidakwa faini yake ni zaidi ya milioni 8 na kama boss wako masikini basii jua ndo tuna kusahau.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa baadae aliishi kwa 90K kwa mwezi
Mbona aliishi, mbona maisha yaliendelea
Sent using Jamii Forums mobile app
Sometimes mtu unaweza hisi maisha yamekupiga ila ukitoka na kusikiliza wengine unapata kila sababu ya kumshukuru Mungu
Binafsi maisha yalinipiga ila si kwa kukosa vocha ama chakula ama nauli ila ni kwa kile nilichoamini napaswa kufikia ktk maisha bila ya kuajiriwa
Hivyo nilikataa nafasi kadhaa za kuajiriwa hapo naelekea kumaliza chuo July 2018 bro wangu akiwa na cheo kampuni x ya utalii akaniambia kuna nafasi maliza chuo uje upige kazi temporal kama store keeper bila chenga nikamchana sitaki kuajiriwa,,, metoka chuo direct ifakara kulima mpunga huko sikurudisha hata mia katikati hapo nikiusubiria mpunga nikauza sana mayai ya kuchemsha na sambusa... by dec 2018 nikawa na uhakika dili la mpunga lishabuma na mebaki sina hata mia pamoja na wenzangu tukapata idea ya kulima maharage Gairo tukaweka mipango sawa then nikarudi home maza alikuwa mgonjwa sana home pale nikaungaunga mixer kuomba nikapata laki 6 nikatoa washikaji wakakodi mashamba na hiyo hiyo ikatosha hadi kwenye mavuno tulikodi heka 20... Wakati wa mavuno wenzangu wakawa na harakati nyingine za hapa na pale mi ikawa ndio wajibu wangu kwenda kusimamia uvunaji huko huko nikasoma gap la kununua maharage kwa wakulima na kuyapeleka town kuuza mixer nilifanya juu chini yale mashamba ya pamoja nikavuna fasta na kuuza mzigo ile hela nikawa nazungushia kununua na kuuza + 2m niliyoomba home kusema kweli ile biashara haina hasara na hela niliiona kiasi chake kilichonikwamisha niliuugua kama mwezi nipo hoi hivyo nilivyopoona msimu ukawa ndio unaishia na hela ya shamba tukagawana ila nikawa bado na chenchi za kuendelea kununua gunia kadhaa na kupeleka town... By sept 2019 nikapata fursa ya kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara ya nafaka ulioitishwa na waziri wa kilimo hapo niliziona fursa kibao na nikapata motisha wa kurudi shamba kupambana upya... Nilirudi ila msimu ulikuwa umefika mwisho haswaa maharage hamna target ikawa ni kusubiria ya mtukula Uganda nikiwaza kwenda huko na shs 3m zangu naona haitoshi ila nikizungumza na watu wananiambia inatosha sana kibaya hapo ni October na msimu unaanza DEC kuelekea January halo nilipata stress na hofu ya kuitumia pesa kutokana na kukosa mzunguko hadi ikafikia hatua ya kuomba kibarua ili nijipange kwa msimu utakaokuja...
Mungu mkubwa kabla ya kupata hicho kibarua ikatokea mama mmoja aliyekuwa ktk ule mkutano tumefahamiana kwa bahati mbaya tu yaan ilitokea mekosea namba nikimtafuta mtu mwingine aliyehit ktk ule mkutano ambae nae alikuwa akimtafuta pia basi nikampa mawasiliano yake mixer story tukajuana na nikawa nampigia kumuuliza feedback kama amefanikiwa kupata msaada toka kwa yule mtu... Siku ya siku nawaza kurudi home akaniambia nina shida sana ya mahindi fanya kunitafutia yeye anasaga sembe na dona nikaingia machaka kadhaa mwisho nikapata chimbo la mahindi na kuyasafirisha hadi dsm kusema kweli baada ya kuanza hiyo biznez upepo ulichange na stress zikanipungua maana nilifikia hatua ya kufata vyeti chuo ili nikaombe kazi... Huu ni ufupisho wa ufupisho sababu niliyofanya na kuyapanga hapo ktkt ni mengi siwezi andika yote ikiwa ni pamoja na kupoteza hela na muda kwenye drop shipping kupitia darasa lililoanzishwa na bwana frank frain Byera Deo Corleone
Mpaka sasa msimu umeisha ila namshukuru Mungu mepata network kubwa dsm na mtaji umekuwa ghafla toka kusafirisha mahindi tani 5 hadi 11 hapa kuna pesa fulani niliomba nikaongezea kwenye mtaji na kupitia hili zao najiona nikitengeneza pesa ya maana mwaka huu... Mungu tu ajalie na kuepusha balaa yoyote
#2020 twenty twenty, twenty plenty
Nimeuza sana screpa za home,majembe yasio na mipini makalai,jalo la mkaa.
Mpaka bi mkubwa akawa anahofia sufuria zake.
Haso la maanaSometimes mtu unaweza hisi maisha yamekupiga ila ukitoka na kusikiliza wengine unapata kila sababu ya kumshukuru Mungu

Pole sana mkuu,yani ulivyomtaja tu huyo jamaa apo nikajua tu lazima aliwaliza tu.Wakati nimemaliza chuo sina ramani nikakutana na mwana kitaa,tukapanga dili ya kununua kuku vijijini na kuuza mjini' tukasema tufanye simple research kabla ya kuingia vijiji vya ndanindani kwahiyo tukaona tutembelee vijiji vya karibu' tukajikoki asubuh moja hivi na baiskeli zetu za kukodi huku tumefunga matenga yetu nyuma ya baiskeli mpaka vijijini huku tunapita nyumba kwa nyumba kuulizia kuku, hapo tupo na bajeti kama ya 120' tukanza kununua kwa buku 7 Mpaka 8 kwa matembe na majogoo kwa buku 12 tulizunguka kuanzia alfajir mpaka usiku tukapata kuku kama 12 hivi'.Kwa bei amboyo tulikua nayo kichwani ni kwamba wale kuku wa buku 7 na 8 tunauza kwa buku 11 mbaka 12 na majogoo kuanzia 16 mpaka 18, dadeki ikafika asubuh hao na matenga yetu tunapita chocho kitaa wasituone si unajua noma wasomi tena na tenga la kuku inakua jau' ile tunatua tu sokoni kuku wa kutoka vijiji kama wote wametua sokoni' kumbe wanunuzi huwa hawanunui kuku mmoja mmoja walioko kwenye matenga ' huwa wanawahesabu then wanakulipa kwa ujumla wao , daa nakumbuka walikuja wateja kama watano hivi wote wanaishia bei ya elfu 80 kudadeki , kwahiyo tukawa tunaishia kuangaliana tu na mwana na kuwasepesha, kumbe time inazidi kwenda ikafika kama saa tatu asubh hivi tukaanza kujiona kama tupo sisi tu na kuku zetu, hapo mzee baba tumetoil kinoma tukipiga hesabu baiskeli tumekodi buku jero kutwa afu zipo mbili, msosi, Muda, bei ya kuku ,full kuchoka lakini kwakua ilikua ni kama sehemu ya kujifunza tukapiga moyo konde..huku na huku akatokea mwana mmoja ndio akatugea maufundi na lecture lakutosha kuhusu hiyo biashara' akatuambia tuzunguke kwenye baa na mama ntilie tutapiga pesa maana huwa wananunia kwa jumla' basi tukajikoki tukaanza kuzungusha mzigo' daa dakika kama 20 tukamaliza kuuza tukapata kama 140k hivi ila kimsingi ilikua hasara' tukarudi kwa jamaa akazidi kutupa maufundi namna ile biashara ilivyo nae kumbe ndio ulikua mchongo wake kutoa kuku vijijini kuleta town ' tukaona mambo si ndio hayo bhana full kumwamini jamaa tukaungana naye " tukatupia mtaji wetu kama 800k hivi hao vijiji vya mbali na wilayani tukakusanya wakutosha kuleta town, huku mchakato wote akiwa anausimamia yeye, tukagonga faida kimtindo tukafanya kama miezi 3 hivi jamaa akalala mbele kusikojulikana na mpunga wote mshenzi yule, na hapo ndio ikawa mwisho wa biashara
Sent using Jamii Forums mobile app