Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Twenty twenty, twenty plenty nimeipenda brother
Sometimes mtu unaweza hisi maisha yamekupiga ila ukitoka na kusikiliza wengine unapata kila sababu ya kumshukuru Mungu

Binafsi maisha yalinipiga ila si kwa kukosa vocha ama chakula ama nauli ila ni kwa kile nilichoamini napaswa kufikia ktk maisha bila ya kuajiriwa

Hivyo nilikataa nafasi kadhaa za kuajiriwa hapo naelekea kumaliza chuo July 2018 bro wangu akiwa na cheo kampuni x ya utalii akaniambia kuna nafasi maliza chuo uje upige kazi temporal kama store keeper bila chenga nikamchana sitaki kuajiriwa,,, metoka chuo direct ifakara kulima mpunga huko sikurudisha hata mia katikati hapo nikiusubiria mpunga nikauza sana mayai ya kuchemsha na sambusa... by dec 2018 nikawa na uhakika dili la mpunga lishabuma na mebaki sina hata mia pamoja na wenzangu tukapata idea ya kulima maharage Gairo tukaweka mipango sawa then nikarudi home maza alikuwa mgonjwa sana home pale nikaungaunga mixer kuomba nikapata laki 6 nikatoa washikaji wakakodi mashamba na hiyo hiyo ikatosha hadi kwenye mavuno tulikodi heka 20... Wakati wa mavuno wenzangu wakawa na harakati nyingine za hapa na pale mi ikawa ndio wajibu wangu kwenda kusimamia uvunaji huko huko nikasoma gap la kununua maharage kwa wakulima na kuyapeleka town kuuza mixer nilifanya juu chini yale mashamba ya pamoja nikavuna fasta na kuuza mzigo ile hela nikawa nazungushia kununua na kuuza + 2m niliyoomba home kusema kweli ile biashara haina hasara na hela niliiona kiasi chake kilichonikwamisha niliuugua kama mwezi nipo hoi hivyo nilivyopoona msimu ukawa ndio unaishia na hela ya shamba tukagawana ila nikawa bado na chenchi za kuendelea kununua gunia kadhaa na kupeleka town... By sept 2019 nikapata fursa ya kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara ya nafaka ulioitishwa na waziri wa kilimo hapo niliziona fursa kibao na nikapata motisha wa kurudi shamba kupambana upya... Nilirudi ila msimu ulikuwa umefika mwisho haswaa maharage hamna target ikawa ni kusubiria ya mtukula Uganda nikiwaza kwenda huko na shs 3m zangu naona haitoshi ila nikizungumza na watu wananiambia inatosha sana kibaya hapo ni October na msimu unaanza DEC kuelekea January halo nilipata stress na hofu ya kuitumia pesa kutokana na kukosa mzunguko hadi ikafikia hatua ya kuomba kibarua ili nijipange kwa msimu utakaokuja...

Mungu mkubwa kabla ya kupata hicho kibarua ikatokea mama mmoja aliyekuwa ktk ule mkutano tumefahamiana kwa bahati mbaya tu yaan ilitokea mekosea namba nikimtafuta mtu mwingine aliyehit ktk ule mkutano ambae nae alikuwa akimtafuta pia basi nikampa mawasiliano yake mixer story tukajuana na nikawa nampigia kumuuliza feedback kama amefanikiwa kupata msaada toka kwa yule mtu... Siku ya siku nawaza kurudi home akaniambia nina shida sana ya mahindi fanya kunitafutia yeye anasaga sembe na dona nikaingia machaka kadhaa mwisho nikapata chimbo la mahindi na kuyasafirisha hadi dsm kusema kweli baada ya kuanza hiyo biznez upepo ulichange na stress zikanipungua maana nilifikia hatua ya kufata vyeti chuo ili nikaombe kazi... Huu ni ufupisho wa ufupisho sababu niliyofanya na kuyapanga hapo ktkt ni mengi siwezi andika yote ikiwa ni pamoja na kupoteza hela na muda kwenye drop shipping kupitia darasa lililoanzishwa na bwana frank frain Byera Deo Corleone

Mpaka sasa msimu umeisha ila namshukuru Mungu mepata network kubwa dsm na mtaji umekuwa ghafla toka kusafirisha mahindi tani 5 hadi 11 hapa kuna pesa fulani niliomba nikaongezea kwenye mtaji na kupitia hili zao najiona nikitengeneza pesa ya maana mwaka huu... Mungu tu ajalie na kuepusha balaa yoyote

#2020 twenty twenty, twenty plenty

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha mafupi sana, hakuna kimfaacho duniani binadamu zaidi ya kuabudu, kula, kunywa na kufurahi, na yote hayo yanahitaji hela (kutafuta) kama zipo sioni mantiki ya kujinyima
Baada ya kumaliza chuo niliyofautiana na mzee. Nikasepa zangu na kuanzisha biashara ya juisi k.koo.

Niliuza juisi kwa mkokoteni. Yani natengeneza kwenye ndoo alafu napaki sehemu nauza. Nilikuwa nanunua bites kwa jamaa mmoja hivyo nauza na juisi. Faida haikuwa kubwa sana lkn changamoto zikawa nyingi sana.

Kuna siku niligonga garibya jamaa mmoja na mkokoteni wangu maglasi yote chini paaaaa. Kama unavyojua wamachinga wa k.koo kila mtu kelele wengine wakishangilia.

Kijana nimejawa hofu na woga, jamaa mwenye gari alinizingua sana ukicheki Gari nimepasua taa ya nyuma na bampa.

Watu waliniombea pale lkn wapi. Akanisachi na kuchukua pesa zote na mkokoteni akabeba.

Mambo ya biashara yakafia pale. Nikarudi zangu gheto na kuwaza nianze fanya nini. Baada ya wiki ya msoto ndipo nikafanya maamuzi ya kwenda kuomba kazi kwa mjomba wangu ambae anamiliki maukumbi makubwa ya harusi.

Sikutegemea kama angenipokea vizuri vile, palepale nikapelekwa kwenye moja ya ukumbi wake na kutangazwa meneja.

Nyota ndio ilianza kung'aa kuanzia hapo. Mambo si mabaya sasa, watu waliokuwa wananijua nauza juisi walikuwa hawajui kama nimesoma. Leo wakinikuta wananiambia nilikuwa USALAMAA wala sio muuza juisi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Watu tumesota sana, ndio maana sipendi kuishi maisha ya kishenzi, kula sana bata.
Maamaaeee!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] pole boss
Aise umenikumbusha kiwanda cha mo dewj nilibebeshwa cement, mbolea mafuta vindoo vidogo mnabeba vinne kwa pamoja kushoto 2 kulia 2 kazi ilinishinda sku ya kwanza tu nikadanganya dam zinatok puan ela skupewa nikarud hom sku ya pili mgongo unauma balaha sikurud tena aya maisha oneni tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha Yana Vingi Sana

Mimi Niligonga O Advance Bihawana Hapo Dodoma

Kurudi Kitaa Dah Raia Wote Wanajua Mim Naenda Chuo Muda Ulipofika Nikawa Bado Nipo Nikasingizia Mkopo Kumbe Nilipiga Bashite La PCB Yaan Pure 0 (Gs Na BAM Zote F)

Basi Nikamuomba Bro Mmoja Akawa Ananipa Boda Yake Nakula Vichwa Usiku Huwezi Amini Siku Ya Kwanza Usiku Nikagonga Mtu Nikapelekwa Sero Nikakaa Wiki.

Nipo Ndani Nikawaza Vingi Sana Ndipo Nilipotoka Nikajiunga Na Jf Nikapata Kazi Ya Lodge Humu Humu Mshaara 100k Ipo Huko Airport Lakin Shughul Yake Sio Ya Kitoto, Unafua Shuka Watu Wamelana Ndogo Yaan Mav Kabisa Na Hakuna Gloves Kabisa Yaan Unapitia Tabu Mpaka Unaona Dah Hapa Siwez Ila Ukikumbuka Msoto Wa Home Unafanya Then Unasahau, Nilikaa Pale Miez Mitano Nikamuibia Ibia Nikapata Kama 2M.

Nikarudi Kitaa Nikanunua Boda 1.2M Kwa Bro Kuja Kuchunguzwa Kumbe La Wizi Nikaenda Tena Ndan Mwezi Sema Bi Mkubwa Akaja Kunitoa.

Nikarud Mtaan Tena Nikawa Najichanganya Tu Mpaka Nikpata Nafasi Ya Chuo Diploma CO.

Kufika Chuo Ndio Nikaanza Kujifanya Fund Simu Na Laptop, Mtu Akileta Simu Naenda Choon Na Google Jins Ya Kuifungua Na Tatizo Lake, Nikawa Nafanya Hivyo Na Zinapona Na Nyingine Zinazima Kabisa But Nashukuru Mungu Hii Mishe Iliniingizia Pesa Sana Na Ndio Naifanya Mpaka Now Japo Ka Diploma Ninako Ila Sikatumii.

#Wilmer


Sent using Jamii Forums mobile app
Hii kazi ya lodge na mimi niliomba asee...dah.
 
2017 ulikuja kuomba connection ya kazi humu, mtaji wako ulotoka nao chuo ulikata? Je ulikata kwa mazingira yapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ofcourse nilileta uzi humu huku nikiwa naendelea na biashara pia japo haikua ikienda vizuri sana,na sababu ilikua hiyo product imekua nyingi sana sokoni tena kwa bei nafuu wakati mimi nikiuza bei kubwa kiasi(quality)so wateja wengi walihamia kwenye bei rahisi.

Pia sikua serious sana na hiyo biashara, nilitamani nipate kazi ili nipractice nilichokisomea darasani pia aisee, nashukuru kupitia uzi wangu nilipata response nzuri,hatimaye nikapata kazi na nikafanya for a year.Jf idumuu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Rubeho msimu wa maharage huwa ni mwezi wa ngapi mpk wa ngapi? Vipi bei yake huwa inakuaje ?
Pole kwa kupigwa na upepo wa drop shipping.
Mwaka huu mvua hazitabiriki mfano sasa maharage yashakomaa tayari kuvunwa ila mvua inanyesha yanaharibika ila mwezi wa saba ndio mavuno makubwa bei inategemeana na wingi wa mavuno
 
Back
Top Bottom