Sakayo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 56,366
- 161,495
Mbona kulegea jamani mkuu
Mbona kulegea jamani mkuu
Unakumbu kumbuka sanaTayari nimeweka ile story
Nilikuwa nasoma kazi za "kimasihara" hahaSis darling umekujaje huku[emoji23][emoji23][emoji23]
Hivi wewe ndio e$9¥?[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
Espy, Atoto ndio mie.Hivi wewe ndio e$9¥?
NB:haka kastory nimehadithia juu juu tuu kwasababu siwezi kuandika sana,
Katika harakati za maisha na ugumu wa maisha tulikutana na mkongomani story za hapa na pale mpaka kuzoeana akasema kama tupo tayari kujilipua kuna sehemu uko congo DRC kuna almasi nje nje ,ni kuingia kwenye maji tuu na kuzitafuta basi tukajipanga ,tukaenda kwa papa mmoja ivi tukamuuliza kama anaweza kununua almasi ya congo ambayo itakuwa imeingia kwa njia za panya akasema anaweza ,sisi hatukuwa vizuri kifedha hivyo tuliona mambo ya kufatilia vibali yatatukatisha tamaa,kuna jamaa akatuchorea ramani ya njia za panya na gharama yake mpaka kufika kasai tshikapa congo,
Tulienda kwa kupitia Rwanda,tukatoka Rwanda kwa njia za Panya tukaingia bukavu ,tulitulia bukavu kwa siku kadhaa,tukaanza safari ya kuitafuta tshikapa ipo mpakani mwa congo na angola,ilituchukua wiki nzima kufika huko kwa sababu ya miundombuni ya barabara na usafiri pia ulikuwa wa shida na enzi hizo kulikuwa hamna boda boda kama sasa,hatimaye tulifika tshikapa ,tulipumzika kwa siku kadhaa na kuzungumza na wenyeji ili kupata abc’s za sehemu ambayo ina migodi ya almasi lakini walitushauri ni hatari sana kwenda huko migodini kwani hakuna usafiri wa uhakika ni bora kama tuna pesa tuishie kijiji cha kamabue na tununue diamond kwa wachimbaji wadogo,sisi hatukuwa na pesa ya kuweza kununua maana mpaka kufika huko tumeunga unga basi tuliambiwa kuna nyoka sana inatupasa tubebe dawa ya sumu ya nyoka,iyo dawa ni unga unga mweusi,
Siku siku tukaanza safari ya kuelekea kijiji cha kamabue ili tuweze kuifikia migodi ilitupasa tusafiri kwenye mto kasai kwa kutumia boat ambayo ilikuwa ni tia maji tia maji,lengo ilikuwa ni kufika sehemu ambayo wanatafuta diamond chini ya maji,nyoka walikuwa ni wengi sana na tulianza kuingiwa na hofu,hatimaye tulifika sehemu tukatia nanga pamoja na mwenyeji wetu,tulivyoshuka tuu hatujakaa sawa mwenzetu akagongwa na nyoka mkonononi sijui alikuwa anafanya nini,yule mwenyewe wetu akatusadia kumpa huduma ya kwanza kwa kutumia ile dawa kienyeji na ikatupasa turudi haraka tshikapa kumpeleka mwenzetu hospitali ilituchukua siku tatu kufika tshikapa kuna vijiji tulikuwa tukifika inabidi tulale,Mwenzetu alipona na hatutaka tena kurudi kule migodini ,tukasema ni bora tukajipange tutafute mtaji wa kwenda kununua kwa wachimbaji wadogo.Asanteni
SK2016
Gallius
dexterous
The 13
WAKU-GOOGLE
[B][SIZE=5]Root[/SIZE][/B] mkorinto
Apo kwenye congo DRC niliandika tuu congo badae nikaongezea DRC ili iwe rahisi kueleweka kwasababu kuna congo mbili Kinshasa na Brazzaville
Hivi mkuu wewe ni ke/me? Naomba unijibu maana kwa uhalisia wako wa ke huwa navutiwa nawe. Jibu lako litanisaidia.Apo kwenye congo DRC niliandika tuu congo badae nikaongezea DRC ili iwe rahisi kueleweka kwasababu kuna congo mbili Kinshasa na Brazzaville
MdadaHivi mkuu wewe ni ke/me? Naomba unijibu maana kwa uhalisia wako wa ke huwa navutiwa nawe. Jibu lako litanisaidia.
Tulikuwa na wanaume piaMdada ulikuwa unaenda Congo?? Ndani ndani kutafuta madini? Interesting
Wish I could see you if not knowing...
Sitarudia tena mimi
Ila Ref Wayne kiboko [emoji114][emoji114] mimi sasa hivi sitredi ila kwenye channel yake sijatoka, mara moja moja huwa naingia kuchunguliaNdo unamjua leo. Sandi sio bingwa ni ref wayne tu. Na wengine wachache ninao wajua
Sent using Jamii Forums mobile app
Ujana maji ya moto sis darling!!!Nilikuwa nasoma kazi za "kimasihara" haha
Hahaha, nasoma huku nacheka. Courage kubwa sana hiyo, kuna maeneo napita huwa naona vijana me na ke wanahubiri live, sasa nafanya kukuona unavyotangaza injili[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Umewezaje kunicheka jamani!! Nilihubiri mnoo, huo ndo ulikuwa mtaji wangu sikuwa na mtaji wa kuanzia kabisaa! Wazo likaja naweza kuhubiri injili nipate sadaka!
Hii ndiyo passage bora kwangu kwa mwaka huu 2020Basi wakuu,nilipoenda chuo nikaendeleza harakati zangu,nilikua nauza nguo,kofia,sabuni hasa hasa manjano akina dada wanazipenda sana hizi,liwa,n.k. Nikawa dalali wa simu na assets mbalimbali. Yani nilikua bize haswaa muda wote kichwa yangu inawaza pesa tu,japo mkopo sikukosa japo kwa asilimia kadhaa,hapo mixer niliambatanisha vyeti vya vifo vya kutosha,yani full viambata.
First year mapema semester ya pili nikajichanga vijisent vyangu vya mtaa na nyingine nyingine nikachukua boxer mpyaaaa!!! then nikamuachia mwanangu Yuzzo kitaa apigie kazi.
Mikosi ikaanza upyaa...
Third year final semester nikaibiwa hiyo pikipiki,wahuni walikata rock wakatembea nayo,(kilikua ni kitendo cha kuingia ndani na kuchukua koti,kutoka nje wameacha alama tu za matairi chini. Daah niliumia sana but nikapiga moyo konde. Hapo katikati sijasimulia jinsi miradi ya saloon,chips na mitumba ilivyokufa kisa wana,sitaki story iwe ndefu.
Msoto mkali baada ya Chuo.
Basi wakuu,nikamaliza chuo then nikarud kitaa kupambana,hapo sina A wala B,kila kitu kimepukutika,nina akiba tu kiasi. Nikajaribu kucheki upepo street nikaona pagumu, nikapata wazo la kwenda kuuza moja kati kiwanja changu nje kidogo ya mji(hivi nilinunua bei ya mbuzi kipindi cha ufreelancer wangu,sehemu fulani panaitwa Kitasengwa).
Sikua na namna nikauza then nikamchek mwanangu fulan yuko Mbeya tukazama bush kwako kuchek mali nije nayo town (kosa kubwa kutokusoma alama za nyakati) daah mvua ikaharibu kila kituuu!! Tukakwama bush kama week mbili nikajikuta nazidi kuishiwa tu na hakuna tumaini la kuokoa mzigo.
Niko bush nahangaika napata taarifa huku getto wameiba kila kitu!
Daah wakuu! Nilitamani hata nitoweke tu duniani,nikajiona si kitu mbele ya uso wa dunia! Nikawaza mengi sana! Why Mungu ananiacha nitaabike hivi?
Nilidhoofu sanaaa,sikua hata na hamu ya kutafuta pesa tena! Nikajiona ni mtu nisiepiga hatua katika maisha. Yani bush nmekula loss na huku town wameniliza kila kitu daah wakuu!!
Kwa kifupi nilichoka nikachakaa,hali ikazidi kuwa mbaya nikaona bora nirudi kwa jamaa wa TIGO,jamaa wakanipa mashine zile za kusajilia line kwa alama za vidole "FAMOCO" kidume nikaingia kitaa daah!
Nikaona hapa hakuna namna wacha nipige kazi,issue nzuri ni kuwa mtu akiniona alikua anadhani either nimetoka makao makuu au niko kitengo tofauti na kile cha kusajili,hapa nazungumzia usmart,convincing,e.t.c. So nilipiga noti kwa kiasi fulani mpaka December 31 nilikua nishapata kianzio nikaachana na ile kazi, ijapokuwa kwasasa bado sijakaa sawa kabisa ila angalau ninacho kianzio.
Hayo ni baadhi tu ya niliyopitia wakuu,jambo la msingi katika maisha ni kutokukata tamaa,haijalishi ni magumu kiasi gani unapitia. Ukianguka usilale hapo hapo,inuka songa mbele kwa umakini zaidi.
Maisha ni kama mshale,ili uende mbali zaidi ni lazima uvutwe sana nyuma,so GOD PULLS US BACK TO SHOOT US FORWARD.
Sent using Jamii Forums mobile app