Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Daah pole sana mzee mi pia nimepitia Garage ila sikupata changamoto kama zako ila kweli hua hawakulipi kuna dogo nilimkuta hapo Garage ana miaka miwili analala kwenye magari katokea Mtwara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo wewe unakaa kijiweni unaomba watu wafe ilo upate ulaji [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna vipigo aisee huwezi hata kufanya hiyo kazi ya ajabu
 
Duuh, pole na hongera kwa kuvuka mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipohitimu Chuo nikawa sina hata mia, nakaa mpaka siku 3 sijala.

Mpaka nikilala wakati mwingine, tumbo linahamia upande mmoja - wakati huo huo Transcript, Academic, Enrolment Baraza na License natakiwa kulipia kama Tsh 200,000 ili nipate uhalali wa kutumia taaluma yangu.

Waswahili nao majungu mwanzo mwisho. Kila nikiomba hata kazi Car Wash sipati.

Hapo ndio nikaanza kuuelewa ule msemo wa "What do you do for a living huwa una maana gani ?"

So, Nikawaza kwanini nisianze kuokota machupa.

Yaani Natoka Ukonga naenda hata Mburahati huko wasikonijua Naokota Nauza then narudi Jioni ?

Baada Ya Kutafakari sana, nikaghairi.

Nikaamua kuingia Kampuni za ulinzi. Yaani wakati naftafuta kazi hizo hata gari zenyewe nilikuwa napata nauli kwa kuunga sana, na kwasababu ya njaa nusura siku moja nizimie kwenye daladala ( Kwasababu Ya Foleni na Kusimama )

Mpaka sasa niko huku mwaka wa pili huu.

Mimi ni mwoga sana ninapoona hakuna tumaini la kupiga hatua hata kidogo tu kwenye maisha, huwa nakonda ghafla.
 
2011 ilivyostishwa kazi yangu ktk kampuni nilipigika sana nikaamua kukimbilia katika kisiwa kimoja kilichopo ziwa victoria (Ikuza) nikiwa huko nilijikuta nimefanya kazi ambayo ni tamaa ya pesa

niliingia ktk hifadhi taifa ya rubondokinyume na taratibu kwenda kutega samaki usku wa manane nikiwa mgeni mimi pekee wenzangu walikua wenyeji siku nyingi walikua wakiingia ikiwa ndio malayangu ya tatu kuingia tulikamatwa na watu wa dolia gemu

kipondo tulichopewa ni cha mbwa koko miaka mi3jera hadi leo mguu wangu wa kulia una hitilafu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka Jana nilipigika Sana madeni Kila Kona. Nikafikiria Sana nikaona hapa dili ni kuwa BABA NTILIE, nikatafuta masufuria na sahani na vyombo vingine nikapata Ni biashara inalipa kwa maeneo ya huku nilipo kwani nilishafanya utafiti kwa baadhi ya MAMA NTILIE. Tatizo kupika sijui ikabidi niuze vyombo vyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mlikuwa mnatumia kemikali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka leo bado unafanya ulinzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…