Wakati Urusi bado wanahangaika na HIMARS, sasa USA kutuma 'VAMPIRE' Ukraine

Nimeiona hii CNN mkuu aisee huyu mnyama ni hatar
 
Us huenda ana silaha ambazo hazijulikani majina na madhara yake.
Mzee Putin pole sana
 
Simpendi mmarekani kabisa lakini urusi imeyumba sana inapigana kizamani imeniangusha, nasema uongo MK254
Hapana .mrusi anajifanya .kama vita imemshinda .hii si kweli ebu jaribu kufikiria toka wa magharibu watume machuma yao ukrein nn kimebadilika? Mrusi anakuambia silaha anazotumia sasa nizile toka vita kuu ya pili. Zana zake mpya hajazigusa kabisa anasubiri wa magharibi wamalize kutoa zakwao ndiyo muone mrusi anafanya nn ukrain .
 
Sio kwa Urusi! Hapo Marekani atatoa mikopo mingi kwa Ukraine ila akija kushtuka Ukraine yenyewe haitokuwepo tena.
Yani kwa kifupi Marekani atakula hasara kubwa itakayopelekea anguko lake
Daaa yaani uchambuzi mwingine huu!!yaani wewe uliyopo matombo huko, umeliona hilo kuliko hao maprof.wa duniani!!!hahaaa
Eti atakuja kula hasara babu kubwa!!!lile taifa achana nalo unafikiria ni dola trilioni ngapi zilitumika kwenye vita afganistani?, leo karibia dunia nzima kuna bases za kijeshi za USA, tena ni kwa gharama zao, mashirika yote ya kimataifa mchangiaji mkubwa ni yeye, umeshaona ametetereka?!mbona bado ndio taifa linaloongoza kwa uchumi duniani?
 

Ha ha ha!!! Mlisheherekea sana wakati Mrusi anaanza kuparamia Ukraine, leo anapokea za uso mnaanza kulalamikia Marekani.
 
Angemheshimu tu mkubwa! Kama wanavyofanya baadhi ya majirani zake. Putin asingekubali kirahisi tu Ukraine kuwa mwanachama wa NATO.
Mbona hajawahi kuwa mwanachama wa NATO. Putin hata alipoitwaa Crimea 2014 Ukraine bado haikuwa NATO. Labda kitu pekee Ukraine angefanya ni kutulia aingiziwe vidole...

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Usiwe unadanganyika kirahisi,,hizo S.3000 na S.4000,jumlisha hypersonic mesiles alikuwa nazo kwenye nyakati za vita ya pili ya dunia!? Warusi ni mabigwa wa propaganda pia. Wakati Putin anaanzisha huo upuuzi wake alitarajia kazi ingeisha ndani ya siku tatu hadi wiki moja.
Sasa amekuwa kama sangara aliyenaswa na mfupa wa gogogo, kuumeza hawezi na kuutema hali kadhalika!

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Jamaa hajui kitu huyo ndo maana mimi nikampuuzia. Russia ametumia mpaka laser weapons ili kupambana na dronea za ukraine. Masilaha yote hayo wasemaje ni ya WW II? ni kumsamehe tu.
 
Mbona hajawahi kuwa mwanachama wa NATO. Putin hata alipoitwaa Crimea 2014 Ukraine bado haikuwa NATO. Labda kitu pekee Ukraine angefanya ni kutulia aingiziwe vidole...

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Mwaka huu wa 2022 huyo Zelenysky alipanga kuiingiza Ukraine kwenye Umoja wa Ulaya na NATO! Jambo ambalo Putin alishalipinga tangu mwanzo. Ila sasa kwa sababu huyo Zelenysky alishajazwa upepo na Marekani, akajifanya mkaidi.

Na mwisho wa siku Putin akaja na hii oparesheni yake maalum ya kutaka kuiindoa kimabavu hiyo Serikali ya Ukraine yenye mafungamqno na nchi za magharibi na Marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…