Mkuu, sera zilikwishatengenezwa miaka zaidi ya 20 sasa kuhusu kuifanya Russia iwe kainchi chenye kuwategemea wao NATO na Marekani.
Hiyo ya kusogea kidogokidogo pembezoni kwa Russia kutaka kuizunguka, kisha kuivamia na kuigawa mazima na baadae kupora rasilmali zake yabaki kuwa ndio sera pekee kwa sasa.
Hiyo ndo sababu Marekani na NATO wataendelea kusaidia silaha hadi hapo wanaaamini Russia itaanguka na itachukuliwa nao na Ukraine ndio awe mbadala wa Russia.
Tufahamu kuwa sasa hivi NATO na Marekani wamesema wazi kuwa maadui wao ni Russia na China hivyo lazima waongeze bajeti zao za ulinzi kwa ajili ya kukabiliana nao, ni vita ya kugombania maeneo yenye rasilimali na kuyamiliki kwa nguvu au "Hegemovy".
Lakini hapohapo kuna mambo mawili makubwa kuhusiana na vita hii ya Ukraine ambayo Zelenski anatumika.
Kwanza, ni makubaliano ya siri kati ya Marekani na NATO ambao viongozi wake wanakutana kuamua sera mbalimbali za dunia kwa siri huku wakificha ukweli halisi malengo ya walo nyuma yao ambao wana hisa katika rasilimali na uchumi wa dunia hii.
Pili, mzizi khasa wa vita hii ni lazima ueleweke baina yetu kwamba, huu ni mgawanyo wa dunia baina ya mataifa makubwa ambazo tangu mwaka 1991 USSR ilipoanguka wanataka kuizunguka Russia na kumuondoa raisi Putin na kuhodhi rasilimali za nchi hiyo bure kwa niaba ya hao watu ambao huitwa "finance capital".
Hawa watu wapo na ndo hupanga mipango ya dunia hii, ila safari hii wamekumbana na Vladmir Putin, jambo ambalo ni mtihani mkubwa kwa kujipa kazi ya kukabiliana na hawa jamaa.