Wakati wa Klabu ya Yanga kuuzwa rasmi kwa Manji umefika


Unafikiri kwa nini Congo DRC timu yao ya taifa ina mafanikio kuliko Taifa Stars ?
 
Tunachokitaka kutoka kwake ni kuona timu inafanya vyema kwenye michuano mbalimbali kama ilivyokuwa mwaka huu.

Biashara zake hazituhusu.

Chochote kitacho tokea ni cha ziada tu... au mbwembwe!
Yule ni binadami ipo siku atakufa, Yanga kama taasisi ina mikakati ipi ya kujitegemea? Mtu anayekujenga kwenye misingi ya kuwa tegemezi hakusaidii.
 
[emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Yule ni binadami ipo siku atakufa, Yanga kama taasisi ina mikakati ipi ya kujitegemea? Mtu anayekujenga kwenye misingi ya kuwa tegemezi hakusaidii.

Kabla ya Manji Yanga haikuwepo ?
 
Nani amewadanganya klabu kumilikiwa na mtu ndio inapata mafanikio ?
Kama Manji ndiye analipa hadi viongozi wengine mnaogopa nini kummilikisha timu ?
 
kuna kipindi Manji alitaka kuinunua Yanga kwa bilioni tatu miaka kumi ishapita mpaka sasa kama angefanikiwa angemiliki hisa asilimia sitini na kuwakopesha wanachama asilimia arobaini,sijui kilitokea nini baadae katika uongozi wake nilisikia wametoa mapendekezo yakuifanya Yanga kuwa kampuni mapendekezo hayo yatarudishwa kwa wananchi iliyaweze kupigiwa kura
Naunga mkono hizi timu mbili simba na yanga kuendeshwa na watu binafsi alafu sisi wanachama na mashabiki tununue hisa huu ndo utakuwa umiliki wa kweli wa timu tutakuwa na haki yakuhoji mwenendo wa timu sio kama saivi tumekuwa wanasiasa kelele tuu,timu hatujui inaendeshwa vipi,wachezaji wanalipwa vipi,mauzo ya jezi n.k
 
Tumpe timu .
 

Itabidi MANJI azungumze na waliochangia Tofali na kubeba mchanga ili awarudishie pesa zao au hata awaachie jengo yeye achukue timu kisha timu ipange hapo jangwani. Au mnasemaje wana wa Jangwani?????? Sio kila siku tunasikia mimi Yanga damu, wakati hata mlo mmoja kwa siku ni shida. tehe teheteheeee he kho!
 
Pointi tupu mkuu! Umeongea kisomi sana!
 
Unataka watu wamalizane kwa kulogana kugombea hela ya pango ? Uliza jengo la mtaa wa mafia nani anachukua kodi !
 
Azam ina mafanikio gani mkuu?
 
Azam ina mafanikio gani mkuu?

sidhani kama timu ya Azam ina miaka 10 tangu imeanzishwa lakini tayari imejengeka vizuri kimiundombinu, kiuchumi, etc.

pia kwenye dimba uwanjani imeshanyakua mataji makubwa mawili (TZ & Cecafa) na imekuwa ikishika nafasi 2 za juu kwa miaka takribani 5 mfululizo kwenye ligi yetu. pia fanbase yake imeongezeka kwa kiasi kikubwa sana.

kwa zama hizi za ushindani, na ukizingatia Azam haikuwahi kuwa brand maarufu sana, haya si mafanikio madogo hata kidogo.

sasa tumia template hiyo kwa brands kubwa Simba au Yanga - boom!!!
 
Na ukitaka uone maajabu huyo manji aanze za habari kutaka kuinunua club,wataanza maneno utafikiri wao ndo wanamlipa kamusoko mshahara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…