Wakati wa Klabu ya Yanga kuuzwa rasmi kwa Manji umefika

Wakati wa Klabu ya Yanga kuuzwa rasmi kwa Manji umefika

Kama klabu haiwezi kugharamia gharama za klabu then akaja mtu mwenye pesa zake bila shaka itafanikiwa.....

TP mazembe & AS vita.! Zingatia hizi klabu.

Simaanishi Mafanikio ya Yanga SC yameletwa na Manji. La hasha, bali uwepo wake umeongeza ubora zaidi kwa klabu.

Unafikiri kwa nini Congo DRC timu yao ya taifa ina mafanikio kuliko Taifa Stars ?
 
Tunachokitaka kutoka kwake ni kuona timu inafanya vyema kwenye michuano mbalimbali kama ilivyokuwa mwaka huu.

Biashara zake hazituhusu.

Chochote kitacho tokea ni cha ziada tu... au mbwembwe!
Yule ni binadami ipo siku atakufa, Yanga kama taasisi ina mikakati ipi ya kujitegemea? Mtu anayekujenga kwenye misingi ya kuwa tegemezi hakusaidii.
 
Kuna vimtu duni visivyo hata na kumi mfukoni huwa vinadumaza sana hizi klabu zetu. Umefikia wakati vijana kureplace wazee kwenye hizi klabu ndio tutaona tija. Haiwezekani klabu iwe na mwenyekiti anatinga mkutanoni na makubazi hata kusoma hajui anaongea mate yanamtoka mdomoni staha hana kazi ushirikina.

Azam ile pale, hamna majungu makubwa sababu hamna njaa. Simba imefeli sababu ya njaa. Tusibishe kwenye hili, ni Manji ndio kaileta hii Yanga ya kimataifa
[emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Yule ni binadami ipo siku atakufa, Yanga kama taasisi ina mikakati ipi ya kujitegemea? Mtu anayekujenga kwenye misingi ya kuwa tegemezi hakusaidii.

Kabla ya Manji Yanga haikuwepo ?
 
kuna kipindi Manji alitaka kuinunua Yanga kwa bilioni tatu miaka kumi ishapita mpaka sasa kama angefanikiwa angemiliki hisa asilimia sitini na kuwakopesha wanachama asilimia arobaini,sijui kilitokea nini baadae katika uongozi wake nilisikia wametoa mapendekezo yakuifanya Yanga kuwa kampuni mapendekezo hayo yatarudishwa kwa wananchi iliyaweze kupigiwa kura
Naunga mkono hizi timu mbili simba na yanga kuendeshwa na watu binafsi alafu sisi wanachama na mashabiki tununue hisa huu ndo utakuwa umiliki wa kweli wa timu tutakuwa na haki yakuhoji mwenendo wa timu sio kama saivi tumekuwa wanasiasa kelele tuu,timu hatujui inaendeshwa vipi,wachezaji wanalipwa vipi,mauzo ya jezi n.k
 
Kama klabu haiwezi kugharamia gharama za klabu then akaja mtu mwenye pesa zake bila shaka itafanikiwa.....

TP mazembe & AS vita.! Zingatia hizi klabu.

Simaanishi Mafanikio ya Yanga SC yameletwa na Manji. La hasha, bali uwepo wake umeongeza ubora zaidi kwa klabu.
Tumpe timu .
 
......... mifano ni mingi sana ! Hapo jirani DRC , PDG Katumbi hakuna asiyeujua mchango wake kwenye harakati za TP MAZEMBE kutawala soka la Africa .

Shime wana Yanga wakati ni huu , yale mambo ya kudai " nilichangia tofali au sijui nilibeba mchanga " yamepitwa na wakati .

Itabidi MANJI azungumze na waliochangia Tofali na kubeba mchanga ili awarudishie pesa zao au hata awaachie jengo yeye achukue timu kisha timu ipange hapo jangwani. Au mnasemaje wana wa Jangwani?????? Sio kila siku tunasikia mimi Yanga damu, wakati hata mlo mmoja kwa siku ni shida. tehe teheteheeee he kho!
 
kuna kipindi Manji alitaka kuinunua Yanga kwa bilioni tatu miaka kumi ishapita mpaka sasa kama angefanikiwa angemiliki hisa asilimia sitini na kuwakopesha wanachama asilimia arobaini,sijui kilitokea nini baadae katika uongozi wake nilisikia wametoa mapendekezo yakuifanya Yanga kuwa kampuni mapendekezo hayo yatarudishwa kwa wananchi iliyaweze kupigiwa kura
Naunga mkono hizi timu mbili simba na yanga kuendeshwa na watu binafsi alafu sisi wanachama na mashabiki tununue hisa huu ndo utakuwa umiliki wa kweli wa timu tutakuwa na haki yakuhoji mwenendo wa timu sio kama saivi tumekuwa wanasiasa kelele tuu,timu hatujui inaendeshwa vipi,wachezaji wanalipwa vipi,mauzo ya jezi n.k
Pointi tupu mkuu! Umeongea kisomi sana!
 
Itabidi MANJI azungumze na waliochangia Tofali na kubeba mchanga ili awarudishie pesa zao au hata awaachie jengo yeye achukue timu kisha timu ipange hapo jangwani. Au mnasemaje wana wa Jangwani?????? Sio kila siku tunasikia mimi Yanga damu, wakati hata mlo mmoja kwa siku ni shida. tehe teheteheeee he kho!
Unataka watu wamalizane kwa kulogana kugombea hela ya pango ? Uliza jengo la mtaa wa mafia nani anachukua kodi !
 
imefika wakati hizi timu mbili (Simba na Yanga) zisonge mbele kiuchumi ili soka la nchi yetu liende hatua moja zaidi mbele. njia pekee ni kuondoa Uswahili kwenye hizi klabu na kuzi-commercialise. wafanya biashara walio interested wapewe nafasi ya ku-bid for the majority shareholding. Waswahili wa-retain some shares for loyalty.

kibiashara these are very attractive brands. nionavyo mimi ziko much stronger than Manji, Mo & Bakhresa all rolled into one.

so, Yanga wanaweza kuanza na the Manji's of this world. Simba kuna Mo ambaye tayari ameonyesha interest kubwa.

Chelsea, Liverpool, ManCity, Man U, Arsenal, TP Mazembe au hata Azam - oneni zinavyoendeshwa kwa mafaninikio na kuwafurahisha wapenzi wao.

wito kwa ninyi wanachama wa hizi timu 2: chukueni hii ajenda (seriously) muende nayo kwenye mkutano mkuu. ama sivyo kutoka hapo mlipo ni ndoto ya alinacha!
Azam ina mafanikio gani mkuu?
 
unnamed%2B%252868%2529.jpg

Manara akishangilia goli la pili la Yanga dhidi ya Simba.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Always huwa unaitendea haki ID yako.
 
Azam ina mafanikio gani mkuu?

sidhani kama timu ya Azam ina miaka 10 tangu imeanzishwa lakini tayari imejengeka vizuri kimiundombinu, kiuchumi, etc.

pia kwenye dimba uwanjani imeshanyakua mataji makubwa mawili (TZ & Cecafa) na imekuwa ikishika nafasi 2 za juu kwa miaka takribani 5 mfululizo kwenye ligi yetu. pia fanbase yake imeongezeka kwa kiasi kikubwa sana.

kwa zama hizi za ushindani, na ukizingatia Azam haikuwahi kuwa brand maarufu sana, haya si mafanikio madogo hata kidogo.

sasa tumia template hiyo kwa brands kubwa Simba au Yanga - boom!!!
 
Na ukitaka uone maajabu huyo manji aanze za habari kutaka kuinunua club,wataanza maneno utafikiri wao ndo wanamlipa kamusoko mshahara
 
Back
Top Bottom