Wakati wa Klabu ya Yanga kuuzwa rasmi kwa Manji umefika

Uko vizuri...lete kwa lugha moja...wengine tumetoka Kaliua.
 
Very true , Mo alichemsha vibaya sana , ila Kajumulo alikuwa anaibiwa tu na watoto wa mjini .
 
Mimi nauliza tu, mbona biashara za Manji zinakuwa na kupanuka lakini Yanga haina biashara licha ya asset ilizonazo?

Manji ni walewale tu yupo Yanga kutimiza ajenda zake, kwahiyo akifa Manji na Yanga kwishney?
Wewe Nyumbu Yanga haiwezi kufa hata siku moja
 
Hahahaaaa!
Hili suala la fanbase huwa kila siku najiuliza hivi hizi timu kama elimu inatolewa kwa wapenzi na mashabiki wakawaelewa viongozi kuwa kwa wiki unatoa mia tano unanunua gazeti la yanga imara au ngurumo za simba kwa uchache wauze nakala laki mbili kwa wiki ingekuwa bonge la kitega uchumi wapenzi wanaambiwa sio tu unapata khabari za timu pia unakuwa umechangia klabu .
Leo watu wapo radhi kuvaa jezi za nje tena original sio kafa ulaya kwanini morali huo usibadilishwe na kuwa wa yanga na simba?dhamira na uthubutu walio kuwa nao kina mzee tabu mangala upo wapi?enzi za youth timu kama black stars ilio toa kina pondamali ipo wapi?
 
Katibu wa klabu na msemaji wa klabu wanaweza kufanya kampeni ya kuongeza idadi ya wanachama hai nchi nzima,hata kufanya hivi ni lazima tuwape timu hao wahindi ?
Ni aibu Simba/Yanga wanachama hai hawafiki hata 20,000
 
Yanga ina hazina kubwa sana ya mashabiki ikiamua kutilia mkazo kuikuza brand watapata mpunga wa maana.

Juzi nilikuwa uwanjani nikamuona Meneja Masoko wa Yanga nikajiuliza huyu mtu kazi yake ni nini pale Jangwani?
 
So far ni club ya wanachama. Kwanza igeuzwe iwe kampuni ili wanahisa wajulikane. Baada ya hapo auziwe kwenye ushindani na watu wengine.
 
Yanga ina hazina kubwa sana ya mashabiki ikiamua kutilia mkazo kuikuza brand watapata mpunga wa maana.

Juzi nilikuwa uwanjani nikamuona Meneja Masoko wa Yanga nikajiuliza huyu mtu kazi yake ni nini pale Jangwani?
Kuna vyeo vimewekwa kulindana tu Msemaji wa klabu,Katibu wa klabu,Meneja Masoko hakuna cha maana wanachofanya,nakumbuka hata TFF waliwahi kumuajiri Jimmy Kabwe hicho cheo hakuna alichofanya
 
Kuna vyeo vimewekwa kulindana tu Msemaji wa klabu,Katibu wa klabu,Meneja Masoko hakuna cha maana wanachofanya,nakumbuka hata TFF waliwahi kumuajiri Jimmy Kabwe hicho cheo hakuna alichofanya
Tuna safari ndefu sana hadi kufikia kuona mafanikio ya Vilabu vyetu na Taifa kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…