Wakati wa Lowassa ''walishitakiwa'' ICJ; Wakati wa Lissu ''wameshitakiwa'' ICC

Wakati wa Lowassa ''walishitakiwa'' ICJ; Wakati wa Lissu ''wameshitakiwa'' ICC

Mkuu;
Kwani nikijipa moyo wewe unaumia?

Nadhani umesoma tu heading na kutoa maoni kama mlivyo ''makamanda''!

Kwanza naunga mkono hoja yako namba 1 kwamba sisi waafrika husasani Watanzania ni wajinga, na tunamaliza oxygen bure kwenye hii dunia. Mwaka 2013-2015 tulikuwa tunaimbishwa kama wendawazimu kuwa uchumi wa gas ndio mkombozi wa nchi, na kuwa bomba la gas likifika Dar tatizo la umeme litakuwa historia na bei itashuka na mabomba ya gas yatasambazwa majumbani!

Leo hii bomba la gas limefika Dar, umeme haujashuka bei, wala haujasambazwa majumbani, bali hadithi imebadilika kuwa sasa ni umeme wa maji kwani gas sio yetu maana tumepigwa! Wanaosema haya ndio hao hao waliokuwa wanatuimbisha uchumi wa gas kama mazuzu, huku mishipa ya shingo ikawatoka kuwa umeme wa maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Ukitaka kujua kweli sisi ni vituko vya karne, wanaosema umeme wa maji utakuwa bei chini, hawatumbii kwanini umeme unaozalishwa mpaka sasa kwa vyanzo vya maji, kwanini haukuwa bei rahisi! Na watu wanashangilia vibaya sana.

Sasa ngoja aje rais mwingine na yeye ataachana na umeme wa gas na maji, atasema umeme wa makaa ya mawe ndio sahihi maana tuna akiba ya kutosha, atasema kwenye gas tumepigwa, na wa maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi! Watatokea tena wapambe kama nyie mlioko sasa, mkimsifia rais huyo kwa kubeba maono ya watanzania kwani ni msikivu na anashaurika! Hii ndio specie iliyopo Tanzania.
 
Narudia tena, msiishi kwa mazoea mkajidanganya mmarekani anawaogopa, nyie ni vipofu wa fikra.
Mmarekani asiwaogope Libya na Iraq na nchi zingine yaani atuogope sisi kwa lipi.
Ss bado nitegemezi na hatuna chochote cha maana au Tanzanaite tuliyonayo ambayo nayo wanaweza kuiwekea vikwazo vilevile.
 
Yaani hawa jamaa wanafurahisha sana!

Baada ya muda hizi kelele hatutazisikia tena mpaka baada ya uchaguzi mkuu 2025

Kwani kuna habari ya kudumu, umeona watu wanaendelea kumuongelea Kikwete, au kombe la Dunia lililopita? Kila jambo hujadiliwa kwa muda wake, na kutoachwa kujadiliwa sio kupuuzwa au kuridhika, bali hiyo ndio nature ya binadamu.
 
Mkuu ningependa nikujibu kwa undani hoja zako lakini naogopa nikifanya hivyo nitakuwa nimetoka nje ya mada yangu!

Hoja zako zimejaa nadharia kuliko uhalisia!
 
Jipe moyo tu, endelea kuishi kwa mazoea.

Mmefanya mambo ya ajabu kwenye uchaguzi mkashinda kwa namna ya aibu, mkapewa maelekezo mrekebishe mambo mmegoma, sasa Mmarekani ameshaonesha dalili anaanza, wewe endelea kuota na habari zako za Lowassa.
Tulizana sindao ikuingie,
Kama una data yoyote weka hapa pia ulete data ya kuonyesha nchi gani ilishitakiwa kwa ujinga wa waharifu kumi hao kwa hiyo mahakama ya ICC ikaendesha kesi?
 
Mkuu;
Ningependa nikujibu kwa undani hoja zako lakini naogopa nikifanya hivyo nitakuwa nimetoka nje ya mada yangu!

Hoja zako zimejaa nadharia kuliko uhalisia!

Najua fika, ukijibu kama nilivyosema utakuwa umehama mada yako ya msingi, nilitaka tu kuweka rekodi sawa kwenye mada yako namba moja, maana ulinganifu ni huo huo.
 
Narudia tena, msiishi kwa mazoea mkajidanganya mmarekani anawaogopa, nyie ni vipofu wa fikra.


Narudia tena, msiishi kwa mazoea mkajidanganya mmarekani anawaogopa, nyie ni vipofu wa fikra.

Mkuu hivi unafahamu kinachoendelea sasa Marekani?
 
Unataka nichukue masaa mangapi kusoma unavyojiliwaza kama mtoto mdogo?!

Ukishajua fulani hatofautiani na jiwe, huna sababu ya kumsoma, siku zote anawaza vile vile.
Aiseee hili tatizo ni kubwa namna hii kumbe!?

Kuna jamaa ( mwalimu) alisimulia juzi kati akasema vijana wa siku hizi wengi wao hawana uwezo wa kutafakari na kutafuta suluhu ya changamoto!

Nikamuuliza una ushahidi gani na hilo, akasema vijana zaidi ya robo tatu ya darasa lenye idadi ya wanafunzi karibu mia mbili wa semesiter ya saba, aliwafundisha na akatoa mfano wa swali la kimahesabu darasani yeye na wao wakaurudia kulikokotoa darasani !

Kwenye mtihani akarudisha mfano ule ule lakini akabadili takwimu moja na kuipa alama "b". Hivyo alitegemea kwa kuwa wanafunzi ni wanamahesabu, basi jibu la swali litakuwa 'in terms of b'!

Ajabu anasema ni robo ya darasa walipata swali hilo.

Ndugu msomaji wa post hii ni wajibu wako sasa kuamua denooJ awekwe kundi la robo tatu ama kundi la robo kwa post yake hii niliyonukuu.
 
Ungemalizia sentesi yako kwa kuandika, ''bali hiyo ni nature ya binadamu WASIOJITAMBUA au WANAOPOTEZA MUDA''

Kuna wakati tulikuwa tunajadili sana ripoti ya makinikia hapa jukwaani na nchini, ripoti ile ikafanyiwa kazi hadi na TRA ikakuta tunawadai Barrick $192b! Mbona kila siku huanzishi uzi kujadili ule uhuni ili tuone kipimo chako cha uelewa?
 
maelezo mengi kiasi hicho yana tija gani zaidi ya uwoga, usimfananishe lissu na yule babu..
Ni wapi nimemfananisha!

Tatizo lako la kusoma heading pekee na kutoa maoni halina tofauti na wanaojiita "makamanda"
 
Tulizana sindao ikuingie,
Kama una data yoyote weka hapa pia ulete data ya kuonyesha nchi gani ilishitakiwa kwa ujinga wa waharifu kumi hao kwa hiyo mahakama ya ICC ikaendesha kesi?
Hana data zozote bali ana makelele ya kijinga!
 
Kuna wakati tulikuwa tunajadili sana ripoti ya makinikia hapa jukwaani na nchini, ripoti ile ikafanyiwa kazi hadi na TRA ikakuta tunawadai Barrick $192b! Mbona kila siku huanzishi uzi kujadili ule uhuni ili tuone kipimo chako cha uelewa?
Mkuu;
Bado unajaribu kunitoa nje ya mada yangu!
 
Mkuu;
Bado unajaribu kunitoa nje ya mada yangu!

Sijaribu wala sitaki kukutoa kwenye mada yako, na iwapo utatoka huo utakuwa ni udhaifu wako na sio wangu. Ninachotaka kukuonyesha unachosema kwa upande mwingine, kwa maneno marahisi naifanya mada yako kuonekana kama mbuni aliyefunika kichwa kwenye mchanga, huku mwili mzima uko wazi. Na kwa taarifa yako, ninafahamu vizuri nifanyacho kwenye mada yako uliyodhani ina nguvu hiyo.
 
Back
Top Bottom