Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 72,020
- 129,293
Huwa ninacheka kwa nguvu nikisikia mali zetu zitaporwa. Raslimali zetu zote kama kuna wageni wanachukua, wote wameingia mikataba na viongozi wetu, tena wote ni wa ccm. Sasa huwa najiuliza ni lini hao wazungu waliwahi kuja na kuvuka mpaka kibabe kuja kuchukua hizo raslimali? Halafu hii propaganda mfu huwa ninasikia mpaka wasomi wanasema eti raslimali za nchi yetu zitaporwa! Ndio maana huwa sionagi tofauti ya wasomi na wasiosoma ndani ya nchi hii.
Huyu mwenye huu uzi ameuleta ili kuonyesha kwamba kuna kundi fulani ni la watu wajinga, lakini kuna mahali nimemjibu tena kwa mifano, ili kumuonyesha hilo tatizo la ujinga ni kubwa kuliko alivyojaribu kuonyesha kwenye post yake namba moja. Halafu ni bora wangeishia kwenye ujinga tu, lakini mbali ya ujinga wakachanganya na unafiki juu. Magufuli amesaidia kuanika ujinga na unafiki wa watanzania wengi.