Wakati wa Utawala wa Ali Hassan Mwinyi, ameshawahi kutekwa au kuuwawa mtu?

Wakati wa Utawala wa Ali Hassan Mwinyi, ameshawahi kutekwa au kuuwawa mtu?

Mara hii mshabadili gia. Maana mwanzoni mlikua na wimbo wa wanaoingia masjid ni watu wa haki hawauwi ovyo wala kuteka leo mshaanza kutaja majina na kujitenganisha kiutawala aiseee
 
Huwa bado nawaza sana balozi Simoni Sirro enzi akiwa IGP aliwahi kusema kuwa Polisi wana ushahidi kamili kuhusu mashitaka dhidi ya Freeman Mbowe katika kesi yake ya 'ugaidi' iliyokuwa inahusisha pia utekaji na mipango ya mauaji kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa na tuliona kina Kingai wakienfa mahakamani kutoa matokeo ya upelelezi wao, ambapo mahakama ilimkuta Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu; mara ghafla bin vuu tukaona DPP amesita kuendelea na kesi, Mbowe akatoka jela yeye na washtakiwa wenzake, siku hiyo hiyo akaenda Ikulu kuonana na Samia, mara ghafla tukaambiwa maridhiano, Kisha IGP Sirro anatolewa U-IGP na kuteuliwa kuwa balozi Zimbabwe;....
 
Jamani sina mengi sana nimemkumbuka Rais wangu Ally Hassan Mwinyi, Mungu amjalie pepo ya filidausi, kweli sisi sote ni mashahidi wake na amani iwe juu yake mpaka siku ya kufufuliwa kwake
Kuna mwandishi wa habari anaitwa Stan Katabalo....nadhani aliibua ile kashfa ya Loliondo...sina uhakika sana ni wakati wa mwinyi au mwanzoni mwa mkapa.
 
Jamani sina mengi sana nimemkumbuka Rais wangu Ally Hassan Mwinyi, Mungu amjalie pepo ya filidausi, kweli sisi sote ni mashahidi wake na amani iwe juu yake mpaka siku ya kufufuliwa kwake
Kuna muandishi wa habari Stan Katabaro, na mkemia wa kupima vyakula kama vinafaa au havifai Kwa matumizi ya Binadamu
 
Mimi naamini yule Mzee wa watu hakuwahi kuwa na tone la damu mikononi mwake, hata kwa kuongea tu hakuwa kumfokea mtu au kujimwambafai, kweli alikuwa na hofu ya Mungu
 
Mimi naamini yule Mzee wa watu hakuwahi kuwa na tone la damu mikononi mwake, hata kwa kuongea tu hakuwa kumfokea mtu au kujimwambafai, kweli alikuwa na hofu ya Mungu
Vipi issue za nguruwe za magomeni? Au ulikuwa mtoto mdogo?
 
Mimi naamini yule Mzee wa watu hakuwahi kuwa na tone la damu mikononi mwake, hata kwa kuongea tu hakuwa kumfokea mtu au kujimwambafai, kweli alikuwa na hofu ya Mungu
Una point ila uovu wa mtu haupimwi machoni wala kile anaongea. Hata mchawi huwa anakaa siti za mbele kanisani na mstari wa mbele msikitini

Duniani kuna watu huwa very humble kwa nje, Ila kwa ndani ni mafia
Na Kuna wale wao kwa nje ni evils na kwa ndani ni evils
 
Back
Top Bottom