Wakati wangu wa kuomba maombi ya nguvu za kutawala, kumiliki, kinga, na kushinda vita zote

Wakati wangu wa kuomba maombi ya nguvu za kutawala, kumiliki, kinga, na kushinda vita zote

Maombi bila kazi, ni uchawi, hutapata kitu zaidi ya msongo tu,
Mchina hafanyi maombi, mchina anatumia vitu ambavyo tayari"Mungu"ameishawapa wanadamu,
Kwenye tekinilojia ya magari ya, umeme, Mchina kwenye soko anamiriki asilimia 60!, kijeshi, tekinilojia, anawatisha USA, na, umoja, wa, ulaya, China hakuna "tumsifu yesu kristo,wala bwana asifiwe,china wanatenda kama mfsno wa, Mungu!!
Kama huko Dar angalia utitiri wa makanisa na wachungaji, kila Kona wanahubiri kututatulia matatizo(tena ya kiuchumi)!
Vitendo ndio huleta tija,sio kuomba tu, cha ajabu unakuta jumapili wanawake kibao wapo kwa mwamposa ni kusali tu, kunywa maji,kupaka mafuta,kulamba chumvi!
Jtatu wapo kwa mchina wanatsfuta riziki, mchina mwenyewe,mwenye kiwanda, hamtaji Yesu! Ila anamuomba Mungu! Kwa vitendo, maana tayari kila kitu kipo!
Ukiona mtu anaomba kitu akitokei jua huyo hisia zake zipo kinyume na anachokitaka ndio maana hachukui hatua , bila ata kuomba ukiwa na hisia chanya huwa unafanikiwa kwa unachokitaka.
 
Kuna siri ya ushindi ukifanya maombi ya vita muda huu. Naingia vitani (maombi ya vita) kisha nakuja kutoa darasa kidogo. Nimerudi sasa.

Ulimwengu huu unatawaliwa na siri nyingi, na siri hizi ziko kwenye mfumo wa namba.

Namba 3,6,9 zina nguvu sana ya kufanya uumbaji wa jambo kimwili na kiroho.

9 ndio namba kubwa zaidi hivyo ina nguvu nyingi zaidi.

Huwa natumia lisaa lizima, yaani 9.00 usiku hadi 9.59 kuamuru siku yangu, kuwaangusha adui zangu, kuinua biashara zangu, kuboresha afya yangu, mahusiano yangu na pia kuwaumba wanangu wawe kama vile nitakavyo mimi.

Nalitumia jina la Yesu, maana kasema ombeni lolote kwa jina langu, huku nikujumlisha na siri nyingine za kanuni za kiroho za uumbaji ambazo hawafundishwi kanisani.

Maombi haya yana matokeo sana, na muda huu huwa na utulivu, hivyo nafanya chanting. Natoa sauti.

Hata mchawi akiwa anafanya uharibifu wake, anaongea manuizi yake kwa kutoa sauti, hafanyi kimoyomoyo.

Sio lazima ukubaliane na mbìu zangu na wala mbinu zangu sio sheria. Kuna kanuni nyingi za kiroho za kukuvusha.

JITAFUTE
Saaafi
Ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom