Tetesi: Wakati wowote mbunge wa Mtwara Mjini (CUF) atazungumza na waandishi wa habari

Tetesi: Wakati wowote mbunge wa Mtwara Mjini (CUF) atazungumza na waandishi wa habari

Status
Not open for further replies.
Waje tuu tutawapokea, usajir unakaribia kuisha maana usajiri wa mwisho ni wa bwana Mbowe a.k.a Mugabe wa TZ
 
Ukiangalia yanayotokea katika siasa za Tanzania utadhani yanayofanyika ni comedy. Hii nchi inaweza kuwa ni yakwanza Duniani kwa haya yanayotokea

Tulimumu ,
Mkuu,
Hilo jambo limetokea nchi nyingi kwa mfano, USA miaka ya 1800s, Kenya miaka ya 1990s to early 2000s.

Lakini sasa, matokeo yake yalikuwa siyo mazuri (matokeo yake yalikuwa hasi kwa wananchi ila kwa wanasiasa ikawa ni daraja lao kupata nafasi za uongozi na nyadhifa zingine) .
Kwa sababu, wananchi walifanywa kafara maana, mtifuano ulianza ndani ya vyama kisha ukarushwa kwa wananchi.

Sasa, wananchi nao kwa sababu ya umbumbumbu na kushabikia mambo bila kutathimini mambo hasa madhara ya ushabiki huo wakajikuta kwenye vita za wenyewe kwa wenyewe.

Guess, you know what!? The same Politicians who brought such a tragedy to their countries in one voice and together they decided to settle out their differences and continued with politics while, normal citizens were already in poverty, wounded, disunited and deaths.

Kwa hiyo, hizo hamahama zinahitaji wananchi wenye ufahamu mkubwa juu ya wanasiasa uchwara hasa tamaa zao za madaraka pasi kuangalia how they cling into positions.

Kwa sababu, wao wanatumia wananchi kama migongo na ngazi ya kufikia matakwa yao.

Any way, as a nation and one strong poeple we need to open widely our brains and not our mouths to see clearly this junk kind of politics in its immaturity stage.
 
Taarifa za kuaminika kutoka kwa Mbunge wa Mtwara mjini Mhe Maftah Nachuma kupitia CUF zinabainisha kuwa Mbunge huyo anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari ili kutangaza maamuzi magumu ya kisiasa.

Nachuma ambaye ni CUF Lipumba anatarajiwa kujivua uanachama wa CUF na kujiunga na CCM kwa lengo la kugombea tena nafasi ya Ubunge wa Mtwara Mjini kwa iketi ya CCM.

Taarifa zaidi zinadai kuwa mipango yote ya kumteua Nachuma kuwa mgombea kupitia CCM imekamilika, na amehakikishiwa support kubwa na uongozi wa CCM Taifa.

Stay Tuned, Humphrey Polepole aliposema kuna wapinzani zaidi ya 200 wanataka kuhamia CCM hakuwa anatania.

Pichani Mbunge huyo akiwa na Rais Magufuli

View attachment 643078
Akigombea tena CCM ataishia kwenye Kura Za maoni
 
Akigombea tena CCM ataishia kwenye Kura Za maoni
Kabisa! Mimi mwaka 2010 nilipogombea ubunge hiyo ilikuwapo. Kwamba mtu aliyetoka ccm akaenda upinzani kisha ajarudi kata jina hata kama atashinda kura za maoni. Nsijua hiyo siri...
 
Ifikie mahali wananchi tupewe meno ya kuwaburuza mahakamani watu ambao wanaliingiza Taifa kwenye upotevu wa fedha bila uchungu wakati wapo watoto wanakosa huduma muhimu kwa ukosefu wa fedha hambozo zinapelekwa kwenye marudio ya uchaguzi!
 
upinzani upo njiapanda
Ni kweli, CCM wameshawagonga Cuf, Chadema wakifanikiwa kukwepa dhoruba hii basi wataibuka wakiwa wapya na wenye nguvu zaidi.

Any way, upinzani ukidhoofika nchi itakuwa na hali mbaya sana. Hizi hujuma wanazofanya CCM dhidi ya Chadema sio za kufurahia kabisa kwa watu wenye akili timamu.

Vv
 
Chadema kufa sio leo wala kesho chadema ni taasisi nyuma yake tuko wengi ZAIDI ya asilimia 70% ya wa Tanzania.

Sajilini mkimaliza mseme.
..hivi ukiwa nyuma ya keyboard ya computer yako zile nobs za keyboard nazo huwa unaziona kuwa ni wananchama wenzako? Pole wajameni.
 
Hizi siasa si zakushabikia hata kidogo taifa linakula hasara kubwa, ni nani aliwaambia kuwa mbuge wa upinzanani huwezi kufanya kazi na raisi mpaka uwe ndani ya chama chake na pia kufanya kazi na mtu si lazima kumuung mkono lakini pia kwa kumkosoa , huu ni uchizi mkubwa elimu yetu mbovu na haya ni matunda yake.............
 
Kuishi bongo ni kwasababu hatuna pa kwenda

Nilisikia kama Kenyatta kafungua milango kule kwao. Japo ardhi yote yenye rutba inamilikiwa na familia yake (Starehe ya dingi kuwa mpigania Uhuru, Nyerere sijui alikuwa na akili gani kuacha familia yake bila kitu😎)

Hivyo pakwenda papo, usijilazimishe kuishi bongo ndugu.
 
Ifikie mahali wananchi tupewe meno ya kuwaburuza mahakamani watu ambao wanaliingiza Taifa kwenye upotevu wa fedha bila uchungu wakati wapo watoto wanakosa huduma muhimu kwa ukosefu wa fedha hambozo zinapelekwa kwenye marudio ya uchaguzi!

“Tupewe”? Na maCCM? I’m sorry chief, ila fikra kama za kwako hazina tija kwa sasa. Sasa inabidi wananchi tufikirie kulazimisha, na siyo kupewa ama kuomba. Tunaweza kujifunza kwa kujisomea civil movements za Burkina Faso, Sierra Leone na Ivory Coast, jinsi zilivyoangusha tawala za kiimla kama hii ya Magufuli.

Tuache kufikiria vyama vya upinzani kama ndivyo vinaweza kutusaidia! They will never, kwani ni rahisi sana kwa chama-dola CCM ku-deal na wapinzani. Ila siyo rahisi ku-deal na wananchi mmoja mmoja tukiwa mamilioni!
 
Chadema kufa sio leo wala kesho chadema ni taasisi nyuma yake tuko wengi ZAIDI ya asilimia 70% ya wa Tanzania.

Sajilini mkimaliza mseme.
ukifuatilia mienendo ya vyama vya upinzani utagundua kuwa kila chama cha upinzani kikifika kwenye peak hushuka kwa kasi ya ajabu mfano
Nccr
cuf
TLP
CDM japo inangangania kuto kufa lakini sioni jinsi kitavyo pona ukituo hiyo ruzuku ya 300 inayoliwa na wachache kwa sasa hivyo ambapo 2020 haitakuwepo na na ndicho kitakachohitimisha kifo cha CDM maana hawa watu wakipata hata wabunge 5 mwaka huo washukuru sana mungu
 
Hahahaha [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hii kweli fashion imeshika kasi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom