Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Well said!
 
Unaona jinsi mnavyosoma Biblia kama hadithi! Hivi hujawahi kuona msitari ambao Yesu anaagiza chochote tutakachomwomba baba yake kupitia yeye tutakipata? Kazi kweli kweli!
Sawa ila pia wengi hawajui majira ya Muumba kutokana na mapokeo ya dini na dhehebu mbalimbali,maana mistari kweny kitabu imeandikwa ili itimie na majira ya Yesu ilishaisha tupo majira ya Muumba mwenyewe kwa mujibu wa

1Korintho 15:24-28
24
Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.

26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.

28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe (Yesu) naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

Zekaria 14:9
Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.

Maana hata Yesu alipotufundisha sala ya Baba yetu,alisema tuombe ufalme wa Baba yake uje.

Mathayo 6:9
Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
 
Mwili tu ndiyo unaokufa roho inashi kati ya sehemu hizi mbili (1) peponi (11) kuzimu kote zinangoja siku ile ya hukumu.Hivyo wanapomwomba Maria,hawamwombi MTU Bali ile roho iliyopeponi kwa kuwa yeye alibarikiwa tayari na Mungu mwenyewe.Je wewe na Mimi tukifa tutaenda idara gani?
 
1. Kuna kifungu chochote kwenye biblia kinacholazimisha kuongea na Yesu kupitia kwa roho ya bikra Maria badala ya kuongea na Yesu moja kwa moja?

2. Tupe kifungu kwenye biblia kinachoidhinisha roho za wafu kutumika kuwaombea walio hai.
 
Yupo hai kiroho,na katika sala tunahusisha roho kwahiyo kuwasiliana na roho mwanadamu (mwili na roho) anayonafasi yakupitia kwenye roho iliyokaribu katika unyenyekevu.
Wapi pameandikwa kwamba mtu hafiki kwa Yesu pasipo kupitia kwa bikra Maria?
 
 

Attachments

  • 686EF917-88B5-4F56-870E-73B5E0BC1BF4.jpeg
    53.8 KB · Views: 1
Mbona biblia imeeleza vzr Tu au hamsomi
 
Kumbe ni Kwa akili zako fupi hapo sawa....ila haujui kuwa hakufariki alipalizwa mbinguni!?? ....we soma tu madrasa ndugu... Kama sio msabato basi wale wazee wa kobazi na baraghashea ndio mnaujua kuhangaika na Ukatoliki kuliko Imani zenu.
 
Kumbe ni Kwa akili zako fupi hapo sawa....ila haujui kuwa hakufariki alipalizwa mbinguni!?? ....we soma tu madrasa ndugu... Kama sio msabato basi wale wazee wa kobazi na baraghashea ndio mnaujua kuhangaika na Ukatoliki kuliko Imani zenu.
Mkuu sasa kwanini usitupe hiyo elimu tufaidike wote hapa badala ya kutuambia tu kwamba kuna maandiko badala ya kuyaweka hapa hayo maandiko?
 
Lete kifungu tusome mkuu
Yesu Kristo, kulingana na mafundisho ya Biblia, ni njia ya pekee ya kufikia Mungu Baba ,hakuna cha Maria wala mtakatifu yeyote. Katika Yohana 14:6, Yesu anasema:
"Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."
Hii inaonyesha kwamba Yesu ni mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu, akiunganisha uhusiano uliovunjika na dhambi.

Ni kweli kwamba Yesu mara nyingi aliwafundisha wafuasi wake kumwabudu na kumuomba Mungu Baba moja kwa moja. Kwa mfano:

Katika Mathayo 6:9, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake Sala ya Baba Yetu

"Basi, ninyi salini hivi, Baba yetu uliye mbinguni..."
Hii inaonyesha kwamba maombi yanaweza kuelekezwa kwa Baba moja kwa moja.

Katika Yohana 4:23, Yesu anaeleza kwamba waabuduo wa kweli watamwabudu Baba katika roho na kweli. Hii inaonyesha umuhimu wa uhusiano wa moja kwa moja kati ya muumini na Mungu Baba.

Yesu pia anafahamika kama Kuhani Mkuu wa agano jipya. Katika Waebrania 4:14-16, Yesu anatajwa kama Kuhani Mkuu ambaye anatuwezesha kupata neema mbele za Mungu. Hii inamaanisha kwamba ingawa waumini wanaweza kumuomba Baba moja kwa moja, Yesu ndiye anayefanikisha upatanisho huo.

Katika Yohana 10:30, Yesu anasema:
"Mimi na Baba tu umoja."
Maneno haya yanaonyesha kwamba kumuomba Yesu au Baba ni sawa kwa sababu wana uhusiano wa karibu kabisa. Kwa hivyo, wakati Wakristo wanapomuomba Mungu kupitia Yesu, hawampuuzilii Mungu Baba, bali wanaheshimu jukumu la Yesu kama mpatanishi.

Aya ni nyingi sana zipo
 
Kumbe ni Kwa akili zako fupi hapo sawa....ila haujui kuwa hakufariki alipalizwa mbinguni!?? ....we soma tu madrasa ndugu... Kama sio msabato basi wale wazee wa kobazi na baraghashea ndio mnaujua kuhangaika na Ukatoliki kuliko Imani zenu.
Hakuna hilo andiko si useme ukweli tu mnafata mapokeo ya WANADAMU,

Kuna Aya Huwa mnaitumia ya ufunuo 12:1

Ukweli haihusihani kabisa , fundisho la maria kupalizwa ni fundisho la kipagani na limepokelewa na kanisa katoliki juzi juzi tu hapa ,muwe mnasoma historia

Mnamo tarehe 1 Novemba 1950, Papa Pius XII alitangaza rasmi mafundisho ya kupalizwa kwa Mariamu kuwa fundisho rasmi la imani (dogma) kwa tamko la Munificentissimus Deus. Alisema:
“Baada ya maisha yake duniani, Mama wa Mungu, bila dhambi, alipalizwa mwili na roho kwenda utukufu wa mbinguni.”
 
Unalazimisha ku u-define ukatoliki kwa kutumia ulokole. Hau-ujui undani wa ukatoliki.

Pia sio kazi yetu sisi wakatoliki kukufundusha kitu ambacho hauko tayari kukipokea; ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
 
Sanaaaa..... Inakuhusu nini...... Wewe si una Imani yako Baki nayo ikuponye ...waache wakatoliki na Imani Yao wapotee shida yako nini.... Au unataka Mudi akubusu kama alivyombusu swahaba wake.
 
Sanaaaa..... Inakuhusu nini...... Wewe si una Imani yako Baki nayo ikuponye ...waache wakatoliki na Imani Yao wapotee shida yako nini.... Au unataka Mudi akubusu kama alivyombusu swahaba wake.
Kaka tunajuzana na biblia imeruhusu mijadala ,by the way mm ni mkristo sio muislamu

Ukatoliki ndio ulianzisha uislmau
 
Unalazimisha ku u-define ukatoliki kwa kutumia ulokole. Hau-ujui undani wa ukatoliki.

Pia sio kazi yetu sisi wakatoliki kukufundusha kitu ambacho hauko tayari kukipokea; ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Kama umeona huyo hafundishiki, tufundishe sisi mkuu; achana naye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…