Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Bila shaka hawa watakuwa wale wenzetu wavaa vibagharashia. Mimi leo siko huko mkuu. Yesu na Mungu ni roho mbili tofauti; sio kitu kimoja mkuu.
Kama unasema mungu ananguvu nyingi alafu awe na nafsi moja basi huyo mungu hana nguvu, kiumbe chenye nafsi moj6ni mwadamu mungu yeye sio mwadamu kama sisi na tunasema kuwa ananguvu nyingi kwanini jambo la nafsi tatu lishindikane mbele zake.
 
Yesu hana mama yeye alikuwako tangu kabla ya maria,
Maria na Yosefu ni wazazi walezi/walishi wa Yesu, walimlea tangu utoto wake, Hata Yesu mwenyewe anawathamini, wewe ni nani usiwape thamani yao? Mungu ndiye aliwapa heshima ya kutimiza Unabii wake kupitia wao.

Yohane 19:26-27
Basi alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, mwanao.
Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama mama yako. Tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.
 
Tuanze na wewe kwa kunionyesha kwamba hakupaishwa! Tupe kifungu kwamba hakupaishwa.
Kifungu kinachothibitisha kuwa bikra Maria alipaishwa sina mkuu. Kama wewe unacho, unaweza kukiweka hapa kwa faida ya wengi. Kama huna, tusubiri wenyewe waje mkuu.
 
Hakuna kifungu kinacho onesha kuwa alipaishwa na hakuna kifungu kinacho oneshwa kuwa hakupaishwa, je wewe unaamini alipaishwa kwa kifungu kipi?
 
Kifungu kinachothibitisha kuwa bikra Maria alipaishwa sina mkuu. Kama wewe unacho, unaweza kukiweka hapa kwa faida ya wengi. Kama huna, tusubiri wenyewe waje mkuu.
Kifungu unachopaswa kupewa mkuu ni cha kifungo cha miezi sita na viboko saba vya shingoni.
 
Mnanishangaza sana Waislamu wanamtambua Bikira Maria ila nyinyi protestants hamumtambui?Hizo dini mlinazo zote zilitoka Roma.Baada ya Luther na wengineo kuondoka ndio mkapata haya makanisa yote yaliyopo sasa.Mungu ni mmoja tunaheshimu ila pia msidhihaki vitu ambavyo hamvijui kuna mengi sana ambayo protestants hamyajui.Mimi ni shuhuda wa miujiza ya Bikira Maria na ninasema hapa wakristo tunamheshimu kwa sababu ni mama wa Mungu wetu na msaada wetu katika shida.Utakapokufa Yesu mwenyewe hawezi kumpokea mtu anayemdharau mama yake, kW maneno ya kumdhihaki.Mungu ajakuambia wewe udhihaki dini au imani za watu wengine kitu ambacho hukifahamu sio vyema kukiongelea
 
Point na suala ni moja tu; Baada ya hayo yote, Je, Maryamu/Maria anastahili/hastahili HESHIMA kwa kuwa sehemu ya utimilifu wa Unabii wa MUNGU?
 
Luka 1
29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?

30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?

35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

(Maria mnamtoa wapi ?)
 
Biblia imehaririwa sana tu
 
1. Nani hamthamini bikra Maria mkuu?
2. Tunaomba utupe vifungu vya huo ufunuo mkuu. Sote hapa tunajifunza. Kama haya masuala unayafahamu vizuri, itapendeza ukitushirikisha.
 
Mtake msitake hata mama yake na mtume halipi hapa kwa bikira mariamu ( maria).
 

Attachments

  • 5887319-0e638715bf809aa1b17ffd05ad57727.mp4
    1.2 MB
Hakuna jina la Maria kwenye Biblia.
Acheni kuwapotosha watu.

Mathayo (Mat) 1:18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Piganeni tu 🤣 🤣.
 
Huwa wanatafuta mstari mmoja ulio tata kwenye biblia ili waanzishie kanisa la kupata maokoto.Pure conmen!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…