Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Yesu hajawai piga picha
 
Yupo karibu na Mungu,anasaidia kumshawishi Mungu wetu
 

Bado hakuna sehemu inaonyesha watu walimtuma Mariamu.
 
Wakati unajibiwa ongeza na hili. Wale ma bikra 72 watatosha wanaume wote huko kwenye pepo ya mashariki ya kati? Au ni mwendo wa ku share hao 72 kwamba ni free ?
 
Hapa unawaambia nini ambao huamini kua Yesu ni Mungu? kwa mujibu wa andiko lako hapa ni kua Yesu na Mungu ni vitu viwili tofauti,

Ufafanuzi tafadhali.
YESU na Mungu ni tofauti ndio, ila Yesu ni Mungu

Soma hapa kwenye zaburi

Zaburi 45:6-7 (Agano la Kale)

Kiebrania cha Asili:

"Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, ni cha milele na milele; Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
Umeupenda haki, ukachukia ubaya; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta kwa mafuta ya furaha kuliko wenzako."



Aya hii inamtaja mfalme (katika muktadha wa zaburi hii) kama Mungu (kwa lugha ya heshima), lakini pia inasema Mungu ndiye aliyemtia mafuta, akionyesha mamlaka ya juu zaidi.

Waebrania 1:8-9 (Agano Jipya)

Aya hii inamnukuu Yesu kama mfano wa utimilifu wa unabii huo wa Zaburi 45:6-7:

"Lakini kuhusu Mwana asema:
‘Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, ni cha milele na milele,
Na fimbo ya haki ni fimbo ya ufalme wako.
Umependa haki na kuchukia maasi;
Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta ya furaha zaidi ya wenzako.’"
 
Yesu alipokuwa anazungumza na MUSA na ELIYA alikuwa anazungumza na marehemu?
Wazee mbona hamsomi maandiko , mtatapeliwa sana na kina mwamposa kwa mtindo huu ,

Musa na Eliya hawakuwa wafu, Eliya alipaa mbinguni anawakilisha ambao hawataonja mauti, Musa ALIKUFA ,baadae akaja kufufuliwa na malaika ,anawakilisha watakaokufa na kufufuliwa

Ushahidi wa maandiko

Biblia inaonyesha kwamba Eliya hakufa bali alichukuliwa mbinguni akiwa hai. Hili liko wazi katika:

2 Wafalme 2:11

"Ikawa walipokuwa wakienda, wakizungumza, tazama, gari la moto na farasi wa moto likawatenganisha; Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli."

Hii inaonyesha kwamba Eliya hakuonja mauti, bali alichukuliwa moja kwa moja na Mungu.

Musa Alikufa na Akafufuka - Maandiko Husika

Biblia inasema wazi kwamba Musa alikufa, lakini kuna ushahidi wa kihisia kwamba alifufuliwa, na hili linatokana na tafsiri ya baadhi ya maandiko:

Kifo cha Musa:

Kumbukumbu la Torati 34:5-6

"Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko katika nchi ya Moabu, kama Bwana alivyosema. Akamzika katika bonde, katika nchi ya Moabu, juu ya Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo."


Musa Akifufuka (Hili linafahamika kupitia Yuda 1:9):

Yuda 1:9

"Lakini Mikaeli, malaika mkuu, alipokuwa akishindana na Ibilisi, akibishana juu ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumleta shitaka la kumhukumu, bali alisema, ‘Bwana na akukemee.’"
 
Mbona mnajichanganya sana? Mnasema yesu ni mungu, alaf hapohapo unasema mungu wenu alimchagua Maria awe mama wa yesu sasa yesu ni mungu au siyo mungu? au ndo alijichagulia mama?
 
Wakati unajibiwa ongeza na hili. Wale ma bikra 72 watatosha wanaume wote huko kwenye pepo ya mashariki ya kati? Au ni mwendo wa ku share hao 72 kwamba ni free ?
Tusubiri wenyewe waje mkuu
 
Pole sana kwa kukosa maarifa. Hakuna unachokijua. Umchanga sana katika imani. Jibidishe ili uujue ukweli wa kiimani. Hakuna kitu hata kimoja kinachofanywa na Kanisa Katoliki kisicho na msingi wa kiimani.
 
Wewe ndio unajichanganya soma vizuri biblia soma vizuri nilichoandika
Mbona mnajichanganya sana? Mnasema yesu ni mungu, alaf hapohapo unasema mungu wenu alimchagua Maria awe mama wa yesu sasa yesu ni mungu au siyo mungu? au ndo alijichagulia mama?
 
Bikra Maria alipalizwa mbinguni akiwa mzima bila kufa.
Bado anaendelea na safari ya mbinguni au ameshafika ametulia sehemu ? Na atakua anafanya shuhuli gani hapo mahali kwa miaka yote hiyo
 
Hakuna jina la Maria kwenye Biblia.
Acheni kuwapotosha watu.

Mathayo (Mat) 1:18
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Nadhani original ni marry sasa kuipeleka kwenye lugha yako ni maamuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…