Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Mfate tu, Paroko atakujibu vizuri tu, maana hili jambo limeulizwa humu na kutolewa majibu, nyuzi zingine zilifutwa
Hizo nyuzi sikubahatika kuziona mkuu. Majibu gani yalitolewa?
 
Kwanza kwanini anaendekea kuitwa bikira wakati ilitolewa?
 
Kule kana walimtumia akiwa hai. Sasa hivi wanamtumiaje wakati tayari ameishakufa mkuu?
 
Kwa hiyo kupaishwa mbinguni kwa Eliya na Musa na bikra Maria (kama inavyodhabiwa), moja kwa moja waumini wanaweza kupitishia maombi yao kwa watu hawa badala ya kumuomba Yesu moja kwa moja mkuu?
 
Kwa hiyo kupaishwa mbinguni kwa Eliya na Musa na bikra Maria (kama inavyodhabiwa), moja kwa moja waumini wanaweza kupitishia maombi yao kwa watu hawa badala ya kumuomba Yesu moja kwa moja mkuu?
Hakuna maandiko yanayosema mariamu alipaishwa

Pia maandiko yanasisitiza hakuna jina WALILOPEWA WANADAMU ISIPOKUWA JINA LA YESU Tu
 
Kwa hiyo mkuu hapa inabidi tuamini tu bila kuhoji kama vile wapagani wanavyoamini tunguli za sangoma?
Hapo ndio kunashida ya dini hii,ukianza kuhoji unaonekana we ni mpotevu.
 
Hakuna maandiko yanayosema mariamu alipaishwa

Pia maandiko yanasisitiza hakuna jina WALILOPEWA WANADAMU ISIPOKUWA JINA LA YESU Tu
Sawa mkuu. Sasa naanza kupata mwanga kwamba maombi ya wakatoliki kupitia kwa bikra Maria ni ya kudhania tu.
 
Una swali la msingi na mimi naomba kuuliza kwa kujazia nyama,

Kwani wakristo hawawezi kumuomba Muumba wao (Baba yake Yesu) moja kwa moja bila kupitia kwa Yesu kama alivyosema Yesu wamwabudu baba yake tu?

Yohana 4:23
Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.

Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma(mtume).

1korintho 15:28
Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe (Yesu) naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
 
Unaona jinsi mnavyosoma Biblia kama hadithi! Hivi hujawahi kuona msitari ambao Yesu anaagiza chochote tutakachomwomba baba yake kupitia yeye tutakipata? Kazi kweli kweli!
 
1. Ujue kwamba Mungu alipenda kuukomboa ulimwengu kupitia kwa Maria, mama wa Yesu. Huu haukuwa mchezo wa kuigiza. It's the 'economy of salvation' (mpango wa Mungu wa kuwakomboa wanadamu).
2. Mungu hafungwi na muda. Kila jambo mbele ya Mungu linatenda sasa (Zaburi 90:4 na 2 Petro 3:8). Hakuna wakati uliopita au ujao.
3. Harusi ya Kana (Yohane 2:1-25) na pia Yesu alipobaki Jerusalem (Luka 2:41-52) na kutafuta na wazazi wake, 1) kule Kana waliokuwa harusini walimwendea Maria ili amwambie mwanae kwamba wsmeishiwa divai, na Maria akamwambia, na kisha akawaambia wale watu "atakachowaambia fanyeni". 2) Kule Jerusalem pia Maria na Yosefu walikuwa wakimtafuta Yesu, kisha wakamkuta hekaluni na mama yake akamuuliza "mbona umetufanya hivi...?" Katika masimulizi yote mawili Yesu alifuata au alitimiza aliyoambiwa na mama yake. Kanisa Katoliki linatambua umuhimu wa Maria katika maisha ya Yesu na katika ukombozi wa wanadamu. Haiwezekani Maria akabaki pembeni wakati Mungu mwenyewe alipenda kumshirikisha katika kumzaa Yesu na katika ukombozi wa wanadamu. Hivyo, Maria ana hadhi ya kuwa mama yetu kiroho/mama wa Kanisa na tunaweza kumwomba, kama walivyomwomba kwenye harusi ya Kana, amwambie mwanae kwamba wageni harusini wameishiwa divai na Yesu alitimiza alichoambiwa. Tunapomwomba Maria, tunamwomba atuombee kwa mwanae. Tunataka kuonyesha muunganiko uliopo/uhusiano ulioko kati ya yeye na mwanae na sisi pia. Kumbuka pale msalabani Yesu alimwambia Yohane (mmoja wa wale wanafunzi wake aliyempenda zaidi) "huyu ni mama yako" na kwa Maria "huyu ni mwanao" na kuanzia siku hiyo Maria alikwenda kukaa kwa Yohanne. Pia katika Luka 1:48 baada ya kujazwa na Roho Mtakatifu Maria alisema: "kuanzia sasa vizazi vyote vitaniita mbarikiwa/mwenyeheri."
4. Kwa hiyo, tukimwomba Maria (kama nilivyosema kwamba mbele ya Mungu kila kitu ni sasa) hakuna cha wakati uliopita, yote yanatendeka sasa. Na Yesu alisema "anayemwamini hata kama amekufa, ataishi milele" (Yohanne 11:25). Je, Maria alimwamini Yesu? Je, Maria anaishi? Ndiyo.
 
Mtuache jamani na imani zetu..yani huku kwetu hakuna umaskini wa kutupwa wala majini wala mapepo..wakatoliki tuna kula raha hapa duniani..tunaishi kwa raha bila masharti kama waganga..nyumba zetu zina furaha na amani...tunakunywa ka mvinyo ketu na kula kitimoto kg moja...
Yanii kiufupi tuu tuna raha..
Na ukitaka kumjua mama Bikira Maria sali rozali yake...utaona maajabu mengi atakayokutendea kupitia mwanae Yesu Kristo...
Malizia kwa kusema haya
"Bikira Maria Malkia wa amani,mama wa msaada,kimbilio la wakosefu,mama wa tumaini jema,malkia wa familia...msaada wa wagonjwa....n.k
Utuombeee
 
Yupo hai kiroho,na katika sala tunahusisha roho kwahiyo kuwasiliana na roho mwanadamu (mwili na roho) anayonafasi yakupitia kwenye roho iliyokaribu katika unyenyekevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…