kwa bahati nzuri, niujue au nisiujue ukatoliki haiongezi thamani yeyote ya maisha yangu, ila nikiujua ukristo halisi, ule wa Kitabu cha matendo ya mitume (ambao wakatoliki wako mbali nao kabisa) hapo ndio ningefaidika. kwa kukusaidia, mfano wa kukusaidie iwe ni kanisa la kwanza, lile limeandikwa kitabu cha matendo. JIfunze kwa Petro, YOhana, Mathayo, Marko, Paulo, stephano, filipo na wengine. usiangalie jengo, angalia theme ya ukristo wa kwanza ungekuwaje. kwa sababu kama ni jengo najua utakuja na hoja kwamba st.Peter pale vatican ilijengwa na aidha Petro au Paulo kwa hiyo kwa sababu mabaki ya jengo bado yapo basi katoliki ni kanisa la kwanza. mnajidanganya na kujilisha upepo. wakatoliki sio wakristo kabisa, kwa sababu zifuatazo ambazo ndio character halisi ya Mkristo.
1. Wakatoliki (sambamba na wasabato) hawaamini kuokoka. Lakini Yesu alikuja kuleta wokovu. ukisoma MATENDO 2:47 SUV ... wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. KUMBE, kanisa la kwanza watu walikuwa wakiokolewa, ila wakatoliki hamuokoki, mnaabudu dini.
2. Kanisa la kwanza lilijawa na Nguvu za Roho Mtakatifu. kanisa katoliki wanapinga ujazo wa Roho Mtakatifu. ukisoma Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. ukisoma pia MATENDO 19:3-6 3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. 5 Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.
3. WAKATOLIKI wanaomba kwa bikira maria na wafu. Yesu aliseme yeye peke yake ndiye njia kweli na uzima, na tukiomba tupitie JIna lake tu ndio maombi yetu yatafika.
4. Kanisa la kwanza, waliombea wagonjwa na wenye shida wakapona. Kanisa katoliki na hata wasabato, hata pepo tu hawawezi kuombea, kwa sababu hawana Nguvu za Mungu kufukuza pepo. kitu pekee ukiwaletea pepo watatoa sababu nyingi kujitetea na kuonyesha siku hizi sio za maombezi. (ijulikane, maombezi ninayoongelea hapa ni yale ya kitabu cha matendo ya mitume, sio haya maombezi ya manabii wa uongo na wauza maji na mafuta, matapeli wakubwa).
kuna mengi sana ambayo yananifanya niamini katoliki sio wakristo, kwa sababu hawana Kristo. mtu ataitwa Kristo kama akimpokea Kristo.
kwa sababu hizo na nyingi, kumfanya maria ni kitu chochote ni kujilisha upepo na kupoteza muda wakati shetani anakushtukiza akuchinje mwende wote motoni.