Hujaelewa nini mkuu? Hoja nimeijibu kwa kukwambia kwamba huo ni utaratibu tu ambao unaweza ukawekewa condition kwamba kama kuna jambo la dharula hasa la kiroho hata la kimwili, ndoa inafungwa tu. Mfano, labda wachumba wana safari ya pamoja wiki moja ijayo kwenda masomoni Iraq, na kwa mzingira halisi wangependa watoke wakiwa tayari wameshafunga ndoa, basi Askofu/Paroko akiona kuna logic anatoa kibali. Au kama wawili wamekuwa wakiishi pamoja bila ndoa na mmoja wao ni mgonjwa na asingependa afariki bila ya kufunga ndoa, basi kibali kinaweza kutolewa. Hiyo ni mifano tu, usiniquote!