Wakatoliki, imekuaje kipindi cha Kwaresma mmefungisha ndoa ya Mrema?

Habari wana Jukwaa,

Niende moja Kwa moja kwenye hoja, imekuaje sheria ya Kanisa imekiukwa Kwa kufunga ndoa wakati wa mfungo wa Kwaresma? Kwa kipindi hiki huwa hakuna harusi au sherehe yoyote Makanisani ikiwemo ndoa.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa nchi yetu, watu maarufu kupewa kipaumbele hata kama nikwakuvunja sheria zilizopo, yaani mtu akiwa na vijisenti au kiongozi mkubwa serikalini ni mara chache sana sheria kufuatwa.

Wakatoliki nisaidieni kunipa mwongozo hili la Mrema limekaaje?

Kila la heri mzee Mrema katika maisha yako ya ndoa takatifu.

Nimepata ufafanuzi kutoka kwa PAROKO wangu! :-

JE NDOA ZINARUHUSIWA KIPINDI HIKI CHA KWARESMA?

Leo katika mitandao ya kijamii, kumekuwa na mjadala mzito kuhusu ndoa mpya ya Mzee wetu Dkt Augustino Mrema, iliyofanyika hivi punde huko mkoani Kilimanjaro.

Watu wengi wamekuwa wakihoji sana kuwa, je ni halali kufunga ndoa wakati huu wa Kwaresma? Na wengine wameenda mbali zaidi wakisema, siku hizi dini imekuwa ni biashara tu kama biashara zingine, tena pesa imekuwa na nguvu kuhalalisha jambo fulani lionekane jema hata kama ni haramu.

Mpendwa! Hakika nimesikitika mno baada ya kuona mada hii ikishika kasi mno huko mitandaoni, na kibaya zaidi watu wasio Wakatoliki ndio wanaovumisha vitu hivyo vya uongo kuhusu imani yetu.

Ukweli ndoa ni zawadi nzuri ya ajabu na yenye nguvu, kwa kuwa Mungu alituumba kwa upendo na anataka tuudumishe upendo huo katika mahusiano yetu na watu wengine.

Ndoa sio uhusiano tu wa mwanaume na mwanamke, bali ni zaidi ya hayo kwa sababu Kristo ameinua ndoa na kuwa Sakramenti.

Hii inamaanisha kwamba, ndoa ni ishara inayoonekana inayomfunua Bwana Yesu na upendo wake usioonekana wala usio na mwisho.

Pia Katekisimu ya Kanisa Katoliki namba 1601 inasema, ndoa ni agano la maisha kati ya mwanaume na mwanamke, ambalo huamriwa kwa ustawi wa mwenzi na malezi ya watoto.

Baada ya kuona hayo, turudi sasa katika mada yetu kuu inayosema: Je ni halali kufunga ndoa wakati wa Kwaresma?

Jibu: Sheria za Kanisa Katoliki haijakataza mtu kufunga ndoa wakati wa Kwaresma, kwa sababu ndicho kipindi maalumu cha toba ambacho mwanadamu anaamua kwa dhati kumrudia Mungu wake kwa kuacha dhambi na kutenda yaliyo mema.

Hivyo mtu anapotaka kufunga ndoa kipindi hiki cha Kwaresma, anaruhusiwa kabisa kufunga. Maana Kanisa haliwezi kumkataza mtu asifunge ndoa ili aendelee kuishi kwenye uchumba sugu, kitu ambacho ni kinyume na Mafundisho ya Neno la Mungu linavyosema.

Kadhalika ndoa inaweza kufungwa wakati wowote ule, lakini siku ya Alhamisi kuu na Ijumaa kuu ndizo siku pekee ambazo Kanisa haimruhusu mtu kufunga ndoa. Kwa sababu ndani ya siku hizo mbili, Kanisa linakuwa na tafakari kubwa yenye huzuni ndani yake kuhusu mateso na kifo cha Yesu pale Msalabani.

Kwahiyo nihitimishe kwa kusema kuwa, ndoa wakati huu wa Kwaresma zinaruhusiwa sana ila kinachokatazwa pale ni kwamba, pasiwepo na shamra shamra yoyote, sherehe wala vifujo vya furaha yaani ndoa inakuwa kimya kimya pasipo na makelele yoyote.

Na ndio maana watu kutaka ufahari, wanaamua kufunga ndoa zao kabla na baada ya kipindi hiki cha Kwaresma. Na sio kwamba Kanisa linawazuia, hapana, naomba ieleweke hivyo.

...TUMSIFU YESU KRISTO...

Nionavyo-
Mwenye kuelewa, ataelewa!
 
mi niliona picha za GIGY MONEY akiwa ndan ya tinted na macho matatu pembeni mzee wa tLp

hata hawakukaa pozi la kikanisani

utazani wasanii PAPA YA MOBIMBA.

Sizani km ilikuwa ni ndoa ile.

kilaini alifafanue hili
Yote hata hapa kwetu kkkt kuna mtu kafunga ndoa jana
 
Milele Amina
 
Hapo hujadili hoja ila unaleta personal attack........jadili hoja mkuu na Kwa taarifa yako mm siyo mkatoriki ila nimeishi kwenye ukatoriki Kwa miaka kama 6 hivi...... kwahiyo usilete ujuaji sana mkuu
Umeatakiwa wapi hapo....kakupa na mfano juu!!
 
Je ina maana kuwa hii ndoa ni batili na mama mrema hana haki katika mirathi ya Dkt.Mrema?
 
Habari wana Jukwaa,

Niende moja Kwa moja kwenye hoja, imekuaje sheria ya Kanisa imekiukwa Kwa kufunga ndoa wakati wa mfungo wa Kwaresma? Kwa kipindi hiki huwa hakuna harusi au sherehe yoyote Makanisani ikiwemo ndoa.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa nchi yetu, watu maarufu kupewa kipaumbele hata kama nikwakuvunja sheria zilizopo, yaani mtu akiwa na vijisenti au kiongozi mkubwa serikalini ni mara chache sana sheria kufuatwa.

Wakatoliki nisaidieni kunipa mwongozo hili la Mrema limekaaje?

Kila la heri mzee Mrema katika maisha yako ya ndoa takatifu.

Ndoa ni moja ya sakramenti kati ya zile saba. Kumbuka vizuri.

Nimesema ndoa sio sherehe. Ni kama watu wanavyoaswa kutubu sana kipindi cha kwaresma ili wamrudie MUNGU vivyo hivyo wanaoishi maisha ya zinaa wanavyoaswa kufunga ndoa.

Nimeongezea tu. Kama umesoma commnt ya wa kwanza ukijumlisha na hii utaelewa.
 
Hapo hujadili hoja ila unaleta personal attack........jadili hoja mkuu na Kwa taarifa yako mm siyo mkatoriki ila nimeishi kwenye ukatoriki Kwa miaka kama 6 hivi...... kwahiyo usilete ujuaji sana mkuu
Kama sio mkatoliki unaeleweshwa huelewi basi wewe ni punguani
 
Habari wana Jukwaa,

Niende moja Kwa moja kwenye hoja, imekuaje sheria ya Kanisa imekiukwa Kwa kufunga ndoa wakati wa mfungo wa Kwaresma? Kwa kipindi hiki huwa hakuna harusi au sherehe yoyote Makanisani ikiwemo ndoa.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa nchi yetu, watu maarufu kupewa kipaumbele hata kama nikwakuvunja sheria zilizopo, yaani mtu akiwa na vijisenti au kiongozi mkubwa serikalini ni mara chache sana sheria kufuatwa.

Wakatoliki nisaidieni kunipa mwongozo hili la Mrema limekaaje?

Kila la heri mzee Mrema katika maisha yako ya ndoa takatifu.

Mrema ni mkatoliki?
 
Kama ni utaratibu uwe Kwa wote siyo Kwa watu wa tabaka fulani
Kuna huduma uliitaka ukanyimwa?
Huo ni utaratibu tu sio Sheria. Hpo yawezkana mzee alishaanza kuishi na huyo bibie?? Sasa kumuidhinisha iwe tabu Kiasi hicho.unaijua dk mbili Zako zinazofuataaaa??
 
Back
Top Bottom