Wakatoliki, imekuaje kipindi cha Kwaresma mmefungisha ndoa ya Mrema?

Enzi zamani ukisoma historia kipindi cha kwaresma ilikuwa marufuku hata mtu kulala na mkewe.Siku hizi aaaa
Siku hizi mambo yamebadilika sana hasa mtu akiwa maarufu au mwanasiasa
 
Kaulize vizuri utaelewesha........na si RC tu ni Makanisa yote
Nakushauri ukaombe kwanza. Ukikataliwa ndio uje hapa kulalamika, tena uziweke hadharani hoja zako ulizopeleka na jinsi walivyokujibu. Ukikubaliwa sio lazima urudi hapa, maana kukubaliwa ni jambo la kawaida, sio la ajabu kama unavyolazimisha lionekane
 
Kaulize vizuri utaelewesha........na si RC tu ni Makanisa yote
Mimi ni Mkatoliki.

Nimeshashuhudia ndoa nyingi tu zinafungwa wakati wa Kwaresma kama kuna sababu ya msingi.

Hata leo Mama Kanisa anasherehekea kupashwa habari kwa Bikra Maria kama atakuwa Mama wa Mungu. Hii ni sherehe kabisa na inasherehekewa tukiwa katikati ya Kwaresma.

Kila Jumapili hatufungi, maana ni siku za sherehe... Hata kama tupo kwenye Kwaresma.

Ndio maana nikakuuliza utaratibu wa wapi huo? Hebu tueleze.
 
Nakushauri ukaombe kwanza. Ukikataliwa ndio uje hapa kulalamika, tena uziweke hadharani hoja zako ulizopeleka na jinsi walivyokujibu. Ukikubaliwa sio lazima urudi hapa, maana kukubaliwa ni jambo la kawaida, sio la ajabu kama unavyolazimisha lionekane
Ndiyo akili zetu hizi,mtu akileta jambo amekataliwa? Wakati wa Kwaresma hakuna Kanisa linafungisha ndoa,labda kama hujui
 
Umeshuhudia Wakati wa Kwaresma?
 
Injili ya mathayo kwani imekataza?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana nikakuuliza utaratibu wa wapi huo? Hebu tueleze.
Huyu hajaomba na kukataliwa. Kama umemsoma vizuri, alitaka kulazimisha mtazamo wake humu kwamba 'vigogo' wanabebwa katika kanisa Katoliki. Bahati nzuri ametukuta wengine humu tupo kwenye Halmashauri za Walei Parokia, tunajua yote na pia tunajua mitazamo ya watu wengine wa nje walio na tabia za kupiga mawe Kanisa Katolik. Mpango wake umefeli kuanzia post ya pili ya uzi huu. Kwa sasa nachojaribu ni kujitutumua tu, ila anatafuta njia ya kutokea taratibu
 
Utakuwa umevurugwa mkuu.......kwanza nikweli Makanisa yanawabeba watu maarufu na wanasiasa hata kama hawafuati taratibu za Kanisa......kwenye ndoa na misiba hilo halina ubishi,pili Kwaresma hakuna Kanisa ndoa inafungwa
 
Nimeishi RC zaidi ya miaka 6, usiniulize nilikuwa nafanya nini
Basi kukusaidia, yeyote anayetaka kufunga ndoa kipindi hiki, mwambie akamueleze Paroko wake. Sana sana kuna requirement ya kiserikali kwamba nia ya kufunga ndoa itangazwe mara tatu kwa kipindi cha wiki tatu kabla ya siku ya ndoa, sasa serikalini siwezi kuwasemea, ila kanisani hata kesho katika ibada ya asubuhi ukipeleka ombi likakubaliwa utafunga tu
 
Utakuwa umevurugwa mkuu.......kwanza nikweli Makanisa yanawabeba watu maarufu na wanasiasa hata kama hawafuati taratibu za Kanisa......kwenye ndoa na misiba hilo halina ubishi,pili Kwaresma hakuna Kanisa ndoa inafungwa
Acha kulalamika, tafuta hela ukalipe mahari umalize mambo ya kimila. Isije ukawa umekwamishwa kimila halafu unasingizia Kanisa. Kwanza Kwaresma yenyewe ni siku 40 tu, huna haja ya kuitolea macho
 
Ni siku mbili tu ambazo Kanisa Katoliki haliwezi kufungisha ndoa nazo ni: IJUMAA KUU na JUMAMOSI KUU! Siku zingine ni ruksa kwa busara ya ya Paroko wako!
 
Kwenye hii imani kuna mambo mengi ambayo ni miongozo ya binadamu si maagizo toka kwa Mungu,taratibu ni nyingi mno walizoweka hao walioanzisha dhehebu lakini ukiangalia andiko lenyewe khaswa hakuna mahala linaelekeza hizo mambo,ndio maana utakuta kkkt wanamuongozo wao ,Agrican nao hivyo Romani nao pia so kila thehebu wamejiwekea yao kulingana na matakwa ya muasisi wa hilo dhebu,so kwakuwa ni mipango ya wanadamu haiwezi kosa double standard mkuu
 
Acha kulalamika, tafuta hela ukalipe mahari umalize mambo ya kimila. Isije ukawa umekwamishwa kimila halafu unasingizia Kanisa. Kwanza Kwaresma yenyewe ni siku 40 tu, huna haja ya kuitolea macho
🤣🤣🤣Njoo uwe mshenga Kwa mke wa pili mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…