Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

Wakatoliki mnakwama wapi kwenye media?

Ngoja waje...

Cc: Mahondaw
naasubiri waje, ila waje kwa hoja, wasijisikie vibaya kuambiwa ukweli, ni muhimu ili kuponya roho zao. na ukweli huu huwa anaupata yule aliyejaribu kutoka, bahati mbaya sana wakatoliki wameshikilia watu kwenye fundisho la kuombewa baada ya kufa, watu wanawaza kwamba hata akitenda dhambi siku ile akizikwa na padre ataombewa na kusamehewa dhambi zake. watu wanaogopa kutoka huko wasije kushindwa kuzikwa na padre. ndio maana mapadre wana jeuri mno utafikiri wao ndio wanagawa uzima, usipohudhuria ibada hata za mitaani wanakwambia hatutakuzika, mtu anahofu kwamba asipozikwa na padre hataenda mbinguni ila motoni, wakatoliki wanaishi kifungoni, ukigombana tu na kanisa la katoliki hata kwenye mambo ya siasa watu wanakwambia tutakutana tu (siku ya maziko),

hapo ndipo shetani alipowashikilia, laiti wangejua kuwa ukishakufa nyumbani au hospitalini imeshatoka hiyo, hakuna kutubu tena na hata ukiombewa na maombi milioni hautasemehewa kamwe. kwasababu kutubu na kusamehewa ni wakati ukiwa hai, baada ya kifo ni hukumu tu, ndio maana Yesu alisema kesheni, kama kungekuwa na kusamehewa dhambi kwa kuombewa tukishakufa pasingekuwa na haja ya kuacha dhambi manake watu wangefanya tu dhambi na wakifa tunawaombea wanasamehewa hukohuko.

WAEBRANIA 9:27 - 28 INASEMA, Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; kadhalika Kristo naye akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiano kwa wokovu.
 
Ukweli ni kwamba nipo home naperuzi stesheni za TV. Ukija clouds unakutana na chomoza, ukurudi chanel ten yupo Mwamposa. TVE yupo kuhani Musa. Wasafi yupo tena Mwamposa. Naperuzi zaidi nakutana na Upendo TV ya walutheri. Sasa Jumapili natoka kanisani kazi yangu ni kutazama maudhui ya madhehebu mengine tu? TV tumaini mmeshindwa kuingia DStv? Hata hivyo content mnazo?

Ukirudi kwenye redio ni yaleyale. Usiku redio zote zimeshikwa na hawa walokole. Namaanisha almost zote, tena hadi alfajiri. Ukija redio Tumaini na redio Maria ni sala %80. Hivi, ni nani anakaa au yuko nyumbani aache kufanya pilika za nyumani atulie kufuatilia sala redioni? Hata hao wanaoongoza sala redioni wametulia sehemu. Badilikeni

Waumini wakitoroka msiwalaumu. Kanisa katoliki ni kongwe kweli ila ifike sehemu mabadiliko, hasa kwenye uinjilishaji yawepo. Watu/waumini wanataka content.

Kanisa halijakosa waumini wenye karama za kuhubiri. Kwa nini wasipewe nafasi kwenye media? Kanisa halijakosa waumini wenye uwezo bunifu kwenye vipindi/maudhui. Mnatengeneza mazingira gani kuwawezesha hawa.

Niishie hapa kwa leo.
Labda maagizo ya Papa,

mi sio mkatoliki ila ile salamu Maria na sala zinginezo nimeikariri mwanzo mwisho kutokana na kuisikiliza sana hiyo redio ile miaka ya giza ambapo stesheni zilikuwa za kutafuta na tochi
 
Duh! Miaka ya giza tena? 😁
 
Wakatoliki hata makanisa yetu yamejificha ukiwa na shida yatafute
Sembuse media
Kwa necha ya makanisa yetu, ni kweli yako ndani ndani. Machache yako njiani kama Makuburi, Kinyerezi, Kristo Mfalme (kwa Dar). Ni makubwa sana na yenye huduma karibu zote za msingi. Ni ngumu kufananisha na makanisa ukubwa wa nyumba ya kuishi, au misikiti. Kwa maeneo tu tupo vizuri
 
Bahati
kwa bahati mbaya sana, ni neno gumu nitakuambia, linakwaza na kuonyesha kama vile najiinua au labda natukana watu au nabeza imani za watu, ila dawa hata kama ni chungu ni muhimu kuinywa. MAPADRE HAWANA ROHO MTAKATIFU, KWASABABU HAWAJAOKOKA NA HAWAAMINI KUOKOKA.

Tangu siku ya Pentecost, Roho Mtakatifu aliposhuka, kuna ishara za wazi kabisa zinazoweza kukuonyesha pasi na shaka kuwa huyu ana Roho na huyu hana, imani hii inaweza kukusaidia umpate Roho na hii haiwezi kukusaidia. hata kipindi kile pamoja na kwamba wayahudi walikuwa wanasali sana kwenye masinagogi, tena pamoja na mitume (kwasababu awali mitume walikuwa bado wanaenda kusali kwenye masinagogi yaleyale pamoja na wayahudi), lakini ni mitume tu walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wale waliokuwa wakiokoka. wasiookoka hata kama walishika dini namna gani, hawakuwa na Roho Mtakatifu, na ndivyo ilivyo hadi sasa. kwa bahati mbaya, hata utetee namna gani au kuwasafisha mapadre kwamba wana Roho au la, hautawasaidia, wewe sio final say, ila kwa kuangalia Neno la Mungu unaweza kujua huyu ana Roho na huyu hana.

ISHARA ZA ROHO MTAKATIFU

1. KUNENA KWA LUGHA
. kila aliyejazwa Roho Mtakatifu kwenye kitabu cha Matendo ya mitume, alinena kwa Lugha, na wale ambao hawakunena waliwekewa mikono ili wanene. Marko 16:17-18 "Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya,..." sasa tuambie ni padre gani ulishawahi kumwona ananena kwa lugha? au mkatoliki gani anene kwa lugha kama hajafukuzwa ukatoliki siku hiyohiyo? why? MATENDO 19:1 -10 inasema, Ikawa Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso, akakutana na wanafunzi kadhaa wa kadhaa huko, akawauliza, je? mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini? wakamjibu la hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. akawauliza basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? wakasema kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, kyaani Yesu. waliosikia haya wakabatizwa kwa Jina la Bwana Yesu. na Paulo alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao, wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri. sasa tueleze, ulishawahi kuona wapi Padre ana dalili yeyote kama hii? tusijidanganye, bila kujazwa Roho kwa namna hii,hauna Mungu. na huwezi pata kama haujaokoka, na kama dini yako inabeza kuokoka manake wote kuanzia viongozi hadi muumini hamna Mungu, ila mna dini.

2. ROHO MTAKATIFU ANADHIHIRISHWA PIA KWA MATUNDA YAKE. ila hiyo haimaanishi kwamba hutakiwi kunena, unalazimika kujazwa ila tutajua kama bado amekaa ndani yako au ameshakuacha kwa kuangalia matunda yako. yapo Wagalatia 5:22.

3. Wakorintho 12 kuna karama za Roho Mtakatifu. 1Wakorintho 12, ndani yake tutajie ipi ulishawahi kuiona kwa padre yeyote, au mkatoliki yeyote (ukiondoa wale wachache karismatic).

mjadala umefunguliwa, leta hoja, hakuna matusi.
Nzuri pia ni kwamba na wewe sio final say. Na vigezo vya kuwa na huyo roho huviweki wewe. Pia hujawajua vizuri mapadre. Kwa upande mwingine nao ni binadamu.

Sasa tuje kwenye kuokoka. Ndio kuongozwa ile sala ya toba? Hayo makanisa yaitwayo ya kiroho tunayajua. Vijana wengi wanatimkia huko kukwepa wajibu wa kiimani. Free style churches ambapo wanadhani mbele ya Mungu unaenda tu kirahisi. Kutubu dhambi wanadhani ni mchakato rahisi. Sisi tunajua kuokoka ni baada ya kufa. Binadamu anaongoka. Waganda waliwahadaa na hilo neno "balokole". Binadamu anaingoka akisubiria kuokolewa siku ya mwisho
 
... bahati mbaya sana wakatoliki wameshikilia watu kwenye fundisho la kuombewa baada ya kufa, watu wanawaza kwamba hata akitenda dhambi siku ile akizikwa na padre ataombewa na kusamehewa dhambi zake.
Hiyo umesema wewe. Ingekuwa wanaamini kuombewa tu baada ya kufa basi wasingekuwa na misa za Jumatatu hadi Jumapili kila siku zinazohudhuriwa na watu walio bado hai. Wakatoliki wanaamini kuwa Mungu hapangiwi na mwanadamu namna ya kumsamehe mwenye dhambi, lakini Walokole na waprotestanti wengine mnaamini kuwa mnafahamu Mungu hawezi kufanya lolote kwa mtu aliyekufa, kwamba mnafahamu mipango yote ya Mungu, kwamba Mungu hawezi kumsamehe mfu, kwamba mnafahamu hali ya kila mtu katika nukta zake za mwisho za uhai.

By the way naomba nikuulize, kuna dhehebu gani linalozika mtu kimya kimya bila ibada? Ile ibada ya mazishi kwa walokole na waprotestanti pamoja na waisilamu, huwa ni ya nini hasa?
 
WAEBRANIA 9:27 - 28 INASEMA, Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
Kwani wewe unaelewa nini maana ya hukumu? Kusamehewa makosa sio hukumu? Wakatoliki walijenga Kanisa, Hospitali na Shule, walijua umuhimu wa elimu. Tatizo hapa ni elimu!
 
Kwani wewe unaelewa nini maana ya hukumu? Kusamehewa makosa sio hukumu? Wakatoliki walijenga Kanisa, Hospitali na Shule, walijua umuhimu wa elimu. Tatizo hapa ni elimu!
sijawahi kusoma shule iliyojengwa na wakatoliki, hata hivyo elimu Tanzania haikuletwa na wakatoliki peke yake.

kwa kukusaidia, maana ya huo mstari ni kwamba, Mungu amekupatia nafasi sasaivi ukiwa hai utubu, siku utakayokufa ndio mstari unachorwa mwisho wa nafasi ya kutubu, kilichobaki ni kusubiri hukumu aliyoielezea Yesu atakapokuja na wingu la malaika, pale atakapokuja kuchambua kondoo na mbuzi. wala suala hili halihusiani na elimu, hata asiyesoma linaeleweka kabisa.

umeuliza kama kusamehewa makosa sio hukumu? Naomba nikusaidie kwamba, kusamehewa makosa sio hukumu, kuhukumiwa/hukumu hata kwa akili ya kawaida kabisa ni kupewa adhabu kutokana na makosa, sasa ukisamehewa hupewi adhabu, utasemaje hiyo ni hukumu sasa? kwa upande wenu, Mtu akishakufa, anasamehewaje sasa, unasamehewa wewe unayemwombea au yule aliyekufa? na wakati huo huo Biblia inasema kila mtu atabeba furushi lake mwenyewe, wewe utabeba dhambi zako mwenyewe kama hautazitubu ukiwa hai, na mwengine naye hivyo hivyo, huwezi kubeba dhambi za mtu aliyekufa ati utubu kwa niaba yake.

Yesu alishahukumiwa kwa niaba yetu kwa kumwaga damu yake, alikufa kwa niaba yetu (isaya 53), hivyo tunapomwendea yeye tukiwa hai anabeba dhambi zetu, ukishakufa utamkabidhi saa ngapi dhambi? na kama hiyo nafasi ipo si umkabidhi hukohuko ulikoenda si mtakuwa naye umwombee hukohuko msamaha basi kama inawezekana na ninyi kuombea wafu msamaha huku duniani kungekuwa na maana gani? yaani aliyekufa kama ana nafasi tena ya kutubu, si ameenda huko alikoenda kama nafasi ipo ataombea msamaha hukohuko ninyi wa huku duniani ambao bila shaka mpo mbali mno kuliko kwenye msamaha hauoni kama msingehitaji kabisa hata kumwombea msamaha, kama nafasi hio ingekuwepo..shida ni kwamba hakuna opportunity hiyo na mnapoteza muda kuombea watu msamaha wakishakufa, baada ya kifo ni kusubiri hukumu hakuna longolongo hizo. msidanganye watu.

kwa kukusaidia, soma kitabu chote cha Matendo ya mitume, angalia wapi kanisa la kwanza wale mitume wote wapi walikuwa na fundisho kama hili unaloliamini. usije ukajidanganya, patana na Mungu wako kabla pumzi haijakata, ikikata umeshaondoka na mzigo wako.
 
Hiyo umesema wewe. Ingekuwa wanaamini kuombewa tu baada ya kufa basi wasingekuwa na misa za Jumatatu hadi Jumapili kila siku zinazohudhuriwa na watu walio bado hai. Wakatoliki wanaamini kuwa Mungu hapangiwi na mwanadamu namna ya kumsamehe mwenye dhambi, lakini Walokole na waprotestanti wengine mnaamini kuwa mnafahamu Mungu hawezi kufanya lolote kwa mtu aliyekufa, kwamba mnafahamu mipango yote ya Mungu, kwamba Mungu hawezi kumsamehe mfu, kwamba mnafahamu hali ya kila mtu katika nukta zake za mwisho za uhai.

By the way naomba nikuulize, kuna dhehebu gani linalozika mtu kimya kimya bila ibada? Ile ibada ya mazishi kwa walokole na waprotestanti pamoja na waisilamu, huwa ni ya nini hasa?
nadhani hata hatuhitaji kutumia nini wakatoliki wanaamini kupangiwa au kutopangiwa na nini waprotestant wanaamini au hawaamini. TUNACHOTAKIWA KUANGALIA NI NINI NENO LA MUNGU LINASEMA. hoja isimamie hapo. na hii ndio sababu tunasema wakatoliki walipoteza dira baada ya serikali nyingi kuingilia kanisa, upagani ukaingia, na hawafanani hata kitu kimoja na kanisa la mitume wale wa kwanza.

SWALI: je? ni kweli au sio kweli, kwamba huwa mnamwomba Mungu amsamehe marehemu.

SWALI: Je? ni kweli au sio kweli Biblia Wagalatia 6:5 inasema kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe na Warumi 14:12 inasema Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Ukijibu hayo maswali nitajua namna gani ya kukusaidia uelewe.

IBADA ya kuzikana ni kwa ajili ya kuwakumbusha tu wale ambao bado wapo hai kwamba kuna kufa, kuna siku wanaweza kufa hivyo wajiandae. it is so ceremonial and more of religious, ni desturi tu lakini haina impact yeyote kwasababu wapo wengi walikufa bila hata ibada na haina imnpact yeyote. mfano, ukiliwa na simba, ukiliwa na mamba, ukitupwa baharini, meli imezama, umeungua moto haujulikani u majivu tu, n.k, ibada yako itakuwa na maana gani? kuzikwa kuna thamani gani?
 
vi
Bahati

Nzuri pia ni kwamba na wewe sio final say. Na vigezo vya kuwa na huyo roho huviweki wewe. Pia hujawajua vizuri mapadre. Kwa upande mwingine nao ni binadamu.

Sasa tuje kwenye kuokoka. Ndio kuongozwa ile sala ya toba? Hayo makanisa yaitwayo ya kiroho tunayajua. Vijana wengi wanatimkia huko kukwepa wajibu wa kiimani. Free style churches ambapo wanadhani mbele ya Mungu unaenda tu kirahisi. Kutubu dhambi wanadhani ni mchakato rahisi. Sisi tunajua kuokoka ni baada ya kufa. Binadamu anaongoka. Waganda waliwahadaa na hilo neno "balokole". Binadamu anaingoka akisubiria kuokolewa siku ya mwisho
vigezo vipo kwenye Neno la Mungu, hata haihitaji kubishana, angalia Neno la Mungu, fuata. usitengeneza vigezo vyako au usifuate vigezo vilivyowekwa na dini.
 
nadhani hata hatuhitaji kutumia nini wakatoliki wanaamini kupangiwa au kutopangiwa na nini waprotestant wanaamini au hawaamini. TUNACHOTAKIWA KUANGALIA NI NINI NENO LA MUNGU LINASEMA. hoja isimamie hapo. na hii ndio sababu tunasema wakatoliki walipoteza dira baada ya serikali nyingi kuingilia kanisa, upagani ukaingia, na hawafanani hata kitu kimoja na kanisa la mitume wale wa kwanza.

SWALI: je? ni kweli au sio kweli, kwamba huwa mnamwomba Mungu amsamehe marehemu.

SWALI: Je? ni kweli au sio kweli Biblia Wagalatia 6:5 inasema kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe na Warumi 14:12 inasema Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Ukijibu hayo maswali nitajua namna gani ya kukusaidia uelewe.

IBADA ya kuzikana ni kwa ajili ya kuwakumbusha tu wale ambao bado wapo hai kwamba kuna kufa, kuna siku wanaweza kufa hivyo wajiandae. it is so ceremonial and more of religious, ni desturi tu lakini haina impact yeyote kwasababu wapo wengi walikufa bila hata ibada na haina imnpact yeyote. mfano, ukiliwa na simba, ukiliwa na mamba, ukitupwa baharini, meli imezama, umeungua moto haujulikani u majivu tu, n.k, ibada yako itakuwa na maana gani? kuzikwa kuna thamani gani?
Yapo mambo mengi huyajui, au unajitoa tu ufahamu. Unaposema kila mtu ataubeba mzigo wake, Yesu alikuja kufanya nini? Ni kweli ataubeba mzigo wake lakini wakati fulani aliisaidiwa kuongoka. Hivyo kwenye ile hukumu ya mwisho utatoa hesabu zako.

Suala la ibada za wafu sio la kimazihara. Watu huchukua hata kidole kilichosalia baada ya kuliwa na mamba na kuja kukifanyia ibada ya maziko. Mwanadamu si hayawani aachwe tu.
 
ndugu yangu, wala sisemi mimi, nimeweka mistari ya Biblia hapo, nakuwekea tena ili ubishane nayo.

Wagalatia 6:5 inasema kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe na Warumi 14:12 inasema Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Anaposema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe manake kila mtu atakuwa accountable kwa dhambi zake mwenyewe zile ambazo amekaidi kama wengi wanavyofanya, hajataka kutubu. Yesu alikuja kulipa garama ya dhambi, na kwa kufanya hivyo Yesu haimaanishi basi dunia yote imeshasamehewa, hapana, yule tu anayezipeleka dhambi zake kwa Yesu ndiye anasamehewa, ndio hukumu yake ya dhambi inafutwa, wale wenye shingo ngumu wanabaki na dhambi zao na watakuwa accountable personally. na hii ndio sababu Yesu alisema kwamba hiii ndio itakuwa hukumu kwamba Nuru imekuja duniani lakini watu wanaikimbia nuru wanapenda giza.

nakuonea huruma sana unapoujali sana huu mwili, unasema suala la ibada ya wafu sio masihara? hiki ndicho kifungo ambacho nilikuwa nasema wakatoliki mmefungwa, ni kifungo kikubwa kuamini kwamba siku ile utakapokufa padre atakuombea na utasamehewa dhambi zako, pambana na mistari nimekuwekea hapo juu, naw ewe kama unayo kinzani niwekee, haujaweka hata mmoja, why? unasema mtu akifa hata kidole tu kitachukuliwa aombewe au azikwe, na kama msipokipata manake nini? wale waliopotea na ndege ya malaysia mmeshapata kidole hata kimoja? mtu akiliwa na mamba mamba akaenda zake kwenye kina cha maji huko mtamfanya nini au mtasubiri ajisaidie haja kubwa ili mchukue kinyesi cha mamba mkakizike?

hiki ndicho kifungo watu wengi wamefungwa, na hakipo kwenye Biblia. ninyi mnaosoma hapa jueni kuwa,

1. Yesu Kristo alikufa, akalipa deni la dhambi, ukitubu anazifuta, usipotubu unabaki nazo.

2. Mungu ameweka nafasi ya mtu kuishi, ukiwa hai tengeneza mambo yako na Mungu,ukifa ndio deadline yako ya kutubu, huko utakakoenda badala ya Yesu Kristo kubeba dhambi zako utakuwa umeshachelewa utazibeba wewe mwenyewe na utakuwa accountable personally kwasababu aliyekuja azichukue haukumpatia mizigo yako hiyo.

3. Huu mwili ni udongo tu, roho ndio itiayo uzima mwili haufai kitu. ukifa unaoza unakuwa udongo tu, kinachotafutwa kuokolewa ni roho yako, huko ndiko kwenye dhambi, na huko ndiyo kwa kusafishwa dhambi, huko rohoni ndiko kunakotubu, ukitubu dhambi na kuziacha roho inakuwa safi, na hata ukifa hapa utaoza ila roho yako itapona. ukifa na dhambi, ni hasara.

4. Kumwombea mtu akiwa amekufa kwamba asamehewe dhambi haipo kwenye Neno la Mungu, Mitume hawajawahi kufanya hivyo, na Yesu hakuagiza hivyo, ni kitu tu kimetungwa na wanadamu, kama vile tu papa anavyotaka kuingiza kuombea mashoga, miaka ijayo hili nalo mtakuwa nalo kwenye ibada zenu.

5. unaweza kumwombea mtu akiwa hai kama ametenda dhambi, Mungu akamsamehe na kumponya ugonjwa wake, ila ni pale atakapotubu yeye na kukiri, msamaha wa dhambi unatokana na kukiri kuwa umetenda dhambi, ukifa huwezi kukiri, imeisha hiyo.

6. wengi hamtaelewa hili hadi siku mtakapofunguka macho na kukimbia kuabudu hiyo dini. Mungu awasaidie.
 
Uko sawa . Vituo vya TV Vya kikatoliki Tanzania ni vichache Sana almost kimoja tuu TV TUMAINI. Redio maria Wana wateja wengi sana ila hawana TV ni muda Sasa nao waanzishe Tv. Kampuni nyingi za TV Tanzania hawajaweka ile TV ya kimataifa ya Kikatoliki EWTN ambayo ni FREE ON AIR
 
umeuliza kama kusamehewa makosa sio hukumu? Naomba nikusaidie kwamba, kusamehewa makosa sio hukumu,
kuhukumiwa/hukumu hata kwa akili ya kawaida kabisa ni kupewa adhabu kutokana na makosa, sasa ukisamehewa hupewi adhabu, utasemaje hiyo ni hukumu sasa?
Ndio maana nikasema kuna umuhimu wa elimu kabla ya kusoma maandiko na kukimbilia kuhubiria watu. Ndio maana umukimbilia kusema kwa akili ya kawaida kwa kuwa hukutaka kutumia akili halisi. Neno hukumu sio lazima iwe adhabu tu. Inaweza ikawa ni adhabu au kusamehewa/kuachiwa huru.
 
weka walau mstari mmoja basi wa Biblia ili uonekana na wewe ulikuwa unajadili kwa hoja.
 
ndugu yangu, wala sisemi mimi, nimeweka mistari ya Biblia hapo, nakuwekea tena ili ubishane nayo.

Wagalatia 6:5 inasema kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe na Warumi 14:12 inasema Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Anaposema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe manake kila mtu atakuwa accountable kwa dhambi zake mwenyewe zile ambazo amekaidi kama wengi wanavyofanya, hajataka kutubu. Yesu alikuja kulipa garama ya dhambi, na kwa kufanya hivyo Yesu haimaanishi basi dunia yote imeshasamehewa, hapana, yule tu anayezipeleka dhambi zake kwa Yesu ndiye anasamehewa, ndio hukumu yake ya dhambi inafutwa, wale wenye shingo ngumu wanabaki na dhambi zao na watakuwa accountable personally. na hii ndio sababu Yesu alisema kwamba hiii ndio itakuwa hukumu kwamba Nuru imekuja duniani lakini watu wanaikimbia nuru wanapenda giza.

nakuonea huruma sana unapoujali sana huu mwili, unasema suala la ibada ya wafu sio masihara? hiki ndicho kifungo ambacho nilikuwa nasema wakatoliki mmefungwa, ni kifungo kikubwa kuamini kwamba siku ile utakapokufa padre atakuombea na utasamehewa dhambi zako, pambana na mistari nimekuwekea hapo juu, naw ewe kama unayo kinzani niwekee, haujaweka hata mmoja, why? unasema mtu akifa hata kidole tu kitachukuliwa aombewe au azikwe, na kama msipokipata manake nini? wale waliopotea na ndege ya malaysia mmeshapata kidole hata kimoja? mtu akiliwa na mamba mamba akaenda zake kwenye kina cha maji huko mtamfanya nini au mtasubiri ajisaidie haja kubwa ili mchukue kinyesi cha mamba mkakizike?

hiki ndicho kifungo watu wengi wamefungwa, na hakipo kwenye Biblia. ninyi mnaosoma hapa jueni kuwa,

1. Yesu Kristo alikufa, akalipa deni la dhambi, ukitubu anazifuta, usipotubu unabaki nazo.

2. Mungu ameweka nafasi ya mtu kuishi, ukiwa hai tengeneza mambo yako na Mungu,ukifa ndio deadline yako ya kutubu, huko utakakoenda badala ya Yesu Kristo kubeba dhambi zako utakuwa umeshachelewa utazibeba wewe mwenyewe na utakuwa accountable personally kwasababu aliyekuja azichukue haukumpatia mizigo yako hiyo.

3. Huu mwili ni udongo tu, roho ndio itiayo uzima mwili haufai kitu. ukifa unaoza unakuwa udongo tu, kinachotafutwa kuokolewa ni roho yako, huko ndiko kwenye dhambi, na huko ndiyo kwa kusafishwa dhambi, huko rohoni ndiko kunakotubu, ukitubu dhambi na kuziacha roho inakuwa safi, na hata ukifa hapa utaoza ila roho yako itapona. ukifa na dhambi, ni hasara.

4. Kumwombea mtu akiwa amekufa kwamba asamehewe dhambi haipo kwenye Neno la Mungu, Mitume hawajawahi kufanya hivyo, na Yesu hakuagiza hivyo, ni kitu tu kimetungwa na wanadamu, kama vile tu papa anavyotaka kuingiza kuombea mashoga, miaka ijayo hili nalo mtakuwa nalo kwenye ibada zenu.

5. unaweza kumwombea mtu akiwa hai kama ametenda dhambi, Mungu akamsamehe na kumponya ugonjwa wake, ila ni pale atakapotubu yeye na kukiri, msamaha wa dhambi unatokana na kukiri kuwa umetenda dhambi, ukifa huwezi kukiri, imeisha hiyo.

6. wengi hamtaelewa hili hadi siku mtakapofunguka macho na kukimbia kuabudu hiyo dini. Mungu awasaidie.
Wakati Katoliki inaandaa biblia, ilijua yote hayo unayoshikia bango. Nakushauri ukaungane na waamini wenzio kutafuta biblia yenu mpya kisha uje na hoja zako.
Pia kama hauna heshima kwa mwili hauwezi kuwa na roho yenye heshima. Mwili hubeba roho na nafsi. Hivyo wakati wa kutamatisha safari ya mwanadamu, kilichohifadhi roho na nafsi nacho kipewe heshima
 
SWALI: je? ni kweli au sio kweli, kwamba huwa mnamwomba Mungu amsamehe marehemu.

SWALI: Je? ni kweli au sio kweli Biblia Wagalatia 6:5 inasema kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe na Warumi 14:12 inasema Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.
1. Ni kweli kabisa Wakatoliki tunamuomba Mungu maombi mbalimbali, sio kuhusu marehemu tu, bali kuhusu afya, uhai, baraka na mambo mengine kwani tunaamini Mungu ndiye mweza wa yote na hayo tunayomuomba atayafanya kadiri ya mapenzi yake
Mathayo 26:39, “Baba yangu, kama inawezekana kikombe hiki kiniepuke, lakini sasa kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.” Kristu anatufundisha tusiache kuomba, lakini tukisha kuomba tuache Mungu atende kadiri ya mapenzi yake. Yeye mwenyewe aliomba aepuke mateso yale pamoja na kuwa ilikuwa imeandikwa tayari zamani katika unabii kuwa atateswa. Je, wataka kusema kwamba hata Kristu alikosea kuomba jambo ambalo limeshaandikwa na manabii? Kwa Wakatoliki tunaomba kila tunaloona jema huku tukiamini Mungu ni mwema na natatenda kadiri apendavyo, sio kwa kadiri ya mawazo ya wanadamu

2. Kuhusu "Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe", ninakuwekea sura nzima ya Sita ili uisome katika maudhui na sio katika kunyofoa mstari mmoja (na hapa ndipo niliposema kwamba Wakatoliki wanathamini sana elimu, maana nje ya elimu ni upotovu na upotoshaji). Baada ya kuisoma na kutafuta mtu mwenye maarifa akufafanulie, utagundua kwamba ulipotoshwa (na wachungaji wako, mitume na manabii wako), na wewe unafanya yaleyale, unapotosha wengine (kondoo zako)

6 Ndugu zangu, mkimwona mtu amenaswa katika dhambi fulani, basi ninyi mnaoongozwa na Roho, mrejesheni mtu huyo kwa upole. Lakini mjihadhari, ili na ninyi msije mkajaribiwa. 2 Chukulianeni mizigo yenu; na kwa njia hiyo mtaweza kutimiza sheria ya Kristo. 3 Mtu akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe siyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe. 4 Lakini, kila mtu apime mwenendo wake, ndipo anaweza kuwa na sababu ya kujisifu bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. 5 Kwa maana, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe. 6 Basi, mwanafunzi na amshirikishe mwalimu wake vitu vyote vilivyo vyema.
 
Back
Top Bottom