Kwamba wewe peke yako document umeielewa kuliko baraza la maaskofu Malawi, Kenya, Nigeria, Poland n.k ?
View attachment 2850412View attachment 2850413View attachment 2850414
1. Sasa ndiyo kusema nini mbona hueleweki?
2. Yesu aliletewa yule mama alikamatwa akizini na kwa Sheria ya Kiyahudi ilikuwa apigwe mawe hadi kufa. Akaulizwa yeye anasemaje? Yesu akawaambia: "asiye na dhambi kati yenu awe wa kwanza kumtupia jiwe." Walipojitafakari wakaacha mawe yao wakaondoka. Yesu akabaki na yule mwanamke. Akamuuliza, "wako wapi washtaki wako?" Yeye akasema "wameshaondoka". Yesu akamjibu "na mimi sikuhukumu, nenda zako, ila kuanzia sasa usitende dhambi tena." Je, Yesu alipenda kuzini kwa huyo mwanake?
3. Hapo juu umeonyesha Papa akiwa kwenye wheelchair na watu wanampa mkono. Je, aliuliza au aliomba watu wa jinsia moja waje wampe mkono? Wewe ukiwa kwenye kundi la watu ukasalimiana nao na mmoja ni mwizi, wengine walawiti, majangiri, wauaji, etc na je na wewe utakuwa umebariki uovu wao kwa kusalimiana nao?
4. Pia umeonyesha kiongozi mmoja akionyesha ishara kama ya kuwabariki watu wawili. Niulize hivi. Kama wewe ni muumini ukienda kanisani na kanisani kuna watu mbalimbali na huenda baadhi ya walio kanisani wanashiriki uhalifu mbalimbali (wengine ni wezi, walawiti, magaidi, wauaji), je mchungaji akiwaombea huwa anaomba waendelee kufanya uovu wao au ili Mungu awasaidie wamjue zaidi na kumgeukia? Ukimwombea mwizi ina maana unataka aendelee kuiba? Kuna watu wanaenda gerezani kuwaombea wafungwa na wamefungwa kwa makosa mbalimbali pia. Je, huwa wanaombewa waendelee kuwa wahalifu? Mara ngapi watu huwa wanatoa ushuhuda baada ya kuombewa kwamba walikuwa wezi, majangili, wauaji etc? Je, vibaya watu kuombewa na kubadilika kuwa watu wema? Ndiyo dini au aina ya imani mnayoihubiri hiyo?
5. Ukiitisha mkutano na wakaja watu mbalimbali - wengine wezi, majangili, wauaji, walawiti - ukaongea na na mkakubaliana mjenge kisima na fedha zikachangwa na kisima kikajengwa watu wakapata maji ya kunywa, je hayo maji yatakuwa na chembechembe za wizi, ujangili, uuaji, kulawiti etc kwa vile baadhi ya waliochangia ni wahalifu?
5. Kwa hiyo, hapa ndipo kuna missing point. Unataka watu wasiombewe ili wabadilike? Wewe ulishaombewa ili uendelee kufanya aina ya dhambi ambayo ulishawahi kutenda au uendelee na udhaifu wako ulionao? Je, kumbe hata kukitokea majanga viongozi wa dini wakaitwa waimbee nchi huwa ni kuomba hayo majanga yaendelee kuleta madhara kwa wananchi au ili Mwenyezi Mungu ayaondoshe? Kwa shoga je? Tukimwombea ni kutaka aendelee na ushoga au Mwenyezi Mungu ampe neema ya kujitambua zaidi na kufanya mapenzi yake? Hivi ni kweli kabisa Mungu hataki mashoga waombewe ili wabadilike isipokuwa wakosefu wengine tu ndiyo waombewe? Na pale Yesu aliposema "sikuja kuwatafuta wenye haki, bali wenye dhambi ili wapate kutubu" alikuwa na maana gani, kwama hao wenye dhambi hawatakiwi waombewe ili wabadilike?
6. Binafsi naona ni aina ya reasoning ambayo ni "retrogressive" ambayo ni proper to unthinking intelligence.