Suala kubwa hapa ni vyanzo vya maji kwa mji mkubwa kama DSM. Tangu enzi za mwalimu kulikuwa na mipango ya kujenga bwawa la maji huko Kidunda, lakin mpaka leo imekuwa ndoto.Magufuli amewahi kutudokeza kuwa kuna watu walikuwa wabafungulia maji kwenye mabwawa ya kuzalishia umeme ili maji yapungue kisha tushindwe kuzalisha umeme ili Wauze Majenerta yao!
Hii ishu ya maji haikubaliki, Watu mpaka wananuka, maji ya kuoga hakuna!
Kwa jiji kubwa kama DSM kutegemea kuchota maji mtoni bila kuwa bwawa la kuhifadhi ni kichekesho na udhaifu mkubwa kwa chama kilichiko madarakani tangu uhuru.
Kwa hali ya upungufu wa mvua za vuli na kutokuwepo kwa bwawa la kuhufadhia maji, uhaba wa maji hauepukiki. Swali ni je viongozi wetu wana la kujifunza au ni kukaa na kupanga namna ya kubaki madarakani?