KERO Wakazi wa Kimara na kata zake hawana maji zaidi ya wiki sasa, DAWASA hamuelezi maji yatatoka lini!
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
3,359
Reaction score
6,568
Uongozi wa mamlaka ya maji safi jijini Dar-es-salaam hautoi taarifa ni lini huduma ya maji safi itarejea Kimara na kata zake zote kwa ujumla.

Wanawake na watoto wanasumbuka kutembea umbali mrefu kusaka maji bila ya mafanikio.

Tunaitaka mamlaka ya maji Dar-es-salaam (DAWASA) kutuelezea ni lini maji yatarejea!
 
Walisema bomba la Ruvu juu limepasuka wanatengeneza
 
Habari JamiiForums, tuna weeks mbili au tatu hatuna maji Kimara mkoa wa Dar es salaam. DAWASA walipita tarehe 12.12.2024 hawana point yoyote kutupa matumaini.
 
Wakazi wa Kimara Temboni wilayani Ubungo,hawana maji kwa karibu majuma matatu ,na sasa tatizo hilo la maji limegeuka fursa kwa bodaboda ambao wamekuwa wakitafuta maji na kuuza kwa shilingi 1000 kwa dumu lenye ujazo wa lita 20,huku wenye visima vya maji chumvi nao wakipandisha bei toka shilingi 100 kwa ndoo hadi 300.
Mamlaka husika haijatoa ufafanuzi wa chanzo cha ukosefu huo wa maji na lini utafika kikomo.Tunaomba Jamii Forums mtusaidie kupaza sauti ili tuondokane na kero hii.
 
Back
Top Bottom