Wakazi wa Kimara Temboni wilayani Ubungo,hawana maji kwa karibu majuma matatu ,na sasa tatizo hilo la maji limegeuka fursa kwa bodaboda ambao wamekuwa wakitafuta maji na kuuza kwa shilingi 1000 kwa dumu lenye ujazo wa lita 20,huku wenye visima vya maji chumvi nao wakipandisha bei toka shilingi 100 kwa ndoo hadi 300.
Mamlaka husika haijatoa ufafanuzi wa chanzo cha ukosefu huo wa maji na lini utafika kikomo.Tunaomba Jamii Forums mtusaidie kupaza sauti ili tuondokane na kero hii.