Wakazi wa Magamba Songwe wachoma mazao yao ya ufuta mashambani mwao kupinga agizo la Mkuu wa Wilaya ya kutaka wauze kwa mfumo wa stakabadhi ghalani

Soko ndio linapanga auzeje na serikali itasimamia mapato yake yahayohusika tu kutoka kwa mnunuzi,mkulima atadeal na Chama chake cha Ushirika,upo?

Mkuu lini mmemsaidia mkulima wa nchi hii? Price topup kwenye biashara unafahamu ni kitu gani? Kwa nini mbolea ni tatizo au inapelekwa msimu wa kilimo ukiwa umeisha?
 
Soko ndio linapanga auzeje na serikali itasimamia mapato yake yahayohusika tu kutoka kwa mnunuzi,mkulima atadeal na Chama chake cha Ushirika,upo?
Nimelima mwenyewe kwenye kuuza ndio mnisimamie? Acheni niuze ninapopataka nikidhulumiwa polisi na mahakama zipo
 
Hivi wale maafisa ushirika vile vitambi vikubwa sio ndio dhulma ya pesa za wakulima kweli maana wanamitumbo kama mapulizo
Kumbeeeee,nishaelewa,njaa mbaya sana,kwani hao ndio wanapanga bei za mazao ya wakulima au soko ndio linaamua?
 
Nimelima mwenyewe kwenye kuuza ndio mnisimamie? Acheni niuze ninapopataka nikidhulumiwa polisi na mahakama zipo
Hakuna nchi ya hivyo duniani,ukitaka hivyo anzisha dunia yako mwenyewe utakayojipngia utakavyo
 
Anaelima ndiye auze anapopataka. Samahani kama nakukwazwa mkuu wa wilaya

Usiombe msamaha hauna kosa, hawa watu wana sera za kipuuzi utaona wanakimbilia kushuka soko la dunia hawajui hata blackmarkets za mazao hayohayo zikoje na wafanyeje mazao ya nchi zao yawe ranked kwenye ubora mzuri wa kidunia wako wanazurura tu hadi mtu unawaonea huruma
 
Kumbeeeee,nishaelewa,njaa mbaya sana,kwani hao ndio wanapanga bei za mazao ya wakulima au soko ndio linaamua?

Wewe mbona hauelewi ? Unahisi kati ya mimi na wewe nani mwenye njaa? Wewe kama ni DC au DED basi tunabahati mbaya kua na watu wa aina yako kwenye uongozi
 
Usiombe msamaha hauna kosa, hawa watu wana sera za kipuuzi utaona wanakimbilia kushuka soko la dunia hawajui hata blackmarkets za mazao hayohayo zikoje na wafanyeje mazao ya nchi zao yawe ranked kwenye ubora mzuri wa kidunia wako wanazurura tu hadi mtu unawaonea huruma
Black markets si ndio hizo mnazopenda za kulanguliwa na walanguzi wakati serikali inaweka mifumo mnaipinga badala ya kuiboresha mnabakia kulalamika lalamika tu,inabidi muonewe huruma tu
 
Wewe mbona hauelewi ? Unahisi kati ya mimi na wewe nani mwenye njaa? Wewe kama ni DC au DED basi tunabahati mbaya kua na watu wa aina yako kwenye uongozi
Mimi ni mkulima mzuri sana nayefaidika na huo mfumo kwani msimu uliopita nimepata kipato ambacho sijawahi kukipata tokea niwe mkulima na msimu huu natoboa kabisa kupitia mfumo huu bora kabisa ulioletwa na serikali
 
DC ahakikishe elimu imewafikia kwanza kabla ya kutoa matamko na maagizo ambayo yataonekana hayana maana kwa wananchi...
 
Mimi ni mkulima mzuri sana nayefaidika na huo mfumo kwani msimu uliopita nimepata kipato ambacho sijawahi kukipata tokea niwe mkulima na msimu huu natoboa kabisa kupitia mfumo huu bora kabisa ulioletwa na serikali
Unajua shida hapo ni elimu haijawafikia, wao wamezoea kuuza na kupata hela papo kwa papo au wakat mwengne kufuatwa kabisa vijijini na walanguzi sasa unapowaletea kitu kipya lazima taharuki itokee ni vitu vya kawaida... Anachotakiwa DC, DeD na wataalam wao wahakikishe elimu imewafikia vilivyo kwanza kabla ya mfumo kuanza
 
Katika kuboresha hili ni muhimu sana kufanywa na viongozi wetu,kwani hata sisi mwanzoni baadhi ya wakulima wenzangu waliingiza mazao machache yauzwe katika mfumo huu kwa kudhani watapigwa pia walanguzi walikuwa wanatutisha kuwa hatutalipwa pesa zetu,baadae walivyoona tunalipwa fresh nao wakaunga tela kwa spidi zote,kwa hiyo elimu ni muhimu sana mkuu
 
Yes, ila tatizo la walanguzi bado linabaki kuwa sugu maana kimsingi huu mfumo ni kwa ajili ya mkulima kumnyanyua mkulima sasa baadhi ya walanguzi nao wamejipenyeza kwenyw vyama vya msingi... Na baadhi ya wakulima wameendelea kuwauzia walanguzi ila ndio shida zetu wakati mwngne wanabanwa so huwezi kuwalaumu moja kwa moja... All in all huu mfumo ni mzuri sana
 
Upo sahihi sana mkuu
 
Kilimo kinaumiza sana, kila nikifikiria hasara ambayo nimekua nikipata kila mwaka
 
Jambo la msingi ni kukaa mezani na kukubaliana nini kufanyika. Huu ubabe ndiyo umesababisha tumebaki masikini licha ya ardhi tuliyonayo.
Hivi hiyo Amri Ni ya mkuu wa wilaya au Ni ya wizara ya Kilimo? Hainiingii akilini (ingawa yawezekana kuwa na faida) kwamba mkuu wa wilaya kaamka kaanza kushurutisha wakulima watumie mfumo huo.
 
Duh wametumia hasira sana, wasingechoma wangetunza tu home Hadi pale malalamiko yao yakifanyiwa kazi. Wamehangaika kupanda, palizi kuvuna wanachoma😒😒
 
Back
Top Bottom