Wakazi wa Mbezi wanaumia sana wakikumbuka ahadi ya Hayati Magufuli

Wakazi wa Mbezi wanaumia sana wakikumbuka ahadi ya Hayati Magufuli

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Siku Hayati John Pombe Joseph Magufuli anazindua Stand kuu ya Mabasi iliyopo Mbezi Louis katika mambo aliyowaahidi wakazi wa Mbezi na Kibamba ni pamoja na Kujenga barabara za Mpiji na Makabe kwa kiwango cha lami.

Siku hiyo aliongea kwa kumaanisha kuwa utekelezaji wake ungeanza mapema tu. Nadhani baada ya ziara hiyo alielekea Ubungo kufungua Flyover (Interchange) na hazikupita siku nyingi akamaliza Mwendo wake ktk Dunia hii.

Ninachoamini ni kwamba angekuwepo ni dhahiri suala la ujenzi wa Barabara hizo ungeshaanza leo hii. Ninamini hivi kwasababu JPM ALIKUWA AKIAHIDI JAMBO LAZIMA AHAKIKISHE LINAFANYIKA.

HAKIKA WAKAZI WA MBEZI NA KIBAMBA WANAKUKUMBUKA SANA IKIWA NI PAMOJA NA KUWALETEA STAND YA KIMATAIFA.

HATA HIVYO MAMA YETU NI MSIKIVU NINAAMINI ATAFANYA JAMBO KAMA TUNAVYOONA ANAVYOIJENGA NCHI
 
Sehemu nyingi tu wanaamini angekuwa hai mambo yakekuwa mbali sana.

Kuna maeneo yalishawekewa hadi mabomba ya maji ila maji hayataki yakiwemo maeneo ya kigamboni, makabe, Goba na Msakuzi.

Hiyo barabara Mbunge wa Kibamba anaililia kila siku.
 
Njia ya makabe naskia lilitengwa fungu kabisa la kujenga kilomita kama 7. Baadae wakahamisha fungu kwingine walichokifanya makabe wakatengeneza kipande cha mita 300 kwa kiwango cha lami uchwara.

Maji maeneo ya makabe, msakuzi kwa liperanya, msumi wamesambaza mabomba sasa inaelekea miaka miwili ila maji hayatoki hadi leo.
 
Kuna barabra ya kutoka Mbezi kwenda Makabe, barabara hii liliwekwa bango itajengwa km 1 lami lakini kilichofanywa na aibu kwa TARURA Ubungo! hata mita 500 haifiki! Mitaro ni aibu!

Imekuwa na nyufa na walikuja kuweka kiraka mwezi uliopita! Tunaomba TAKUKURU na wizara husika kutembelea eneo hilo na kuona uhujumu uchumi uliofanywa na TRURA Ubungo na kuchukua hatua.

Kuna taarifa mwenye kamupuni ya ujenzi huo ni staff wa tarura Ubungo akimtumia ndugu yake.
 
Kuna barabra ya kutoka Mbezi kwenda Makabe, barabara hii liliwekwa bango itajengwa km 1 lami lakini kilichofanywa na aibu kwa TARURA Ubungo! hata mita 500 haifiki! Mitaro ni aibu! Imekuwa na nyufa na walikuja kuweka kiraka mwezi uliopita! Tunaomba TAKUKURU na wizara husika kutembelea eneo hilo na kuona uhujumu uchumi uliofanywa na TRURA Ubungo na kuchukua hatua. Kuna taarifa mwenye kamupuni ya ujenzi huo ni staff wa tarura Ubungo akimtumia ndugu yake.
Sahihi kabisa ndio maana mimi nimeandika hapo juu lami uchwara. Na ni kwanini imeishia pale darajani why wasingemalizia na kipande cha juu kupandisha walau hata kile kimlima mpk pale st.Anns shule atleast.
 
Huu ni muda wa kulamba asali kwa urefu wa kamba...muda wa maendeleo ushapita, na aliepata kapata aliekosa kakosa...poleni sana bandugu.
IMG-20220707-WA0034.jpg
 
Hahahahahahahah
Kifupi waridhike na walichopata...Mengineyo ni Majaaaliwa just incase.
U Cant have both, u need to choose.
Hata ktk level ya familia, unataka ule vzuri au ujenge nyumba nzuri na ktk hayo mawili kipi kianze.
Ss mwenye sera ya nyumba nzuri ashatungulia, now tupo kwenye sera ya tuvae vzuri, tunukie vzuri, mamisosi ya mboga 7 na mapochopocho manjali, chai ya asali na mkate wa blueband na jam, matunda, ma soseji na pesa ya bia mfukoni ili hali tupo kwenye nyumba imestuck kwenye finishing. Kikubwa tuishi sasa, maisha ndo haya haya aka kazi na bata, future kila mtu atajijua.
 
Si kweli, Wakazi wa Mbezi tuna uchungu na alicho kifanya huyo jamaa kwa kubomoa nyumba zetu huku kukiwa na zuio la mahakama, na kutupotezea mali nyingi ukiacha nyumba na viwanja tulivyopoteza

Sema tulifurahi tuliposikia amekufa, maana asingeweza kufanyia wengine tena hivyo na atapata malipo yake huko alipoenda
 
Noop,kila mwanadamu anamapungufu,katiba bora inakwamisha ama kuzuia kwa kiasi kikubwa hayo,ayo mauthubutu na maono aliyepita mnasema alikua nayo ila kulichotokea alipitia njia mbaya kufika huko,watu waliuawa,kupotea,exiled na kufungwa kwa kesi zisizo zao, unadhani hii ndio njia pkee?

Aje uyo mwenye maono na uthubutu plus katiba bora.

Issue sio katiba mpya tu...tunataka watu wenye vipaji vya kuongoza, wenye maono na udhubutu..katiba mpya kwa TZ ni km Barcelona bila Messi...just a mediocre club.
 
Ccm ni wale wale, ndio maana tunahitaji taasisi imara, anapokufa au kuondolewa political head haiathiri utekelezaji wa majukumu, wakazi wa maeneo hayo wangekua na uwezo wa kufungua kesi ya madai kwenye mahakama y kikatiba
 
Sehemu nyingi tu wanaamini angekuwa hai mambo yakekuwa mbali sana.

Kuna maeneo yalishawekewa hadi mabomba ya maji ila maji hayataki yakiwemo maeneo ya kigamboni, makabe, Goba na Msakuzi.

Hiyo barabara Mbunge wa Kibamba anaililia kila siku.
Kwa hiyo wateule wake wote aliteua kwa umakini mkubwa walikuwa famba? Wabunge wake wa CCM aliowajaza Bungeni kwa mtutu nao ni utopolo mtupu?
 
Well said mkuu, nchi kubwa hii haiwezi endeshwa na mtu ila mfumo imara(katiba)
Ccm ni wale wale, ndio maana tunahitaji taasisi imara, anapokufa au kuondolewa political head haiathiri utekelezaji wa majukumu, wakazi wa maeneo hayo wangekua na uwezo wa kufungua kesi ya madai kwenye mahakama y kikatiba
 
Back
Top Bottom