Wakazi wa Mbezi wanaumia sana wakikumbuka ahadi ya Hayati Magufuli

Wakazi wa Mbezi wanaumia sana wakikumbuka ahadi ya Hayati Magufuli

Njia ya makabe naskia lilitengwa fungu kabisa la kujenga kilomita kama 7. Baadae wakahamisha fungu kwingine walichokifanya makabe wakatengeneza kipande korofi cha km 1 kwa kiwango cha lami uchwara.

Maji maeneo ya makabe, msakuzi kwa kiperanya, msumi wamesambaza mabomba sasa inaelekea miaka miwili ila maji hayatoki hadi leo.
Tatizo watendaji sasahivi sio waoga kabisa. Na hawa ndio wanaomharibia Mama. Natamani Mama awe Mkali kwasababu nature ya mtu mweusi akiona hakuna FIMBO nyuma yake anafanya ujinga atakavyo.
JPM alikuwa na mapungufu yake lakini ktk mazuri aliyokuwa nayo ni pamoja na kujenga nidhamu kwa watendaji wa serikali. TUANGALIE TU JINSI BARABARA YA GOBA ILIVYOJENGWA KWA VIWANGO NI KWASABABU WATU WALIOGOPA KULETA UJANJAUJANJA
 
Vipi mkuu wakazi wa Tarime waliozuiliwa kutumia pesa zilizotolewa na mgodi eti kisa mbunge ni wa CHADEMA
 
Njia ya makabe naskia lilitengwa fungu kabisa la kujenga kilomita kama 7. Baadae wakahamisha fungu kwingine walichokifanya makabe wakatengeneza kipande korofi cha km 1 kwa kiwango cha lami uchwara.

Maji maeneo ya makabe, msakuzi kwa kiperanya, msumi wamesambaza mabomba sasa inaelekea miaka miwili ila maji hayatoki hadi leo.
Hilo la maji nitalifikisha sehemu husika
 
Kuna maeneo yalishawekewa hadi mabomba ya maji ila maji hayataki yakiwemo maeneo ya kigamboni, makabe, Goba na Msakuzi.
Siyo kuwekewa mabomba tu mkuu mimi ni mkazi wa Mbezi Makabe nilifunga bomba August mwaka jana kwa gharama kubwa maji yakatoka mfululizo wiki tatu mara yakaingia kwenye mgao kwa wiki mara moja sasa yana miezi miwili hayajatoka.

Ajabu kuanzia police post kurudi madukani maji yanatoka ila kuna namna engineers wa Dawasa wamefanya wanapokea rushwa kutoka kwa wauza maji wa magari ili wasifungue maji area fulani wao watuuzie na ikikaribia tarehe za kusoma Mita wanafungua maji kote usiku wa saa tisa mpaka saa 12 asubuhi wanafunga kesho yake wanapita kusoma metre na kutuma bill kwa wateja.
 
Si kweli, Wakazi wa Mbezi tuna uchungu na alicho kifanya huyo jamaa kwa kubomoa nyumba zetu huku kukiwa na zuio la mahakama, na kutupotezea mali nyingi ukiacha nyumba na viwanja tulivyopoteza

Sema tulifurahi tuliposikia amekufa, maana asingeweza kufanyia wengine tena hivyo na atapata malipo yake huko alipoenda
Ila anaelipisha watu tozo za kinyonyaji ambazo hazina kichwa wala miguu ndio mtu?
 
Siku Hayati John Pombe Joseph Magufuli anazindua Stand kuu ya Mabasi iliyopo Mbezi Louis katika mambo aliyowaahidi wakazi wa Mbezi na Kibamba ni pamoja na Kujenga barabara za Mpiji na Makabe kwa kiwango cha lami.

Siku hiyo aliongea kwa kumaanisha kuwa utekelezaji wake ungeanza mapema tu. Nadhani baada ya ziara hiyo alielekea Ubungo kufungua Flyover (Interchange) na hazikupita siku nyingi akamaliza Mwendo wake ktk Dunia hii.

Ninachoamini ni kwamba angekuwepo ni dhahiri suala la ujenzi wa Barabara hizo ungeshaanza leo hii. Ninamini hivi kwasababu JPM ALIKUWA AKIAHIDI JAMBO LAZIMA AHAKIKISHE LINAFANYIKA.

HAKIKA WAKAZI WA MBEZI NA KIBAMBA WANAKUKUMBUKA SANA IKIWA NI PAMOJA NA KUWALETEA STAND YA KIMATAIFA.

HATA HIVYO MAMA YETU NI MSIKIVU NINAAMINI ATAFANYA JAMBO KAMA TUNAVYOONA ANAVYOIJENGA NCHI
Sasa hivi dar hakuna barabara mpya inayojengwa hata kilometa 1 toka sa100 kachukua nchi ..uwezi hata kuwaona trc wakirekebisha reli ndiyo maana majuzi treni imeanguka na kuua watu
 
Kweli waweke lami barabara hiyo tena iende mpaka msakuzi sijui kwa ribaba
Ila kwa lipe pale watu wajiandae kubomolewa kupisha barabara

Ova
 
Kuna barabra ya kutoka Mbezi kwenda Makabe, barabara hii liliwekwa bango itajengwa km 1 lami lakini kilichofanywa na aibu kwa TARURA Ubungo! hata mita 500 haifiki! Mitaro ni aibu!

Imekuwa na nyufa na walikuja kuweka kiraka mwezi uliopita! Tunaomba TAKUKURU na wizara husika kutembelea eneo hilo na kuona uhujumu uchumi uliofanywa na TRURA Ubungo na kuchukua hatua.

Kuna taarifa mwenye kamupuni ya ujenzi huo ni staff wa tarura Ubungo akimtumia ndugu yake.
Tatizo la hii nchi Kuna wataalamu na wachumia tumbo, au tuite Wala rushwa ijapokuwa amesomea kazi husika
 
Na sisi tunataka lami ya kutokea wazo bwawani,kuja hadi msigani [emoji1] itoke mpk scout

Ova
 
Siku Hayati John Pombe Joseph Magufuli anazindua Stand kuu ya Mabasi iliyopo Mbezi Louis katika mambo aliyowaahidi wakazi wa Mbezi na Kibamba ni pamoja na Kujenga barabara za Mpiji na Makabe kwa kiwango cha lami.

Siku hiyo aliongea kwa kumaanisha kuwa utekelezaji wake ungeanza mapema tu. Nadhani baada ya ziara hiyo alielekea Ubungo kufungua Flyover (Interchange) na hazikupita siku nyingi akamaliza Mwendo wake ktk Dunia hii.

Ninachoamini ni kwamba angekuwepo ni dhahiri suala la ujenzi wa Barabara hizo ungeshaanza leo hii. Ninamini hivi kwasababu JPM ALIKUWA AKIAHIDI JAMBO LAZIMA AHAKIKISHE LINAFANYIKA.

HAKIKA WAKAZI WA MBEZI NA KIBAMBA WANAKUKUMBUKA SANA IKIWA NI PAMOJA NA KUWALETEA STAND YA KIMATAIFA.

HATA HIVYO MAMA YETU NI MSIKIVU NINAAMINI ATAFANYA JAMBO KAMA TUNAVYOONA ANAVYOIJENGA NCHI
Na wa kimara pia aliowabomolea watamkumbuka
 
Back
Top Bottom