Wakazi wa Mbezi wanaumia sana wakikumbuka ahadi ya Hayati Magufuli

So sad huko wachina wanashinda wanavuta fegi na kula kitimoto tu

USSR
Uongo . Kila mradi una kipindi chake cha kuanza na kuisha . Kwani alipokuwepo huyo chizi magufuli wachina walikuwa hawavuti fegi?
 
Siku Hayati John Pombe Joseph Magufuli anazindua Stand kuu ya Mabasi iliyopo Mbezi Louis katika mambo aliyowaahidi wakazi wa Mbezi na Kibamba ni pamoja na Kujenga barabara za Mpiji na Makabe kwa kiwango cha lami.

Siku hiyo aliongea kwa kumaanisha kuwa utekelezaji wake ungeanza mapema tu. Nadhani baada ya ziara hiyo alielekea Ubungo kufungua Flyover (Interchange) na hazikupita siku nyingi akamaliza Mwendo wake ktk Dunia hii.

Ninachoamini ni kwamba angekuwepo ni dhahiri suala la ujenzi wa Barabara hizo ungeshaanza leo hii. Ninamini hivi kwasababu JPM ALIKUWA AKIAHIDI JAMBO LAZIMA AHAKIKISHE LINAFANYIKA.

HAKIKA WAKAZI WA MBEZI NA KIBAMBA WANAKUKUMBUKA SANA IKIWA NI PAMOJA NA KUWALETEA STAND YA KIMATAIFA.

HATA HIVYO MAMA YETU NI MSIKIVU NINAAMINI ATAFANYA JAMBO KAMA TUNAVYOONA ANAVYOIJENGA NCHI
Fedha zake zimetumika kuwahamisha wamasai
 
Kwa kweli JPM tutamkumbuka sana.Alikuwa akisema kitu kinatekelezwa.Siyo kama awamu hii ya kila siku kusafiri nje.yaani unasafiri kwenda kukopa pesa na unazimaliza tena kwa safari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Rais hawezi fanya Kila kitu, hao wabunge 100% ni CCM na Halmashauri zote za hapa Dar zipo chini ya CCM ambao karibu wote waliingia kwa endorsement ya JPM.

Sasa basi..... Ni legacy Gani aliyoacha magufuli kama viongozi wote aliowapitisha wanashindwa kutekeleza ahadi za CCM kwa wananchi?

Nasema hivi Mama Samia awanyime barabara Ili akili ziwakae vizuri next time mchague wabunge na madiwani wenye uzalendo sio wapiga makofi tu.
 
Raisi akisema kitu kinatekelezwa kwa haraka kuliko mbunge kutokana na katiba yetu ilivyo.wabunge waliowahi kutawala huko(kibamba)walishayaongelea sana haya matatizo ya barabara,maji pamoja na huduma zingine.Kipindi cha ufunguzi wa hiyo stendi ya magufuli,rais alielekeza(Magufuli)utekelezaji wa miradi ya barabara,umeme na maji na utekelezaji ulianza siku chache baada ya yeye kusema.Alipofariki tu na utekelezaji ukasitisha.Mbunge hapo hana kosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakandarasi hata aibu hawaoni,kile kipande kutoka stend hadi njia kuu ya kuanza safari ya morogoro road ni mwaka hakijakamilika na mara kwa mara kinasawazishwa kinashindiliwa halafu kinatumika kinaharibika tena.ONENI AIBU KUTOKAMILISHA KAZI.
 
Siku Hayati John Pombe Joseph Magufuli anazindua Stand kuu ya Mabasi iliyopo Mbezi Louis katika mambo aliyowaahidi wakazi wa Mbezi na Kibamba ni pamoja na Kujenga barabara za Mpiji na Makabe kwa kiwango cha lami.

Siku hiyo aliongea kwa kumaanisha kuwa utekelezaji wake ungeanza mapema tu. Nadhani baada ya ziara hiyo alielekea Ubungo kufungua Flyover (Interchange) na hazikupita siku nyingi akamaliza Mwendo wake ktk Dunia hii.

Ninachoamini ni kwamba angekuwepo ni dhahiri suala la ujenzi wa Barabara hizo ungeshaanza leo hii. Ninamini hivi kwasababu JPM ALIKUWA AKIAHIDI JAMBO LAZIMA AHAKIKISHE LINAFANYIKA.

HAKIKA WAKAZI WA MBEZI NA KIBAMBA WANAKUKUMBUKA SANA IKIWA NI PAMOJA NA KUWALETEA STAND YA KIMATAIFA.

HATA HIVYO MAMA YETU NI MSIKIVU NINAAMINI ATAFANYA JAMBO KAMA TUNAVYOONA ANAVYOIJENGA NCHI
Aliahidi vitu viwili lami na maji
 
Rais hawezi fanya Kila kitu, hao wabunge 100% ni CCM na Halmashauri zote za hapa Dar zipo chini ya CCM ambao karibu wote waliingia kwa endorsement ya JPM.

Sasa basi..... Ni legacy Gani aliyoacha magufuli kama viongozi wote aliowapitisha wanashindwa kutekeleza ahadi za CCM kwa wananchi?

Nasema hivi Mama Samia awanyime barabara Ili akili ziwakae vizuri next time mchague wabunge na madiwani wenye uzalendo sio wapiga makofi tu.
Mara nyingi kukimbia hutegemea anayekukimbiza. Leo hii jaffo wa samia sio yule jaffo wa magufuli, ummy wa samia sio yule ummy wa magufuli wizara ya ardhi ya samia sio ile ya magufuli, hata miradi ya samia sio ile ya magufuli kwa kiwango na spidi.
 
Nakumbuka alisema barabara ya kutokea kisarawe kupitia kifuru hadi mbezi peaa ishatengwa,na amsha amsha zilishaanza,hadi leo kimyaa!
 
Sehemu nyingi tu wanaamini angekuwa hai mambo yakekuwa mbali sana.

Kuna maeneo yalishawekewa hadi mabomba ya maji ila maji hayataki yakiwemo maeneo ya kigamboni, makabe, Goba na Msakuzi.

Hiyo barabara Mbunge wa Kibamba anaililia kila siku.
Wewe umemuona wapi akiililia?Barabara ya Msakuzi kwasababu ya Wingi wa Magari Tanroads wakikarabati wiki mbili inaharibika si bora hayo Mamilioni waanze na Lami kidogokidogo,hii akili nayo hadi waelekezwe na Rais?
 
Shida ninayoiona ipo kwa watendaji wa chini. Ni wababaishaji sana . Sijui kwanini huwa hawatekelezi jambo hadi kuwe na Pressure fulani. Yaani leo hii Mheshimiwa Rais akiwaambia " mnaonaje barabara ikijengwa" utakuta haooo wanaanza utekelezaji. NAJIULIZA NI KWANINI HADI MH RAIS AAGIZE!!

Pia sielewi Waziri Mwenye dhamana ya Barabara anachofanya

Kuhusu Mbunge wa Kibamba Mh Mtemvu kwa kweli kijana wa watu anajitahidi sana. Hata huko Bungeni tunamuona anavyopambana.

Barabara za Mpiji na Msakuzi kutokuwekwa Lami muda mrefu ni suala linalosikitisha sana. Barabara hizo zilistahili kuwekwa lami muda mrefu
 
Wewe umemuona wapi akiililia?Barabara ya Msakuzi kwasababu ya Wingi wa Magari Tanroads wakikarabati wiki mbili inaharibika si bora hayo Mamilioni waanze na Lami kidogokidogo,hii akili nayo hadi waelekezwe na Rais?
Amelia bungeni na kwenye vikao.
 
Ndio maana tunahitaji mfumo na si mtu awe anaamua kufanya anavyojisikia, sasa kafa twalia lia
KATIBA Mpya muhimu sana
Hivi kichwani kuko sawa kweli. Mfumo unakuwa hauna msimamizi unajiendesha wenyewe.

Lengo lako useme Katiba Mpya.
Hivi sasa huvi Katiba iliyopo haikiukwi?

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom