Wakazi wa Mbezi wanaumia sana wakikumbuka ahadi ya Hayati Magufuli

Wakazi wa Mbezi wanaumia sana wakikumbuka ahadi ya Hayati Magufuli

Ha haa! Ningepewa wizara ya ujenzi, 'ndani ya wiki moja', bara bara zote zingekuwa na lami. 😎
Nina uwezo (technical know how) wa kujenga km 1, ya lami kwa gharama isiyozidi Tsh mil 120! If u can imagine...
With an annual budget of 200B, kila mkoa ungeweza kupata km 64 za lami kwa mwaka and within 5 yes kila mkoa ungepata km 300 za lami...
 
Neno rahisi tunalo weza kusema ni apumzike kwa amani [emoji24][emoji24]
Jisemehe wewe na nafasi yako. Ungejua walichopitia wakazi wa kimara, ndiyo maana alipokufa kuna watu walifanya sherehe kabisa. Sasa nimejua kwanini mpaka Idd Amin alikuwa na wafuasi
 
Sukuma gang mtapata tabu sana. Wananchi walimshukuru Mungu kwa kuwaondolea bwana yule
 
Hivi kichwani kuko sawa kweli. Mfumo unakuwa hauna msimamizi unajiendesha wenyewe.

Lengo lako useme Katiba Mpya.
Hivi sasa huvi Katiba iliyopo haikiukwi?

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
🤣🤣🤣 Says the man who doesnt know even to write properly, jifunze kuandika vyema hasa alama za uandishi kama (, . ? )nk kisha njoo tena tujadili pa1.
 
Nchi yetu ilivyo itakapoanza kukaribia mwaka wa uchaguzi 2025 utasikia amshaamsha kuziongelea hizi Barabara. Bungeni itaongelewa, Tanroad watatuma Surveyors na hata kuweka namba kwenye nyumba zilizopo pembezoni.

Jamaa wanavyojua kuaminisha watu utafikiri inajengwa Kesho. Kwahiyo ikifika kipindi cha uchaguzi utasikia Bajeti imeshatengwa ya Barabara na Mkandarasi ameshaagizwa aanze upembuzi yakinifu. UCHAGUZI UKISHAPITA TU, Haaaahaaaahaaa!!!!

Nakumbuka Mchakato wa Maji katika maeneo hayo hasa Makabe na Msumi yaani kila hatua kana kwamba ni hadi miaka 5 ya Uchaguzi Ipite. Sasa hivi tangu bomba kubwa la maji liwekwe yaani wakazi wa maeneo hayo hawajui nini kinakwamisha wasiunganishiwe Maji.

NCHI YETU HUWA INAPATA MARAISI WAZURI SANA KAMA ILIVYO KWA MAMA. TATIZO KUBWA NI WATENDAJI WANAOAMINIWA . YAANI NINAUHAKIKA MH RAIS ITOKEE AULIZE TU MBONA HII BARABARA HAIJENGWI LAMI AU MBONA BOMBA LIMEWEKWA MUDA MREFU LAKINI WAKAZI HAWANA MAJI, HAPO NDIPO UTAONA WAZIRI NA WATENDAJI WAKE WANAANZA KUKIMBIZANA.

MUDA MWENGINE HUWA NAUMIA SANA HADI NAHISI NAMKOSEA MUNGU. NAHISI HII NGOZI YETU HUENDE NI YULE MTOTO ALIYEMCHEKA BABA YAKE ALIPOMKUTA MTUPU KISHA AKAMLAANI.
 
Hakika inauma sana mkuu.
Makabe, msakuzi na msumi pamesahaulika sana ifike mahali pakumbukwe sasa. Haiwezekani eneo ndani ya jiji kubwa hakuna maji safi tangu nchi ipate uhuru. Kiukweli ni aibu.
Barabara mbovu inaharibu magari yetu kila leo gerage.
 
Siyo kuwekewa mabomba tu mkuu mimi ni mkazi wa Mbezi Makabe nilifunga bomba August mwaka jana kwa gharama kubwa maji yakatoka mfululizo wiki tatu mara yakaingia kwenye mgao kwa wiki mara moja sasa yana miezi miwili hayajatoka.

Ajabu kuanzia police post kurudi madukani maji yanatoka ila kuna namna engineers wa Dawasa wamefanya wanapokea rushwa kutoka kwa wauza maji wa magari ili wasifungue maji area fulani wao watuuzie na ikikaribia tarehe za kusoma Mita wanafungua maji kote usiku wa saa tisa mpaka saa 12 asubuhi wanafunga kesho yake wanapita kusoma metre na kutuma bill kwa wateja.
Aisee hii ni hujuma kubwa sana kuanzia post makabe kwwnda msakuzi hakuna hata hayo mabomba.
 
Wewe umemuona wapi akiililia?Barabara ya Msakuzi kwasababu ya Wingi wa Magari Tanroads wakikarabati wiki mbili inaharibika si bora hayo Mamilioni waanze na Lami kidogokidogo,hii akili nayo hadi waelekezwe na Rais?
Ndio hapo sasa na sikuhz hata huo ukarabati kupitisha grader hawafanyi. Barabara ina mawe yamesimama kama sindano. Vumbi sana. Maji mtu kwa mwezi unatumia zaidi ya 100k.
Walete hzo tozo huku zifanye kazi
 
Shida ninayoiona ipo kwa watendaji wa chini. Ni wababaishaji sana . Sijui kwanini huwa hawatekelezi jambo hadi kuwe na Pressure fulani. Yaani leo hii Mheshimiwa Rais akiwaambia " mnaonaje barabara ikijengwa" utakuta haooo wanaanza utekelezaji. NAJIULIZA NI KWANINI HADI MH RAIS AAGIZE!!

Pia sielewi Waziri Mwenye dhamana ya Barabara anachofanya

Kuhusu Mbunge wa Kibamba Mh Mtemvu kwa kweli kijana wa watu anajitahidi sana. Hata huko Bungeni tunamuona anavyopambana.

Barabara za Mpiji na Msakuzi kutokuwekwa Lami muda mrefu ni suala linalosikitisha sana. Barabara hizo zilistahili kuwekwa lami muda mrefu
Mbunge apambane ikibidi aonane na Raisi tupate maji na barabara. Otherwise kura hapati
 
Barabara ya Msakuzi kwasababu ya Wingi wa Magari Tanroads wakikarabati wiki mbili inaharibika
Nani aliyekudanganya???nina miaka minne Makabe mara ya mwisho kuona barabara zikichongwa kipindi kisichokuwa cha mvua ni mwaka juzi CCM walikuja na mwenge kuzindua kisima cha maji “yasiyokuwepo" baada ya hapo au kabla sijawahi kuona.

Kama nia ya TANROADS ni kuikarabati hiyo barabara kwanini hawakuja kuikarabati kiangazi hiki since may subiri TMA watoe taarifa leo za mvua kubwa Dar ikiwepo uone kama hawakuingiza vifaa site na walivyo wapumbavu utawakuta wakifanya kazi juu ya mvua.

Yaani mvua inanyesha Skaveta zinachoma mafuta juu ya tope linalotembea,vigogo wa TARURA NA TANROADS hizo ndo barabara zao za kupigia hela unatakiwa ujue hilo na hawataki zijengwe watakula wapi zikiwekwa lami?
 
Ndio hapo sasa na sikuhz hata huo ukarabati kupitisha grader hawafanyi.
Mkuu!

Hizo barabara kama hakujatangazwa mvua kubwa au kuonekana dalili za mvua siku za karibuni tusahau.

Stuff vitengo vya barabara Wilaya ya Kibamba hizo ndo barabara zao zakupigia hela,wanavizia mvua kubwa inanyesha kesho wao wanaanza kazi leo mpaka waje wamalize barabara imeshaharibika tena kikifika kipindi cha mvua msimu mwengine wanaziandikia hela nyengine wanapiga,hivyo yaani mbona tumeshazoea kuona hii michezo?
 
Nimewahi sana kujiuliza hili why wapitishe grader kipindi cha mvua kubwa wakati kipindi cha kiangazi wanaacha barabara ikiwa na ubovu mno?

Wapuuzi sana hawa jamaa. Ila yana mwisho haya.
 
Back
Top Bottom