Wakazi wa Mbezi wanaumia sana wakikumbuka ahadi ya Hayati Magufuli

Tatizo watendaji sasahivi sio waoga kabisa. Na hawa ndio wanaomharibia Mama. Natamani Mama awe Mkali kwasababu nature ya mtu mweusi akiona hakuna FIMBO nyuma yake anafanya ujinga atakavyo.
JPM alikuwa na mapungufu yake lakini ktk mazuri aliyokuwa nayo ni pamoja na kujenga nidhamu kwa watendaji wa serikali. TUANGALIE TU JINSI BARABARA YA GOBA ILIVYOJENGWA KWA VIWANGO NI KWASABABU WATU WALIOGOPA KULETA UJANJAUJANJA
 
Vipi mkuu wakazi wa Tarime waliozuiliwa kutumia pesa zilizotolewa na mgodi eti kisa mbunge ni wa CHADEMA
 
Hilo la maji nitalifikisha sehemu husika
 
Kuna maeneo yalishawekewa hadi mabomba ya maji ila maji hayataki yakiwemo maeneo ya kigamboni, makabe, Goba na Msakuzi.
Siyo kuwekewa mabomba tu mkuu mimi ni mkazi wa Mbezi Makabe nilifunga bomba August mwaka jana kwa gharama kubwa maji yakatoka mfululizo wiki tatu mara yakaingia kwenye mgao kwa wiki mara moja sasa yana miezi miwili hayajatoka.

Ajabu kuanzia police post kurudi madukani maji yanatoka ila kuna namna engineers wa Dawasa wamefanya wanapokea rushwa kutoka kwa wauza maji wa magari ili wasifungue maji area fulani wao watuuzie na ikikaribia tarehe za kusoma Mita wanafungua maji kote usiku wa saa tisa mpaka saa 12 asubuhi wanafunga kesho yake wanapita kusoma metre na kutuma bill kwa wateja.
 
Ila anaelipisha watu tozo za kinyonyaji ambazo hazina kichwa wala miguu ndio mtu?
 
Sasa hivi dar hakuna barabara mpya inayojengwa hata kilometa 1 toka sa100 kachukua nchi ..uwezi hata kuwaona trc wakirekebisha reli ndiyo maana majuzi treni imeanguka na kuua watu
 
Kweli waweke lami barabara hiyo tena iende mpaka msakuzi sijui kwa ribaba
Ila kwa lipe pale watu wajiandae kubomolewa kupisha barabara

Ova
 
Tatizo la hii nchi Kuna wataalamu na wachumia tumbo, au tuite Wala rushwa ijapokuwa amesomea kazi husika
 
Na sisi tunataka lami ya kutokea wazo bwawani,kuja hadi msigani [emoji1] itoke mpk scout

Ova
 
Na wa kimara pia aliowabomolea watamkumbuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…