Jidanganye kaka.wana akili sana kuliko unavyo fikiria...
haya unayoyaona ni mipango na kuna nchi zitatoa hela za kutosha kenya itapata kukopeshwa pes nyingi sababu ya hizi vurugu maana bila hivyo wangepata tabu saana kuendesha nchi madeni ni mengi!
ila kupitia maandamano haya kwanza naona matajiri wengi wa kenya hawataitaka siasa tena kenya na wataokuwa madarakani hawata wadharau tena wananchi heshima inajegwa kwa mbilinge mbilinge kama hilo..nchi zote duniani zilizoendelea na tunazozisifia sasa hivi kidemocrasia zilipitia tanuri la moto kama kenya..
mimi binafsi nawasifu sana vijana wa kenya wametuwakilisha vyema east africa na ni hakika kwenye vikao vya viongozi wetu ikulu huko wamekwisha kuonyana kwa yale yanayotokea kenya.!
Kenya sasa hivi ina madeni yasiyo himilifu hakuna anayeweza kuwakopesha kirahisi.
Pia kwa kinachotokea teyari kimeshaanza kufukuza wawekezaji.
Hili linalotokea sasa sio la kwanza,mwaka 2007 unakumbuka kilichotokea kiasi watu walikufa?
Mpaka Uhuru Kenyatta akapelekwa ICC!?
Mbona hakikubadilisha kitu Kenya ilibaki vile vile na mambo yakajirudia yale yale!?
Hiyo siyo mara ya kwanza Kenya kufanyika maandamano na hakikubadilisha kitu.