Nimefuatilia mada kwa umakini sana ila mwisho wa siku bado hoja ya kuwa ili upate passport ni lazima uwe na sababu ya kusafiri nje ya nchi ina mashiko. Mkuu
joto la jiwe ametoa hoja za msingi ambazo upande wa pili wameshindwa kuzijibu zaidi ya kulalamika.
Binafsi najiuliza ya nini kumpa passport mtu asiye na dhumuni la kusafiri nje ya nchi. Passport ndani ya nchi haina kazi kabisa maana kitambulisho cha taifa ndicho chenye kazi hiyo.
Kama mtanzania anataka kwenda nje kwa sababu yoyote ile ni lazima apate passport na ili kupata passport ni lazima ueleze sababu ya kutaka kusafiri, ukisema unataka kwenda kutembea watakuomba uthibitisho wa mwaliko, ukisema unataka kwenda kutibiwa watakuomba barua ya rufaa, ukisema unataka kwenda kutafuta maisha watakuomba uthibitisho wa mwaliko pia au barua ya ajira, ukisema unataka kwenda kusoma watakuomba barua ya udahili wa chuo. Sasa katika yote haya kuna ugumu gani kuambatisha document inayoonyesha dhumuni la safari, tena wao wanataka tu uweke document wala hawatapiga simu huko kutaka kujua uhalali wa hiyo document.
Maoni yangu watanzania tuache kulalamika bila sababu za msingi, tukae tukijua kuwa passport ni kitambulisho tu cha kimataifa kinachoonyesha taarifa za raia wa nchi fulani, hakuna ugumu kupata passport labda uwe mtu ambaye hujakamilika au unayependa konakona. Uhamiaji wanafanya kazi yao vizuri sana, ukifuata taratibu zinazotakiwa utapata passport ndani ya muda mfupi sana na utatimiza lengo la safari yako.