Wakenya Tupeni Uzoefu Wenu Kuhusu Passport

Wakenya Tupeni Uzoefu Wenu Kuhusu Passport

Unamdanganya nani wewe uhamiaji passport walizotoa hazifiki laki tano kwa taarifa zao wenyewe kwa vyombo vya habari na zimo humu

Hao watanzania milioni 1.6 wenye passport za Tanzania umewatoa wapi?
Nimemuambia mwenzako kwamba, kabla hujachangia, jipe muda wa kujifunza, Wacha kutumia hisia na ushabiki.

Wasikilize Diaspora wenyewe kwenye mitandao, fuatilia michango ya wabunge bungeni kuhusu "Dual citizenship". Hoja Yao kubwa ni kwamba watanzania zaidi ya 1.5M wapo nje ya nchi, kwahiyo wanataka kutambuliwa Kama ni mkoa wa nchi uliopo nje ya mipaka ya Tanzania na wanayo haki ya kusogezewa huduma Kama kupiga kura, wingi wao ndio kigezo Cha kuomba kupata uraia pacha
Wacha kutikisa mbuyu, yatakayotikisika ni matako yako tu.
 
Kama ulivyo wewe mkuu, japo unajifanya uko na akili nyingi. Mimi ni mzalendo wa kweli, nilisoma vyuo vya Ulaya, lakini nilirudi kutumikia nchi yangu.
Hongera kwa kuthibitisha kuwa watu wenye fikra za UJAMAA ni wabinafsi sana.

Umeshaenda Ulaya lakini u naona nongwa kwa Watanzania wengine kwenda.

Ili iweje?
 
Hongera kwa kuthibitisha kuwa watu wenye fikra za UJAMAA ni wabinafsi sana.

Umeshaenda Ulaya lakini u naona nongwa kwa Watanzania wengine kwenda.

Mkuu hata ulie vipi, kamwe halikubaliki kujichukulia passport kiholela, hii nchi sio "failed state", lazima tuwe na Sheria, kanuni na taratibu zetu zenye kulinda usalama, heshima na uaminifu wa nchi yetu.

Ili iweje?
Mkuu, nilikwenda nikiwa na sababu zenye kukubalika, sikuenda kwenda kuzurura mitaani.
 
Mjibu hivi?, Ni taifa gani linalotoa passport huku likijua wazi kwamba hao raia wake wanakwenda kufanya uhalifu huko nje ya nchi?
Kuna mtu anaomba passport halafu akaandika sababu ya kusafiri ni kwenda kufanya uhalifu nje?
 
Taifa gani halina wezi ughaibuni?
Majibu ya mwamba haya hapa chini..!!

1683879643325.png

CC joto la jiwe
 
Hongera kwa kuthibitisha kuwa watu wenye fikra za UJAMAA ni wabinafsi sana.

Umeshaenda Ulaya lakini u naona nongwa kwa Watanzania wengine kwenda.

Ili iweje?
Ulaya aliyoenda itakuwa zile ya nchi za kikomunisti

Hao ndio huongoza kwa roho mbaya
 
Kuna mtu anaomba passport halafu akaandika sababu ya kusafiri ni kwenda kufanya uhalifu nje?
Mhalifu anajukikana kwa kumtizama usoni au anakuwa mhalifu baada ya mahakama iwe ya Tanzania au nje kumthibitisha kuwa mhalifu?

Kwa hiyo mnawanyima watu passport kwa kuwaangalia tu usoni kama waganga wa kienyeji kuwa wakienda nje wanaenda kufanya uhalifu

Kuwa na watu wenye mawazo kama haya ofisi za Serikali sio sahihi

Serikali iwe inaajiri.watu sahihi na ku wa promote watu sahihi
 
Mimi nilikua na sababu za msingi kwenda Ulaya, huko nje Kuna watanzania zaidi ya 1.6M wanaishi kihalali na wamepewa passport, Kila siku watanzania kibao wanaokwenda China kufanya biashara na kurudi, nenda uhamiaji ona idadi ya passport zinazotolewa kwa siku, watu wenye sababu za msingi, huwezi kunyimwa passport, ila passport sio chupi, lazima itolewe kwa kuidhibiti.
Ni Korea ya Kaskazini pekee ndiyo inayoweza kukubaliana na mtazamo wako.
 
Kuna mtu anaomba passport halafu akaandika sababu ya kusafiri ni kwenda kufanya uhalifu nje?
Hivi wewe uko na akili timamu kutoa passport (exit visa) kwa kibaka wa pale Manzese bila kumuuliza lengo la safari yake ni nini?
 
Mhalifu anajukikana kwa kumtizama usoni au anakuwa mhalifu baada ya mahakama iwe ya Tanzania au nje kumthibitisha kuwa mhalifu?

Kwa hiyo mnawanyima watu passport kwa kuwaangalia tu usoni kama waganga wa kienyeji kuwa wakienda nje wanaenda kufanya uhalifu

Kuwa na watu wenye mawazo kama haya ofisi za Serikali sio sahihi

Serikali iwe inaajiri.watu sahihi na ku wa promote watu sahihi
Watu Kama wewe mtaendelea Sana kuwa jobless mitaani, serikali haifanyi kazi kwa maneno, serikali inafanya kazi kwa maandishi, leta barua ya mwaliko, au onyesha ushahidi wa kimaandishi kuonyesha sababu ya safari Ili upewe exit visa(Passport)
 
Hivi wewe uko na akili timamu kutoa passport (exit visa) kwa kibaka wa pale Manzese bila kumuuliza lengo la safari yake ni nini?
Kibaka alishahukumiwa na mahakama ?una hati ya mahakama ya kuthibitisha kuwa yeye kibaka?

Mifisadi na mijizi mikubwa hata inayotajwa ripoti za CAG mingine hadi jela imeenda mbona ina passport mlizowapa ?

Kama mifisadi certified ina passport kibaka mnashindwa nini kumpa?

Omba msamaha huwezi ita mtu kibaka wakati huna hati ya mahakama kuthibitisha hilo
 
Ni Korea ya Kaskazini pekee ndiyo inayoweza kukubaliana na mtazamo wako.
Mkuu, wewe bado ni mtoto mchanga Sana, mnaishi kwa hisia na nadharia, hakuna nchi inayotoa passport bila sababu, Kama zipo basi ni nchi chache Sana, passport sio chupi mkuu.
 
Kibaka alishahukumiwa na mahakama ?una hati ya mahakama ya kuthibitisha kuwa yeye kibaka?

Mifisadi na mijizi mikubwa hata inayotajwa ripoti za CAG mingine hadi jela imeenda mbona ina passport mlizowapa ?

Kama mifisadi certified ina passport kibaka mnashindwa nini kumpa?

Omba msamaha huwezi ita mtu kibaka wakati huna hati ya mahakama kuthibitisha hilo
Punguza hasira mkuu, ila ukweli utabaki ukweli, kwamba bila kuthibitisha sababu ya safari, hakuna Passport itatolewa.
 
Back
Top Bottom