Mkuu, wewe ndio unawashangaza watu, inaonekana hujatembea na Wala hujui jinsi nchi zonavyojiendesha duniani, hakuna nchi yoyote inayotoa "Government documents" kwa urahisi, Wacha passport, hata leseni ya udereva tu kuipata ni ngumu Sana.
Hebu nenda Ulaya ukaombe leseni ya udereva uone hilo sakata lake. Kwahiyo mkuu, hizi serikali zote zinazodhibiti passpot zao unadhani ni wajinga au hawajui kitu, ila ninyi watu wachache ndio wenye akili?.
Mkuu, tatizo hujazunguka Dunia, na Wala hujui "International diplomacy" inavyofanya kazi. Passport ni document yenye kubeba utu wa Taifa nje ya nchi, mtu yeyote aliyebeba passport ya nchi lazima apewe heshima inayoendana na nchi yake huko ktk nchi anakokwenda, ni wajibu wa balozi zetu huko nje kuhakikisha mtu yeyote mwenye passport ya Tanzania anatetewa na kulindwa haki zake, huwezi kuwapa watu wa hovyo hovyo passport.
Mkuu, Kama nilivyokijibu hapo juu, huu uamuzi wa kuidhibiti passport umepitishwa na kukubalika hapa nchini na kupitishwa na vyombo vyote vyenye majukumu ya kusimamia Sheria za nchi na haki za binadamu. Sasa Kama wewe unadhani una akili nyingi kuwazidi hao wote waliopitisha na kusimamia jambo hili, basi Tanzania sio nchi sahihi kwako. Ila unayo haki ya kutoa mawazo yako, na serikali inayo haki ya kufanya vile inavyodhani ni sahihi.