Mkuu, serikali lazima iwe na uwezo wa kudhibiti watu wake kutoka nje ya nchi, Kama ambavyo ni lazima kudhibiti raia wa nchi nyingine kuingia nchini kwake, hakuna serikali yoyote yenye kuacha watu wake hasa kwa hizi nchi changa ambazo watu wake wengi hawana ajira, ni rahisi Sana hawa vijana kwenda na kufanya uhalifu katika nchi za watu, sio sifa kwa nchi kuonekana raia wake ndio wanafanya uhalifu kwa wingi katika nchi za watu wengine.
Nitakubaliana na wewe Kama utailaumu serikali kwa kushindwa kuwasaidia vijana wake kuweza kujiajiri lakini sio kufikiria kuwapa passport kirahisi Ili wakajazane South Afrika kuuza madawa na kuvunja Nyumba za watu.
Mkuu, hao wanaohitaji na kukosa passport hawazidi laki 5, ni chini ya 0.5% ya watanzania wote. Hapa JF sidhani Kama tunazidi watu laki Moja, na wanaolalamika kuhusu passport hawazidi hata elfu 1.
Mkuu, nchi lazima ifanye kazi kwa kutumia taarifa zilizofanyiwa kazi. Bei ya Passport Moja ni zaidi ya Tsh 50,000 ni "source nzuri sana ya kupata pesa kwa uhamiaji, hawana sababu yoyote ya kuzikataa pesa nyingi kiasi hicho, wangekuwa wabinafsi wangeamua kuzitoa hovyo passport Ili wakusanye mapato, lakini ni hatari Sana kwa usalama na heshima ya nchi, zingeangukia mikononi mwa raia wa nchi nyingi na mwisho passport yetu ingepoteza thamani.
Mkuu, Passport ya Tanzania enzi za Nyerere ilikua na nguvu sana, lakini kadri miaka inavyozidi kwenda inapoteza nguvu kutokana na vitendo vyetu vya kujihusisha na hasa madawa ya kulevya na vijana wetu kushiriki ktk mambo maovu ukiwemo ugaidi, lazima passport idhibitiwe kwa nguvu zote