GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
- Thread starter
- #41
Sidhani kama kuna uhusiano wo wote kati ya hali ya usalama wa Kenya na uhuru wa raia wake kwenda ng'ambo.Ndio sababu Kenya is ranked poorly on security, Globally Tanzania is ranked position 54, while Kenya 125.
Tishio la kiusalama linaweza likachangiwa na kupakana na nchi zenye vita kama Sudan na Somalia. Passport hazihusiki kabisa.
Nionavyo mimi, kwa kuwarahisishia raia wake mchakato wa passport, siyo kwamba kumeisaidia tu kiuchumi, bali pia kiusalama.
Unajua maamuzi ya mtu mwenye njaa yalivyo? Kama ajira za ndani hazitoshelezi, na hujawatengenezea watu wako mazingira ya kwenda kutafuta kwingineko, itakuwa unajitengenezea bomu litakalokuja kukulipukia.
Kwa kuwatengenezea watu wake mazingira ya kuweza kwenda nchi zingine kirahisi, Kenya wameua ndege wawili kwa jiwe:
1. Inanufaika kiuchumi
2. Imedumisha usalama wa ndani