Kwa mtu binafsi ni ID ila kwa serikali Kuna mambo mengi sana, Kumbuka raia akiwa nje ya nchi serikali inapoteza udhibiti juu yake lakini bado serikali Ina wajibu wa kumlinda Kama ilivyotokea Sudan.
Sudan kulikua na raia wa USA zaidi ya 13,000, pamoja na nguvu za kiuchumi za USA lakini hadi Leo haijaweza kuwasaidia wote, bado wanapambana kuwaondoa.
Raia anapokua nje ya nchi anakua anawakilisha nchi yake, angalia nchi ya Nigeria ilivyoharibu mahusiano yake ya kidiplomasia na nchi zingine duniani kwasababu tu ya tabia ya raia toka Nigeria wanavyojihusisha na vitendo haramu, nchi nyingi hivi Sasa hazitoi visa kwa raia toka Nigeria.
Siyo jukumu la Serikali kudhibiti raia wake aliye nchi nyingine. Huyo mtu akiwa na shida, yeye ndiye anayepaswa kuripoti ubalozini, siyo Serikali yake.
Serikali yake haina mamlaka juu ya mtu wake aliye kwenye nchi nyingine. Lakini pia ni vyema ifahamike kuwa mafanikio yanaambatana na ujasiri wa kutake risk. Mwoga wa kutake risk siyo rahisi apate mafanikio makubwa. Kama mtu yupo tayari kutake risk, Serikali isimwekee kikwazo. Mbona Huwa haiwazuii wanajeshi kwenda penye vita kunapotokea na uhitaji? Si unafahamu mtu anayeenda vitani Kuna mambo matatu hivi yatakayokuwa yakimkabili? Ama arudi salama, au ajeruhiwe au hata kupoteza maisha. Lakini bado kukitokea uhitaji, Jeshi likiagizwa liende vitanie, litatii. Sasa kwa nini sera za Serikali iwe kikwazo kwa "wapambanaji" wanaotaka kwenda kujaribu maisha sehemu zingine?
Kwamba Wanaigeria wamefanya uhalifu uliopelekea baadhi ya nchi kukataa kuwapa viza si hoja. Mbona Kenya, pamoja na kuwa ndiyo nchi inayoongoza Afrika Mashariki kwa raia wake wengi kuwa nchi za nje, bado passport yao ina nguvu kuizidi ya Tanzania? Hata katika katazo lililotolewa na Dubai mwaka huu, la kukataa kupokea raia wa baadhi ya mataifa, Kenya si miongoni mwao. Dubai kuna raia wengi wa Kenya kuxidi raia kutoka nchi nyingine yo yote ya Afrika Mashariki.
Labda nikutajie na hizo nchi, hasa za Afrika, ambazo raia wa hizo nchi hawatakiwi Dubai kwa sasa(labda kama wameshabadilisha):
Kuna Nigeria, Ghana, Uganda, Sierra Leone, Sudan, Cameroon, Liberia, Burundi, Republic of Guinea, Gambia, Togo, Congo D. R. C., Rwanda, Burkina Faso, Guinea Bissau, Comoros, and the Dominican Republic.
Umeona? Pamoja na Wakenya wengi kuwepo Dubai, hawajahusishwa na zuio la kuingia Dubai.
Kama Wakenya wameweza, hata Watanzania wataweza.