Unachekesha sana, yule ni Mbunge wa bunge la EU, sio mwenyekiti kama unavyosema, ni mbunge wa kawaida kama walivyo wabunge wengine, aliuliza swali, hiyo haina maana kwamba kila alichokisema ni sahihi, ndio sababu aliuliza swali kutaka kujua, usiogope kwasababu ni mzungu ukadhani kila alichokisema ni sahihi:
Pesa zilizotolewa hazikuwa za kupambana na kuenea maambukizi ya Corona, bali zilikua ni kusaidi Tanzania katika kukabiliana na athari za kiuchumi zilizosababishwa na tatizo la Corona duniani, Je unapinga kwamba Tanzania pamoja na kutoathirika sana kiafya lakini uchumi wake umeathiriwa na Corona?.
Tafuta taarifa kuhusu dhumuni la kutolewa kwa zile pesa kabla ya kumsikiliza yule mlevi, hakuna uhusiano wowote wa zile pesa na kuzuia maambukizi, au kuwepo/kutokuwepo kwa Corona, nchi zote duniani zimeathirika kiuchumi hata zile ambazo hadi leo hazijaripoti kisa hata kimoja cha Corona.