TANZIA Wakili Alute Lissu Mughwai (kaka wa Tundu Lissu) afariki Dunia

TANZIA Wakili Alute Lissu Mughwai (kaka wa Tundu Lissu) afariki Dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Screenshot 2026-11-01 090448.png

Alute.jpg

Lissu-na-Alute-Mugwai.jpg


​
Wakili Allute Lissu Mughwai ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amefariki usiku wa kuamkia Leo Novemba 1, 2026.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Dada yake aitwaye Rose Masesa pindi alipozungumza na Jambo TV.

Jambo TV ilipotaka kufahamu chanzo cha kifo chake Rose ametueleza kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza lolote huku akitueleza kuwa msiba upo jijini Arusha.

"Ni taarifa za kweli msiba upo Arusha na mimi naelekea huko" alisema Rose kwa ufupi.


===
Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, Brenda Rupia amethibitisha kutokea kwa msiba huu, amesema "Ni taarifa ya kweli, msiba umetokea na sasa viongozi wetu wanaelekea gerezani kuonana na Mwenyekiti baada ya hapo tutatoa taarifa rasmi na kamili"
 
Screenshot_20261101_082744_Instagram.jpg


Picha hii ilichukukiwa siku tano zilizopita alipohojiwa na That Boy Khalifa wa The Chanzo. Je ni kweli kafariki ? Nini chaweza kuwa chanzo cha kifo? Michezo mibaya ya kisiasa? Au stress ya mdogo wake kusubiri hukumu ya kifo dhidi ya kesi ya uhaini huku akina Heche na Maria na Mange wakikataa maridhiano
 
View attachment 3702462 Picha hii ilichukukiwa siku tano zilizopita alipohojiwa na ThatBoyKhalifa wa The Chanzo. Je ni kweli kafariki ? Nini chaweza kuwa chanzo cha kifo? Michezo mibaya ya kisiasa? Au stress ya mdogo wake kusubiri hukumu ya kifo dhidi ya kesi ya uhaini huku akina Heche na Maria na Mange wakikataa maridhiano
Kama si TEETH kuhamisha goli na kutuondoa kwenye FOCUS basi Poleni ndugu ,jamaa na marafiki.
 
Nilifuatilia mahojiano yake na mwandishi wa habari Mburushi.
Ukimwangalia vizuri alionekana bado mgonjwa na alikuwa akichelewa sana kujibu maswali simple.
Katika mahojiano yake alibainisha yeye ni mwanaccm lakini CCM ile ya Mwl Nyerere si hii ya leo.

Ikiwa ni kweli kafa basi tunamwomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ampokee na kumweka mahali anapostahili.

RIP Alute Lissu.
 
Apumzike kwa amani.

Lissu anakosa haki ya kwenda kumzika kaka yake huku akiwa anasubiri hukumu ya kesi ya uongo, haya ni mapigo mawili kwa wakati mmoja.

Naamini hiyo ndio njia wanayoipitia wenye kuipenda na kujua kuitetea haki, Mungu amjalie nguvu ashinde haya majaribu anayopitia kwa wakati huu.

Umefika wakati sasa wa kumuunga Lissu mkono kwa vitendo, nikiandika kwa vitendo naamini ninaeleweka vizuri.
 
Back
Top Bottom