Hakika sote ni wa mwenyezimungu na kwake tutarejea 🙏Wakili Allute Lissu Mughwai ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amefariki usiku wa kuamkia Leo Novemba 1, 2026.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Dada yake aitwaye Rose Masesa pindi alipozungumza na Jambo TV.
Jambo TV ilipotaka kufahamu chanzo cha kifo chake Rose ametueleza kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza lolote huku akitueleza kuwa msiba upo jijini Arusha.
"Ni taarifa za kweli msiba upo Arusha na mimi naelekea huko" alisema Rose kwa ufupi.
Kufanya nini tena? Au ndio sababu ya kifo?Huyu Godbless Lema ni mtu hatari sana
Duh unaweza kumchukia mtu lkn si jambo jema kumsingizia mtu.Huyu Godbless Lema ni mtu hatari sana
Huyu alikuwa mwana CCM mtiifu isipokuwa tuu damu ni nzito kuliko maji.View attachment 3702462
Picha hii ilichukukiwa siku tano zilizopita alipohojiwa na ThatBoyKhalifa wa The Chanzo. Je ni kweli kafariki ? Nini chaweza kuwa chanzo cha kifo? Michezo mibaya ya kisiasa? Au stress ya mdogo wake kusubiri hukumu ya kifo dhidi ya kesi ya uhaini huku akina Heche na Maria na Mange wakikataa maridhiano
May his soul rest easy in peace. Amen.Wakili Allute Lissu Mughwai ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amefariki usiku wa kuamkia Leo Novemba 1, 2026.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Dada yake aitwaye Rose Masesa pindi alipozungumza na Jambo TV.
Jambo TV ilipotaka kufahamu chanzo cha kifo chake Rose ametueleza kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza lolote huku akitueleza kuwa msiba upo jijini Arusha.
"Ni taarifa za kweli msiba upo Arusha na mimi naelekea huko" alisema Rose kwa ufupi.
===
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Brenda Rupia amethibitisha kutokea kwa msiba huu, amesema "Ni taarifa ya kweli, msiba umetokea na sasa viongozi wetu wanaelekea gerezani kuonana na Mwenyekiti baad aya hapo tutatoa taarifa rasmi na kamili"
"Katika mahojiano yake alibainisha yeye ni mwanaccm lakini CCM ile ya Mwl Nyerere si hii ya leo", huenda uasi huu ndio uliomuua, hakuna tofauti na kupotea kwa Nchimbi, ukiikana CCM wanachomoa fyuzi.Nilifuatilia mahojiano yake na mwandishi wa habari Mburushi.
Ukimwangalia vizuri alionekana bado mgonjwa na alikuwa akichelewa sana kujibu maswali simple.
Katika mahojiano yake alibainisha yeye ni mwanaccm lakini CCM ile ya Mwl Nyerere si hii ya leo.
Ikiwa ni kweli kafa basi tunamwambo Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ampokee na kumweka mahali anapostahili.
RIP Alute Lissu.
Umeeleweka vizuri sana katika lugha nyepesi. Sio kwetu raia wa kawaida tuu hata Madaktari, wahandisi, manesi, WANAJESHI, madereva nk nk.Apumzike kwa amani.
Lissu anakosa haki ya kwenda kumzika kaka yake huku akiwa anasubiri hukumu ya kesi ya uongo, haya ni mapigo mawili kwa wakati mmoja.
Naamini hiyo ndio njia wanayoipitia wenye kuipenda na kujua kuitetea haki, Mungu amjalie nguvu ashinde haya majaribu anayopitia kwa wakati huu.
Umefika wakati sasa wa kumuunga Lissu mkono kwa vitendo, nikiandika kwa vitendo naamini ninaeleweka vizuri.
Alivyokuwa anaongea tu,nadhani hakuwa vizuri kiafya..Hivi,si juzi tu alihojiwa na mwanahabari kuhusu kushawishiwa wamuambie Tundu Lissu amuombe msamaha malkia wa Sheba ili aachiwe huru?Kwamba alikuwa mgonjwa?Kwamba ni natural death?Kwambaaaa.....!?