Wakili: Deni la Membe kwa Musiba liko palepale

Wakili: Deni la Membe kwa Musiba liko palepale

Ndie alie kashifiwa??
Jaribu kuwa unajisomea Sheria peke yako update japo abc zake utanishukuru siku nyingine siyo leo!
Hata mtaani wadaiwa wanalipa madeni kwa msimamizi wa mirathi! Au wewe hujawahi kufiwa au kushiriki shughuli za msiba?
 
Unatafuta expert opinion kwa kumuuliza wakili ambae marehemu alikuwa mteja wake kwenye kesi ya madai na si ajabu malipo yake ni percentage kwenye hiyo award, halafu utegemee neutral response.

Hizi media zetu nazo dah

Ukitaka expert opinion tafuta mtaalamu asie na uhusiano na hiyo case aliebobea kwenye maswala ya tort in general, na awards za defamation zinalenga kusawazisha nini kwa claimant.

Technically hayo madai hayapo tena, kwa sababu mtu pekee alietakiwa kufidiwa ni Membe.
 
Huyo wakili na yeye soon atajikutaa Yuko mbinguni na membe + magufuli wanaimba nyimbo za sifa na kuabudu ...
 
Unatafuta expert opinion kwa kumuuliza wakili ambae marehemu alikuwa mteja wake kwenye kesi ya madai na si ajabu malipo yake ni percentage kwenye hiyo award, halafu utegemee neutral response.

Hizi media zetu nazo dah

Ukitaka expert opinion tafuta mtaalamu asie na uhusiano na hiyo case aliebobea kwenye maswala ya tort in general, na awards za defamation zinalenga kusawazisha nini kwa claimant.

Technically hayo madai hayapo tena, kwa sababu mtu pekee alietakiwa kufidiwa ni Membe.
Kasome vizuri
 
Wakili Jonathan Mdeme, aliyekuwa akimwakilisha mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Bernard Membe (69) kwenye kesi dhidi ya mwanahabari Cyprian Musiba, amesema deni la waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje kwa Musiba liko palepale na msimamizi wa mirathi ataendelea alipoishia.

Membe ambaye alikuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne, amefariki leo Ijumaa Mei 12, 2023 katika Hospitali ya Kairuki iliyopo Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

Itakumbukwa kuwa Oktoba 28, 2021, Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam ilimuamuru Musiba anayejitambulisha kama mwanaharakati huru kumlipa Membe fidia ya Sh6 bilioni.

Katika kesi hiyo namba 220 ya mwaka 2018, Membe alimdai Musiba fidia ya Sh10.3 bilioni kwa madai ya kumkashfu kupitia magazeti yake ya Tanzanite.

Akizungumza na Mwananchi leo Mei 12, 2023 kuhusu hatima ya deni hilo, Wakili Mndeme amesema madai dhidi ya Musiba hayatafutika kwa sababu msimamizi wa mirathi ataendelea kufuatilia madeni ya marehemu.

“Katika makosa ya jinai, mtuhumiwa akifariki kesi inaisha hapo, katika makosa ya madai ni tofauti. Anateuliwa msimamizi wa mirathi ya marehemu halafu anavaa viatu vya marehemu kukusanya madeni na mapato kama yapo.

“Kama madeni yanalipwa, kama ni mapato yanagawanywa kwa mrithi halali kwa maana mke na watoto. Kwa hiyo kesi ya madai dhidi ya Musiba ni shauri la madai hivyo halitafutika kwa sababu msimamizi wa mirathi ataendeleza pale alipoishia,” amesema Mndeme.

Amesema kesi iko katika hatua ya kukazia hukumu au utekelezaji wa hukumu na maombi yaliwasilishwa mwaka 2022 na kupewa namba 26 ya mwaka 2022 na Mahakama ya Kuu Dar es Salaam.

Wakili huyo wa Membe amesema alishateuliwa dalali kuendelea na kazi kukazia hukumu.

Kuhusu Membe

Akizungumzia kifo cha mteja wake huyo, Mndeme ameeleza kusikitishwa akisema alikuwa ni mtu mwenye msimamo na kujiamini.

“Mimi sijapoteza tu mteja, bali nimepoteza rafiki yangu na jana nimezungumza naye na kushauariana naye mambo mengi.

“Nimejifunza kufanya kazi na mtu aliyefanya kazi serikalini. Kujiamini na kusimamia msimamo, ukitaka kufanya jambo unalifanya kwa kujiamini na mteja wangu alikuwa anajiamini na kuendesha kesi miaka mitatu katika mazingira magumu,” amesema Wakili Mndeme.

Amesema Membe alikuwa mtu anayepokea ushauri na kwamba hakuwa mbishi na kwamba alikuwa na uwezo na mwenye kumbukumbu sawia na uelewa mkubwa.

MWANANCHI
Jamaa maisha yake yote kaishi kama mfalume,mwisha sasa hanaitwa maiti hana tena thamani kwa mtu yoyote yule kinacho subiliwa ni kuingizwa kwenye shimo na kufukiwa na kifusi cha tani 10 habari yake hishie hapo
 
Ongeza maarifa hapo mkuu
 
Attachments

  • Screenshot_20230513-090906.png
    Screenshot_20230513-090906.png
    63.6 KB · Views: 4
naomba nifahamu kiwango chako cha elimu kwanza
Sina elimu ya kukariri ili kupata ajira mkuu!
Shauri la Membe ilikuwa madai ya fidia binafsi kutokana na kukashifiwa (compensation for injury of reputation). Hivyo, anayestahili fidia akifa na madai yake yanakufa. Kisheria tuna msemo (maxim) unasema “Actio personalis moritur cum persona” (“A personal action 🥸🥸dies with the person”). Kwa hiyo madai kama hayo hayawezi kuwa sehemu ya mirathi ya marehemu.🥸
 
Jaribu kuwa unajisomea Sheria peke yako update japo abc zake utanishukuru siku nyingine siyo leo!
Hata mtaani wadaiwa wanalipa madeni kwa msimamizi wa mirathi! Au wewe hujawahi kufiwa au kushiriki shughuli za msiba?
Shauri la Membe ilikuwa madai ya fidia binafsi kutokana na kukashifiwa (compensation for injury of reputation). Hivyo, anayestahili fidia akifa na madai yake yanakufa. Kisheria tuna msemo (maxim) unasema “Actio personalis moritur cum persona” (“A personal action 🥸🥸dies with the person”). Kwa hiyo madai kama hayo hayawezi kuwa sehemu ya mirathi ya marehemu.🥸
 
Hakuna haja ya matusi na povu tuelimishane kistaarabu bro! Shauri la Membe ilikuwa madai ya fidia binafsi kutokana na kukashifiwa (compensation for injury of reputation). Hivyo, anayestahili fidia akifa na madai yake yanakufa. Kisheria tuna msemo (maxim) unasema “Actio personalis moritur cum persona” (“A personal action 🥸🥸dies with the person”). Kwa hiyo madai kama hayo hayawezi kuwa sehemu ya mirathi ya marehemu.🥸
Screenshot_20230512-181542_Instagram.jpg

Usititoe kwenye reli
 
Hakuna haja ya matusi na povu tuelimishane kistaarabu bro! Shauri la Membe ilikuwa madai ya fidia binafsi kutokana na kukashifiwa (compensation for injury of reputation). Hivyo, anayestahili fidia akifa na madai yake yanakufa. Kisheria tuna msemo (maxim) unasema “Actio personalis moritur cum persona” (“A personal action 🥸🥸dies with the person”). Kwa hiyo madai kama hayo hayawezi kuwa sehemu ya mirathi ya marehemu.🥸
Kwa kuwa Marehemu alishaprove case yake na kupata decree.That decree is a property and that property survive and passes to the surviving.Hivyo hata kama Musiba akiappeal au asiappeal the right of action never abate.In short deni liko pale pale tofauti ni anayesimamia hatakuwa Membe bali mwakilishi wake dunia/Personal Legal representative.
 
Tusiandikie mate mkuu!
 
Back
Top Bottom